Pole sana ndugu kwa yaliyo kupata, naomba niseme kitu hapa.1 unasema Mbwa walipewa chakula na tunahisi ilikuwa sumu, nani huwa anawapa chakula? na huwa unawapia chakula nnje?2 Nyumba yako imezungushwa ua?3 Huwa unawafunguwa wote kwa pamoja wakati wa kulinda?
USHAURI:
1, Nakuomba usiwe unalishia chakula Mbwa nnje ya banda lao
2, Nakuomba kama Nyumba yako imezungushiwa ua usiwe unawafungulia Mbwa wote kwa pamoja, ukitoa mmoja ndani, 2 wabakie inakuwa rahisi mmoja akipewa sumu wengine watabweka mpaka utaamka tu, maana Mbwa wakiona hatari kuna mlio wanabadilika ufokaji lazima utaamka.
3, Mtu wa kuwalisha awe mmoja ikiwezekana na wakati muupangilie itawasaidia kutokula hovyo.
4, Mbwa uwe unawatarishia chakula kuwapikia maana cha kuchukuwa hotelini huwa ni hatarishi kwa ulaji wa Mbwa maana anapata harufu nyingi tofauti.
5, Ukiwa na nafasi unaweza kusimamia mwenyewe kumwongoza Mbwa asile vyakula vya kuotoka chini, ni somo rahisi sana hilo.
Kwaleo tuishie hapo kwanza. Mbarikiwe nyote. 🙏