Msaada: Mbwa wangu amebakiza saa machache afe

Msaada: Mbwa wangu amebakiza saa machache afe

Its Pancho

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Posts
15,966
Reaction score
26,404
Wakuu,

Mbwa Nilikuwa nao watatu ila cha ajabu wawili wamekufa jana kwa wakati mmoja, nimewazika leo na huyu mmoja aliebaki nae ni hivyo hata hatikisiki na hana nguvu za kusimama.

Dalili zao wote walikuwa wanatoa mapovu mdomoni, wakisimama wanaanguka, na hata kula wakawa hawawezi na walikuwa wana wadudu lakini dawa niliwapatia jana, huyu aliebaki tumbo limevimba,

Nilikuta wamepewa chakula lakini nilipowafungulia wakawa hawawezi kutembea wanaanguka na mapovu wanatoa.

UPDATE >>>
Mida hii saa 19: 00 mbwa wangu huyu aliebaki amefariki, ..
Mlinzi pekee ambae amebaki nae ndio amekwenda, dalili zake zilikuwa zile zile na alikuwa anaharisha pia kama damu hivi,..
Mbwa watatu wamekufa kwa siku mbili wamepishana masaa tu.

Nawashukuru mlionipa ushauri wa kila namna..
 
Hizo ni dalili za food poisoning, au wameumwa na nyoka. Kama ni sumu labda kuna mtu amewarushia nyama yenye sumu, hivyo imarisha ulinzi, hujui ana lengo gani.

Na kama sumu imeingia mwilini ni ngumu sana kumtibu kwa alipofikia,
 
Hizo ni dalili za food poisoning, au wameumwa na nyoka. Kama ni sumu labda kuna mtu amewarushia nyama yenye sumu, hivyo imarisha ulinzi, hujui ana lengo gani.

Na kama sumu imeingia mwilini ni ngumu sana kumtibu kwa alipofikia,
Mkuu unaanza kunifungua akili sasa
Kama ndio ingekuwa minyoo wasingekufa kwa pamoja
Kwahiyo dalili hizo ni walipewa sumu au nyoka, maana sidhani kama minyoo inafanya mbwa atoe mapovu
 
Nimegundua kweli ilikuwa sumu Wale wawili nimekuta wamekauka asubuhi
Sasa sijui nani kawapa sumu maana hawa majirani zangu wananichukia sana toka zamani
Kama unachukiwa na majirani hiyo ni hatari. Wanaweza kukuua hata wewe. Sababu ni nini mpaka ukawa vibaya nao?
 
Iliwahi nitokea na mimi ,kumbe wezi wana mipango yao walimpa sumu mmbwa wiki moja kabla maana dog alikua kikwazo kwao maana alikua Mkali sana wezi walipokuja walinipukutisha kuku 100+.....mmbwa nae alikufa
 
Nakushauri.. Toa taarifa Alaka kwa mjumbe au mwenyekiti wa kitongoji..

Something must be wrong.. Imarisha ulinzi hiyo hali haingii akilini..
 
Back
Top Bottom