Msaada: Miguu kutoa harufu

Msaada: Miguu kutoa harufu

Ninoma

Member
Joined
Aug 29, 2021
Posts
9
Reaction score
5
Habari za midaa wakuu, ninashida ya miguu & viatu kutoa harufu baada ya kuvaa, hata nikivaa masaa 6 baada ya kuvua lazima vitoe harufu.

Mwenye anajua tiba naomba maelezo
 
Hua unasafisha miguu yako kwa unadhifu na kuisugua vizuri?
 
Hua unakausha miguu kabla ya kuvaa viatu au soksi?
 
Chukua jiwe uwe unasugua miguu sehemu zote.dead skin kwenye miguu ndio hutoa harufu.hakikisha kila siku unasugua utakuja kunishkuru
 
Jaribu kuchemsha maji ya vuguvugu, yawe kama lita tatu au nne, weka kwenye beseni, weka chumvi vijiko vya chai 4 au 5, then kamulia limao nne na mbegu zake halafu kaa iloweke miguu humo kwa dakika 5 hadi 10 , halafu osha miguu yako hadi katikati ya vidole kwa maji hayohayo, fanya hivo mara moja kwa wiki au mbili,
 
Chukua jiwe uwe unasugua miguu sehemu zote.dead skin kwenye miguu ndio hutoa harufu.hakikisha kila siku unasugua utakuja kunishkuru

Wakati unasugua miguu ufuate huu ushauri wa kutumia jiwe wanauza jero tu
 
Kama itashindikana zaidi nenda hospital labda zinakua fangasi sasa
 
Jaribu kuchemsha maji ya vuguvugu, yawe kama lita tatu au nne, weka kwenye beseni, weka chumvi vijiko vya chai 4 au 5, then kamulia limao nne na mbegu zake halafu kaa iloweke miguu humo kwa dakika 5 hadi 10 , halafu osha miguu yako hadi katikati ya vidole kwa maji hayohayo, fanya hivo mara moja kwa wiki au mbili,
Asante mkuu
 
Ndio mkuu . lakini shida bado ipo
Harufu huletwa na hizo dead skin ukisugua na jiwe na kuwa unabadili vitu na soks kwa wiki tatizo linaisha unasahau.mimi nilikuwa na hiyo tatizo dokta flan mzungu akanipa hio idea.hadi leo ni stori
 
Harufu huletwa na hizo dead skin ukisugua na jiwe na kuwa unabadili vitu na soks kwa wiki tatizo linaisha unasahau.mimi nilikuwa na hiyo tatizo dokta flan mzungu akanipa hio idea.hadi leo ni stori

Yale mawe wanauza jero, tena wakati unasugua miguu usipake sabuni , tumia maji tu na jiwe ndio dead skin inatoka kiwepesi, sabuni unapaka baadae kama kung’arishia tu miguu
 
Tuanzie kwanza kwenye soksi. Una pair ngapi za soksi (kuwa mkweli hata kama unayo moja, ukisema uongo hautaweza kusaidika).

Ukishanambia idadi ya soksi zako nambie kuhusu style ya uvaaji wako, je huwa unavaa kwa mzunguko upi yaani unavaa leo tu na kuzifua mara tu unapozivua au unavaa kwa kuzirudia daily yaani hiyo pair unaweza irudia kuvaa hata mara tatu kwa wiki.
 
Back
Top Bottom