Msaada: Mke wangu ana tatizo la uzazi

Msaada: Mke wangu ana tatizo la uzazi

Kwa hii issue ya brother naomba nichangie kidogo, ni kwamba wote hawawezi kuwa na tatizo la uzazi maana mwanamke keshafanikiwa kushika ujauzito tena zaidi ya mara moja. Ila nini hupelekea hadi mimba kutoka.? Naomba nigusie sababu kama mbili hivi

1. Pelvic Inflammatory Disease (PID).
Haya ni maambukizi katika via/mirija ya uzazi. Baada ya yai la kike kupevushwa katika mirija (Fallopian tubes) hushindwa kusafiri hadi kwenda kwenye uterus hali inayopelekea mimba kutungwa nje ya mfuko wa uzazi. Na mimba huweza kukaa hadi kipindi cha week 13 (Miezi mitatu) au chini ya hapo kisha ikaharibika na ndiyo hiyo ambayo hutoka na mwanamke kupata bleed. Tatizo hili huweza kufanyiwa kipimo cha Ultrasound katika via vya uzazi na hata nyonga (Pelvic USS and Abdomen USS) ili kuangalia ukubwa wa tatizo na kisha kulitibu. Sababu nyingine ni

2. Rhesus Factors (Rh).
Hizi ni chembechembe za protein ambazo huwa zimo katika chembe chembe nyekundu za damu kutegemeana na aina ya damu mtu aliyonayo. Zinaeza kuwa za hasi ama chanya. Rhesus factor positive means unazo hizo protein or Rhesus factor negative means hauna hizo protein. Kama baba atakuwa ni Positive na mama akawa ni Negative basi kuna uwezekano mkubwa kila atakapokuwa anashika ujauzito mimba ikawa inatoka/kuharibika ama mtoto akafariki kipindi cha kujifungua.

Hii hutokea pale ambapo mimba iliyotungwa inarithi damu ya mama ambayo haina chembechembe za protein, na mama tunamuhesabu kama Rhesus factor negative. Then inaungana na damu ya baba ambayo inachembe chembe za protein kwenye damu (rhesus factor positive), hali hii hupelekea kinga mwili kuanza kushambulia zile chembechembe za damu ambayo ni positive ambazo zishachanganyikana na red blood cells za mtoto na hivo kupelekea mimba kuharibika na kutoka.

Tunashauri pia kabla ya wazazi kutafuta mtoto ni vema kufanya kipimo kuhusiana na Rhesus factor, na endapo itaonekana mama ni Rhesus factor Negative na baba ni Positive basi itabidi mama achomwe sindano tunaita Anti D Immunoglobulin ili iende kuzuia ule mchanganyiko wa zile damu. Kumbuka negative na positive zikiungana lazima upate shoti. Nimeona nishare nanyi ndugu zangu ili tuweze kuelekezana na kujifunza zaidi na zaidi.

Emmaloy...[emoji3578]
 
IMG_3029.jpg

Hapa nimewaambatanishia picha ya kuonesha huo muunganiko wa hizo Rhesus factors. Hizo zenye Compatibility hazina tatizo ila yenye Incompatibility ndio ina shida na mara nyingi hupelekea hiyo changamoto ya mimba kuharibika ama mtoto kufariki punde tu baada ya kujifungua. Nawasilisha.

Emmaloy..[emoji3578]

+255656629352
 
Nimeishi na mke wangu kwa mwaka mmoja na nusu.

Alipata ujauzito mara ya kwanza katika maisha yake, ule ujauzito ulidumu kwa miezi 3 kisha ukatoka.

Akapata ujauzito kwa mara ya pili huu ulikaa kwa muda wa miezi 2 ukatoka.

Akapata ujauzito kwa mara ya tatu huu ulikaa kwa muda mwezi mmoja tu ukatoka yani tulivyopima ujauzito haikupita siku 3 ukatoka.

Tukienda hospitali zenye specialist wa masuala ya uzazi wanampima na wanasema hana tatizo lolote.

Sasa imekuwa ngumu kupata ujauzito na sijui tatizo ni nini? Yaani kila mwezi anaonesha dalili za ujauzito ila ukipima hamna kisha anaingia kwenye siku zake.
Kama bado una tatizo, wasiliana na mimi kwenye PM nikupe contact ya mtu atakayekutatulia tatizo hilo kabisa
 
Back
Top Bottom