Msaada: Mke wangu anataka tuwe tunaishi na mtoto wa dada yake kila wikiendi na likizo

Habari wakuu mke wangu ana dada yake ambaye kazalishwa mtoto mmoja na Dada yake hayuko katika ndoa, hajaolewa na aliyemzalisha alikuja akaoa mwanamke mwingine

Sasa basi mimi na mke wangu tuna mtoto mdogo wa umri sawa na mtoto wa Dada yake.. mke wangu amekuwa akimchukua mtoto wa Dada yake kila Ijumaa na kumrudisha Jumapili kwa Dada yake

Sasa akiwa anataka kumrudisha mtoto hataki kurudi kwa mama yake anataka kuendelea kuishi nasi wakati huo baba wa mtoto hana muda na mtoto wake kwa mahitaji ya mtoto yaani hamuhudumii.

Mama wa mtoto hataki hata siku moja kumpelekea mtoto kwa baba yake sababu ana mke mwingine atamtesa, Sasa amekuwa akimsukumia kwangu kwa kigezo cha kuja kucheza na mwenzake

Je, ni sawa baba wa mtoto yupo na mama wa mtoto kukataa mtoto kwenda kwa baba kutembea kwa kisingizio Cha mama wa kambo atamtesa hivyo kuona ni sahihi aende kwa mama yake mdogo hali ya kuwa baba yupo na anajichana na maisha?
Mkuu hupendi kuona mwanao anafurahia kampani ya mtoto mwenzake?
 
Hivi tabu hapo ni huo ugali marage anaokula kwako au kitu gani? Au kulalia kitanda na kukalia kochi ambalo hata mwanao anakalia [emoji23]
Kwani mkuu hayo maharage nayapata bure? Huyo mtoto ni yatima.
 
Wewe ni maskini wa roho mzee [emoji23] very bad character! Watu wana complain kuhusu ada, gharama za afya ila sio mavi!
Na umaskini nilionao umetokana na ujinga wa kulea ujinga kama huu, vinginevyo ningekua milionea...
Ndio maana tajiri hata awe na ela nyingi kiasi gani hafanyi ujinga kama huu, na ndio maana wao huzaa watoto wachache, kwangu ada na afya sio gharama ila chakula ni gharama maana kula ni muhimu na lazima kila siku.
 
Bro sitaki unijibu ila nakuuliza hivi, huyo mtot ana umr gan? Kama ana miaka 13+ bc una uhalali wa kuhoji ila kama ni below hapo. JITAFAKARI WEWE NI MTU WA NAMNA GANI, huenda upo tofauti na binadamu wema, huenda ww n kauzu, huenda kusaidia wengne huwezi. Psychology niliyonayo nimegundua vitu vingi sana kwako hata kama ndy huyo mtot ana 15+yrs. TAMBUA BINADAMU HATUPO SAWA, ILA MKE WAKO ANAJUA NINI MANA YA KAULI YA "hakuna aijuaye kesho" mpende sana huyo mkeo.

Sign off
Akijibu hili mni tag jamani..... Tunahitaji kujua utofauti wa umri walio nao hao watoto usije kuta ni mtoto wa mkewe
 
Na umaskini nilionao umetokana na ujinga wa kulea ujinga kama huu, vinginevyo ningekua milionea...
Ndio maana tajiri hata awe na ela nyingi kiasi gani hafanyi ujinga kama huu, na ndio maana wao huzaa watoto wachache, kwangu ada na afya sio gharama ila chakula ni gharama maana kula ni muhimu na lazima kila siku.
Kama ni muhimu haviwezi kuwa gharama. Gharama ni kwa vitu ambavyo havina umuhimu.
 
Ni kawaida kwa maskini wa roho na akili kuja na kauli kama hizi
Si ajabu ukute wewe ni tajiri sana lkn una watoto wa2 au wa3 tu, kigezo ili uweze kuwalisha na kuwasomesha vizuri, nyie ndio mnaotucheka tunaozaa watoto wengi wanaotupa shida kulea lkn likija suala kama hili unatetea na kusema ni roho mbaya[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Hivi ile kauli mnayosemaga ya "kulea mimba sio kazi, kazi ni kulea mtoto" sio ya kweli eeh!!
Kabisa mkuu. Huyo mtoto angekua mkubwa hata mimi sikai nae.... ila mdogooo huyo. Na mimi nilichokiona kwa huyu mke wa jamaa na huyo mtoto wa mdogo wake ni kama kuna mazingira yaliyokua mazuri au salama mtoto kushinda siku nzima ndio maana ni holidays na weekends ndio anamchukua

Ila hii ya jamaa imekaa kichoyo sana. Imagine ameshindwa hata kulimaliza na mke hadi amelileta huku.
 
Mtoto wa miaka 6 mdogo?
Jamaa naona yupo sahihi maana huyo mtoto sio yatima ana wazazi wake wote, pia kama kucheza si wapo wa majirani kwanini mkewe aingie gharama ilhali wa majirani ni bure?
Ili alitakiwa tu anwambie mkewe ukweli kua hamtaki huyo mtoto hapo nyumbani sio kuzunguka tuuu
 
Si ajabu ukute wewe ni tajiri sana lkn una watoto wa2 au wa3 tu, kigezo ili uweze kuwalisha na kuwasomesha vizuri, nyie ndio mnaotucheka tunaozaa watoto wengi wanaotupa shida kulea lkn likija suala kama hili unatetea na kusema ni roho mbaya[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
Mkuu mie sio tajiri ila wa nafsi tu mkuu, nina huruma sana na very humble when it comes to such situations. Watoto ni malaika bana angekuwa mtu mzima ungeweza hata kumtimua akajitaftie ila mtoto sio kiumbe cha kuki treat vibaya.

Chuki utakayomjengea itakuja kuwa na athari kubwa sana kwenye vizazi vya mbeleni.
 
Habari wakuu mke wangu ana dada yake ambaye kazalishwa mtoto mmoja na Dada yake hayuko katika ndoa, hajaolewa na aliyemzalisha alikuja akaoa mwanamke mwingine

Sasa basi mimi na mke wangu tuna mtoto mdogo wa umri sawa na mtoto wa Dada yake.. mke wangu amekuwa akimchukua mtoto wa Dada yake kila Ijumaa na kumrudisha Jumapili kwa Dada yake

Sasa akiwa anataka kumrudisha mtoto hataki kurudi kwa mama yake anataka kuendelea kuishi nasi wakati huo baba wa mtoto hana muda na mtoto wake kwa mahitaji ya mtoto yaani hamuhudumii.

Mama wa mtoto hataki hata siku moja kumpelekea mtoto kwa baba yake sababu ana mke mwingine atamtesa, Sasa amekuwa akimsukumia kwangu kwa kigezo cha kuja kucheza na mwenzake

Je, ni sawa baba wa mtoto yupo na mama wa mtoto kukataa mtoto kwenda kwa baba kutembea kwa kisingizio Cha mama wa kambo atamtesa hivyo kuona ni sahihi aende kwa mama yake mdogo hali ya kuwa baba yupo na anajichana na maisha?
Wewe ni mume tu umekuja ukawakuta kwenye udada wao msikilize na mkeo anasema nini kwenye hili
 
Mkuu mie sio tajiri ila wa nafsi tu mkuu, nina huruma sana na very humble when it comes to such situations. Watoto ni malaika bana angekuwa mtu mzima ungeweza hata kumtimua akajitaftie ila mtoto sio kiumbe cha kuki treat vibaya.

Chuki utakayomjengea itakuja kuwa na athari kubwa sana kwenye vizazi vya mbeleni.
Hizo ni imani kama zilivyo imani zingine mkuu, nimelea ndugu na watoto kwa zaidi yq miaka 10 sijaona baraka yoyote, kwani mtoto ni yatima?
Tangu nimeacha huu ujinga hata kibubu changu mwaka huu kimekua, ukweli utabaki palepale huruma zetu zinatuponza sana,

Hata Mungu atakua anakushangaa, kakubariki uwe tajiri lakini kila upatacho unaendekeza misaada tu
 
Mtoto wa miaka 6 mdogo?
Jamaa naona yupo sahihi maana huyo mtoto sio yatima ana wazazi wake wote, pia kama kucheza si wapo wa majirani kwanini mkewe aingie gharama ilhali wa majirani ni bure?
Ili alitakiwa tu anwambie mkewe ukweli kua hamtaki huyo mtoto hapo nyumbani sio kuzunguka tuuu

Hao wanaomuona mleta mada ana roho mbaya waulize wanalea watoto wangapi ambao siyo wakwao?
Au lini wamepeleka hata kilo ya unga kwenye vituo vya kulelea watoto yatima na kuwapa japo maji ya kunywa watoto wa mtaani waliozagaa nchi nzima!!?
 
Sawa chief!

Back
Top Bottom