Msaada: Mke wangu anataka tuwe tunaishi na mtoto wa dada yake kila wikiendi na likizo

Kama hamtaki huyo mtoto na ana sababu za msingi mbona anashindwa kumwambia mkewe?. Yeye ndio baba wa familia yake na sioni kwa nini ushauri wa kitu chepesi kama hiki utoke kwa great thinkers 😁😁
 
Nakubaliana na wewe sana tu,watu wengi wanaliangalia hili suala na 'emotion'zao.Wanaona katoto kanakuja kucheza basi,wanapiga stop hapo.Lakini kuna majukumu ambayo hawayaangalii,hiyo weekend itageuka kuwa 'kila siku' na mtoto na wataanza kusema'mtoto kazoea kuja hapo' mzigo utatuwa kwa jamaa.Kama wazazi wangekuwa hawapo au hawana uwezo basi ni sawa kumchukua mtoto na kukaa nae tena ki roho safi kabisa.Lakini wapo !,aisee no way.Alafu mi huwa
Siwaelewi wazazi wanaozaa alafu kumpa mwengine ulezi,uzuri wa kuzaa mtoto uwe naye karibu,ucheze nae,ujue uzima na ugonjwa wake na mtoto ajue kama ana mzazi anaemjari.Kama haupo tayari kulea, subiri usizae.
 
Maisha yetu hayo mkuu. Tena wewe unakua umejitoa umejinyima hadi umewadhulumu watoto wako kwaajili ya hao ndugu kwa miaka yote hiyo na sasa wanakucheka😁😁 Mimi siku hizi nasema kama ni msaada uwe kwa jambo la msingi, na huo msaada umfikie mhusika hukohuko waliko😎

Ila sioni gharama kwa huyu mtoto maana anachofuata hapo ni usalama tuu. Huyu bwanamkubwa cha kufanya akae na mkewe amweleze ni kwanini wakae nae na wakubaliane kama ni kwa muda gani. Na amwambie mkewe kwa kuendelea maamuzi kama hayo lazima wayaamue pamoja kabla ya utekelezaji
 
Kama hamtaki huyo mtoto na ana sababu za msingi mbona anashindwa kumwambia mkewe?. Yeye ndio baba wa familia yake na sioni kwa nini ushauri wa kitu chepesi kama hiki utoke kwa great thinkers [emoji16][emoji16]
Alitaka kujua magreat thinker wanachukuliaje hilo mwishowe wakamchamba akajikuta kaikana hoja yake akabaki kusema wanaharibiana tabia[emoji23][emoji23]
Hajui kua akili za kuambiwa changanya na zako.
 
Wengi wanaotetea ni masingo mama mkuu, na waliozalisha afu hawalei
 
Gharama lazima ipo mkuu, ukiona jamaa anavolalamika jua kuna jambo kaliona,
Kushinda kwake siku tatu lazima ale afuliwe na mengineyo pia mkewe pengine kwa kujifanya mwema na nguo na viatu anamnunulia pia,
Usisahau mtoto wa miaka 6 anaweza kula mlo mkubwa kuliko wa mtu mzima.
 
Mtoto anakuja weekends siku za wiki yuko kwao ubaya uko wapi? Pengine mazingira aliyopo mama yake sio rafiki kwa michezo labda kuna wahuni wengi au uswahilini mno. Wewe jibaba una complain
Ahame hayo mazingira atafute mazingira rafiki, asingekuwepo huyo jamaa angefanya nini? Mnatetea ujinga, umeshawahi kupeleja hata kilo 2 za mchele kwa watoto yatima kwa huruma mnayikuwa nayo au mnasema tu. Haya mnayaongea hapa ikitikea katika mausha halisi ya kwenu kuletewa watoto mnawakataa. Acheni unafiki
 
Kuna watoto wengi wasio na makazi mitaani, ulishachukua wangapi mpaka sasa?
 
Alitaka kujua magreat thinker wanachukuliaje hilo mwishowe wakamchamba akajikuta kaikana hoja yake akabaki kusema wanaharibiana tabia[emoji23][emoji23]
Hajui kua akili za kuambiwa changanya na zako.
Ma great thinkers wakiona hoja nyepesi inakuvuruga wanaona kama unawavuruga tuuu na matokeo yake wao wanakuvuruga zaidi. 😂😂😂😂😂
 
Ma great thinkers wakiona hoja nyepesi inakuvuruga wanaona kama unawavuruga tuuu na matokeo yake wao wanakuvuruga zaidi. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kwa kweli wamejua kumvuruga adi kasahau kwao
 
Vipi ww ukifa mkeo akaolewa kisha libaba lingine nalo limtimue mwanao?
 
Umeenda mbali sana, muulize ameenda mara ngapi vituo vya watoto yatima na kuwa msaada
Hio hoja nyepesi sana, ni sawa na mtoto amuulize baba kwanini unalala na mama?

Kule kuna utaratibu rasmi uliowekwa na wale watoto wanakuwa managed na Taasisi.
 
Kama hamtaki huyo mtoto na ana sababu za msingi mbona anashindwa kumwambia mkewe?. Yeye ndio baba wa familia yake na sioni kwa nini ushauri wa kitu chepesi kama hiki utoke kwa great thinkers 😁😁
Anashindwa kumuingia mkewe maana anajua hana hoja ya msingi na ataonekana mpumbavu tu mbele ya mkewe. Ndio maana kaja kwenye fikra pevu huku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…