Bado sijaona kinachomfanya mleta Uzi aonekane ana roho mbaya! Kinachoonekana watu wametanguliza hisia zao.
Mleta uzi ametupatia usuli(history) ya mtoto kuwa kila wiki anakuja na ukiliangalia hilo kwake halionekani ni tatizo kila wiki kuja.
Hata mtoto kugoma kwake si tatizo! Bali tatizo wazazi waliyomzaa mtoto wapo na wanashughuli zao na bado wanawajibika kumlea mtoto wao ila kinachoonekana majukumu hayo anataka kupatiwa yeye. Kwa sababu uono wa mleta Uzi ni kuwa hata kama wametofautiana ila bado huyo mtoto ni mtoto wao na ni wajibu wao kumlea.
Ukiangalia mtoto anagoma kuondoka itafika mahala ndo ataishi hapo mazima! Ni kama tabibu, haaangalii matokeo ya ugonjwa bali anaangalia chanzo ili atibu ugonjwa mazima. Halikadhalika kwa mleta Uzi, Sasa kugoma kuondoka kwa mtoto ina maana gharama za uendeshaji wa familia zitazidi ila ukiangalia kwa aliyeleta Uzi hayo yote kwake si tatizo bali tatizo ni kuwa hizo gharama kwake si stahiki na ndipo mazingira yatakavyokuwa huko mbeleni.
Na jamaa yupo sahihi kuwa kugharamikia si tatizo ila ni kwa nini abebeshwe mzigo hali ya kuwa mbebaji wa huo mzigo yupo na uwezo wa kuubeba wanao?
Na ukiangalia kwa undani zaidi utakuta baba wa mtoto anao uwezo wa kumgharamikia isipokuwa wanawake wana roho mbaya sana tena sana! Inawezekana anamkomoa mshikaji kwa kutomhusisha kabisa na mtoto na kwake anafanya ni kama kisasi kwa jamaa.
Hatukatai ndugu, hatukatai kusaidia! Tunachikitaka ni lazima jamii ifahamu wajibu wake na iwajibike. Tusiweke ngao ya undugu au ukaribu kwa mtu kukimbia majukumu yake. Ikiwa kama jamaa kamkataa mtoto na dada wa mkeo hana uwezo hapo sawa mtaangalia njia gani ya kuweza kumsaidia. Kama uwezo anao mta share gharama.