Msaada: Mke wangu anataka tuwe tunaishi na mtoto wa dada yake kila wikiendi na likizo

Eeh anaona watoto ni kero mpumbavu kweli kweli. Watoto ni baraka sana kwani ni kama malaika wa ulinzi watakuwa wanaizingirs nyumba yako muda mwingi.
Swaka sio anaona mtoto kero, acheni kuhamisha mada, swala ni kuendelea kulea mtoto ingali baba yake yupo eti kisa atamtesa. Why alikubali kuacha lango wazi? Acheni unafiki kwa kufikiri kuwa jamaa anaongelea chakula, jiketeni kwenye hoja
 
Hili nalo ni Jambo la kuja kushtaki huku jf.
Unajua mtu mzima anasifa ya kukomaa mwili na akili. Wewe hili la MWISHO bado!
 
Hahahaha mwamba alivyoandamwa kuwa anaroho mbaya.bilashaka atabadilika
 
acha uchoyo wewe
 
Kwanza wanampa uhuru wa huyo mdada kuendelea kula raha...apewe mwanae akae naye kila siku aujue uchungu wa kulea.
 
Acha Acha roho mbaya kwani anakula nini kikubwa hivyo mpaka upanic? Mhhh wanaume hawana tabia hizo
 
Bado sijaona kinachomfanya mleta Uzi aonekane ana roho mbaya! Kinachoonekana watu wametanguliza hisia zao.

Mleta uzi ametupatia usuli(history) ya mtoto kuwa kila wiki anakuja na ukiliangalia hilo kwake halionekani ni tatizo kila wiki kuja.

Hata mtoto kugoma kwake si tatizo! Bali tatizo wazazi waliyomzaa mtoto wapo na wanashughuli zao na bado wanawajibika kumlea mtoto wao ila kinachoonekana majukumu hayo anataka kupatiwa yeye. Kwa sababu uono wa mleta Uzi ni kuwa hata kama wametofautiana ila bado huyo mtoto ni mtoto wao na ni wajibu wao kumlea.

Ukiangalia mtoto anagoma kuondoka itafika mahala ndo ataishi hapo mazima! Ni kama tabibu, haaangalii matokeo ya ugonjwa bali anaangalia chanzo ili atibu ugonjwa mazima. Halikadhalika kwa mleta Uzi, Sasa kugoma kuondoka kwa mtoto ina maana gharama za uendeshaji wa familia zitazidi ila ukiangalia kwa aliyeleta Uzi hayo yote kwake si tatizo bali tatizo ni kuwa hizo gharama kwake si stahiki na ndipo mazingira yatakavyokuwa huko mbeleni.

Na jamaa yupo sahihi kuwa kugharamikia si tatizo ila ni kwa nini abebeshwe mzigo hali ya kuwa mbebaji wa huo mzigo yupo na uwezo wa kuubeba wanao?

Na ukiangalia kwa undani zaidi utakuta baba wa mtoto anao uwezo wa kumgharamikia isipokuwa wanawake wana roho mbaya sana tena sana! Inawezekana anamkomoa mshikaji kwa kutomhusisha kabisa na mtoto na kwake anafanya ni kama kisasi kwa jamaa.

Hatukatai ndugu, hatukatai kusaidia! Tunachikitaka ni lazima jamii ifahamu wajibu wake na iwajibike. Tusiweke ngao ya undugu au ukaribu kwa mtu kukimbia majukumu yake. Ikiwa kama jamaa kamkataa mtoto na dada wa mkeo hana uwezo hapo sawa mtaangalia njia gani ya kuweza kumsaidia. Kama uwezo anao mta share gharama.
 
Huyo mtoto anakujaga room mkiwa mna jigijigi na wife?
 
Mkuu tatizo sio kuishi tatizo ni kuwa mtoto kashaanza kuadapt tabia za kike na mama tu haoni shida kwake
Samahani mkuu kama hutajali naomba kuuliza, umri wa hao watoto na ni tabia gani hizo za kike mwanao anaiga?.
 
Umeongea vizuru sana,ila bado kuna mijitu itatokea itarudi na kusema,jamaa ana roho mbaya.
 
Umeongea vizuru sana,ila bado kuna mijitu itatokea itarudi na kusema,jamaa ana roho mbaya.
Wengi wanaongea tu hapa ila kwa ground utasikia wanasema “naleaje mtoto wa mwanaume mwenzangu na yeye yupo”, ila hapa wanaona jamaa ana roho mbaya. Wabongo ninwanafiki kinoma mzee wangu, tena wanafiki sana. Huyo mtoto hana kosa ila baba yke yupo ahudumie. Kama mama yake hataki kumpeleka amlee mwenyewe na asiwape watu shida
 
Anaefaidika hapa ni mwanao zaidi, watoto waliopekeyao wanakuwa wapweke sana na wanafurahi sana wanapopata watoto wenzio wa kucheza nao.

Mkeo anaakili sana na utu wala hata hutakiwi kuhoji vitu kama hivyo zaidi unapaswa kumjali kama mwanao.

Maisha haya tunapita ukiweza kusaidia mtu mzima acha mtoto fanya tu inakusaidia na kukuongezea riziki maana mtoaji anaona una majukumi mengi zaidi.

Wengine wanahangaika mpaka kuadopt wewe unae tena ndugu bado unajiuliza.
 
Hao watoto wako walafii sana duu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mkatee mzimaaa mtoto wa miaka 4????
 
Mambo mengine siyo ya kuja kutuuliza huku, wewe ni mwanaume kweli au Marioo? yaani hupendi kitu kifanyike kwenye nyumba yako unakuja kutuuliza huku tena kwa ujasili kabisa eti naomba ushauri.
Humtaki huyo mtoto mwambie mke wako wazi kuwa hutaki, PERIOD au ndo wale mnaoa mnaishia kuachia IST nyumbani kwa ajili ya kupeleka watoto wa shule, kwenda kulipa ada za watoto, bili za maji na umeme, mwisho ukaangalie msimamizi wa shamba anaendeleaje. Kwani huyo mtoto akikaa kwako hizo siku tatu unapungukiwa nini? Kuna ubaya gani ikiwa mke wako ameamua kumsaidia mtoto wa ndgu yake, nawe tafuta mtoto wa ngd yako msaidie.
Kuhusu suala la mama mtoto kukataa mwanae kwenda kwa mama wa kambo huenda ana sababu za msingi,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…