Msaada: Mke wangu anataka tuwe tunaishi na mtoto wa dada yake kila wikiendi na likizo

Huwezi ruhusu mtoto ahamie moja kwa moja, akifika umri ambao anaweza kujitegemea like 10 yrs and above unaweza mwambia shemeji akae nae kwake sasa.

Kwa umri huo alionao sasa hata kujipikia hawezi ndio maana kaspgezwa kwako.
Mkuu hawezi mindonaejua we unaweza muacha mwanao wamiaka10 peke take Kisha ukasafiri
 
Kwanza unatakiwa kulipa huuyho mtoto kwa kuja mkucheza na mwanao acha mkufujatioia mambo madogo hao ni ndugu, wa damu nakushauri mchukkuje kbs itasaidia shrm kuolewa........ jama vipi tupe budget ya hizo siku mbili tupange donation......
Mkuu nashukuru mungu najiweza vizur tu Wala siitaji donation
 
Dang son.

Kama uko sawa uko perceptive sana.

Kama umekosea una confidence mbaya sana.
Mkuu sio hivo mtoto niwadada yake..naanzia wapi kuoa mwanamke mwenye mtoto wakat misijawahi kuoa Wala kuzalisha mtu hapo kabla
 
Dogo unawaza ngono tu muda wote.
 
Nyie ni wale wanaume mnsohesabu nyama jikoni
Tena ingefaa kama nafasi ipo mumchuwe aishi na nyie, sabu anaonekana kuwa happy hapo kwenu
 
Unamuelewaje mvulana anaelalamikia gharama za chakula cha mtoto ikiwa yeye pia ana mtoto.
Kuna kitu wewe hujakiona kwa Uzi wa huyu jamaa!

Halalamikii gharama za chakula za huyo mtoto. Ukisoma Uzi wake vizuri utagundua haya yafuatayo:

-Mama wa mtoto anaona mtoto anambana anashindwa kufanya shughuli zake vizuri.

-Baba wa mtoto hajamkataa mtoto na aliruhusu akae kwake kabisa. Baba wa mtoto ana kipato cha kumlea mtoto.

-Mama wa mtoto anadai mwanae anateswa na mama wa kambo hivyo hawezi kuruhusu mwanae akae kwa baba yake.

Kilichofuata ni kipi:
-Mama wa mtoto ameamua kumpeleka mtoto kwenye familia ya mdogo wake kila mwisho wa juma.

Hatua iliyopo sasa:
-Mtoto ameanza kuonyesha ishara ya kugoma kuondoka kwenye familia ya mdogo wa dada.

Muhimu ya kuzingatia:
-Mama wa mtoto anamlea peke yake, anaona mtoto anambana kutokana na malezi hivyo inamuwia ngumu kwake kutekeleza shughuli zake kikamilfu.

-Na watoto wanapendeza wanatia huruma kwenye moyo. Na hii Dada mtu kwake imekuwa ni fursa.

-Kuna harufu ya wazi kabisa mbeleni mdogo mtu atatupiwa mzigo wa malezi wote! Kila kitu kina sababu na ndiyo dada yake anaiandaa kuwateka mdogo na mume wa mdogo wake.

Hii ni nukta muhimu ambayo anaweza akaitumia kama karata kwenye familia ya mdogo wake ili mwanae akae ili yeye aweze kufanya shughuli zake.

Malezi yanafahamika kuna mambo ni lazima yatazamiwe:

Ikiwa mtoto atakaa kwa mdogo wake ndipo hapo mume wa mdogo wake (ambaye ni mleta Uzi) anajiuliza; Yule ni dada wa mkewe ni ndugu huruma ipo baina yao. Yeye anaweka kuona ni sawa mtoto wa Dada yake kukaa kwake lakini kuna haya ya:

1)Kimalezi
2) Gharama

Suala la kwanza anaweza akalivumilia lakini vipi suala la pili? Kumbuka hapo mtoto hajakataliwa na baba yake na baba yake kipato anacho hayo ni maamuzi binafsi tu ya huyo dada. Sasa kuna harufu nzima ya mtoto kubaki kwake na mazingira yanaonyesha wazi lakini Je, suala la gharama za malezi ya mtoto yatakuwaje?

Yatakuja kwa wakati ikiwa mtoto atabaki kwake? Yeye hawezi kuongea moja kwa moja na dada wa mkewe bali ni suala la mkewe kuongea na dada yake. Je, mkewe ataweza kuongea nyeupe moja kwa moja? Na baba mtoto hajakataa kulea damu yake.

Na kwa nini mtoto aletwe kwake?Ukisoma maelezo yake kwa kutulia utaona kuna jambo lengine la msingi. Mtoto anahitaji mapenzi ya baba na mama. Kwa nini hizi siku za mapumziko asizitumie vilevile kumpeleka mtoto kwa baba yake kama anavyofanya kumpeleka kwa mdogo wake? Kwa sababu baba hajamkataa! Kwa hiyo, hapa anapigania haki ya mtoto ambayo ninyi hamuioni.

Itakuwa ni upuuzi hayo majukumu yakavikwa familia yake. Binafsi, mimi ningeli kataa kama yeye anavyolikataa. Siwezi kubeba majukumu ambayo hayana msingi. Kuna upole na kuna upole wa kijinga. Msaada unaenda kwa mtu stahiki! Ninyi mnatanguliza hisiya badala ya mustakabali wa mambo jinsi ulivyo, mnamhukumu jamaa ni mchoyo!

Huyo dada asibebeshe watu mzigo! Atafute mfanyakazi atakaye muangalia mwanae kipindi akienda kwenye mihangaiko yake. Au atafute ndugu atakayekuwepo muda wote nyumbani ili amwangalie mwanae.

Vilevile mtoto apelekwe kwa baba yake hizo siku za mapumziko na ukiangalia jamaa hakumkataa mtoto. Aache wivu! Sijui mtoto anateswa aache wivu. Ikiwa ni kweli anateswa azungumze na mzazi mwenzake jinsi gani ya kumlea mtoto wao.
 
Mkuu Wala Sina tatizo namtoto wote nawatreat vizur tu tatizo lipo kwa mama yake kumkatalia mtoto kwenda hata kwababa yake kwakisingizio Cha kutomhudumia na mama wakambo
kukataliwa mtoto kwenda kwa baba yake linakuaje tatizo kwako?
 
Huna point mzee. Kama hutaki aje mwambie mkeo asimlete
 
Nyie ni wale wanaume mnsohesabu nyama jikoni
Tena ingefaa kama nafasi ipo mumchuwe aishi na nyie, sabu anaonekana kuwa happy hapo kwenu
Wamchukue kwa misingi ipi?

Kwani mtoto ni yatima? Au dada mtu hana kipato cha kumlea mwanae? Kwani mtoto amekataliwa na baba yake?

Baba hajakataa mtoto kipato anacho Licha ya kuwa amekwisha oa na amemkaribisha nyumbani kwake.

Mama wa mtoto ana shuguli zake za kumuingizia kipato.

Sasa amchukue kwa minajili ipi? Ili dada mtu aendelee kuzurura na mikakati yake?

Si bora nikae na mtoto yatima! Kuna watoto wamekosa fursa alizonazo huyo mtoto si bora nikae nao hao! Yaani nijibebeshe upuuzi? Si bora nijibebeshe begi tu hata likiwa halina kitu.
 
Ume summerise vizuri sana mkuu,Bravo!.Ingependeza zaidi watu wangesoma ulichoandika kabla hawaja comment,hasa wale wanaosema'jamaa mchoyo', 'ana roho mbaya' 'mlee tu mtoto'.
Kwa mimi naona ulivoandika;
"Msaada unaenda kwa mtu stahiki! Ninyi mnatanguliza hisiya badala ya mustakabali wa mambo jinsi ulivyo, mnamhukumu jamaa ni mchoyo!" Umebeba ujumbe mkubwa wa hii mada.

Sent from my SM-G960F using JamiiForums mobile app
 
Mwanaume kuandika huu upuuzi ni ishara moja ya upungufu wa akili na gubu na uchoyo
 
Kama ameyaona hayo anashindwa nini kumtafuta mwanaume mwenzie akae nae chini aongee nae
 
Ataongea nae nini mkuu?ukizingatia baba mtu hana tatizo la kulea mtoto bali dada mtu ndio hataki mwanae akaishi kwa baba
Kama ameyaona hayo anashindwa nini kumtafuta mwanaume mwenzie akae nae chini aongee nae
 
Ataongea nae nini mkuu?ukizingatia baba mtu hana tatizo la kulea mtoto bali dada mtu ndio hataki mwanae akaishi kwa baba
Ni hivi kuongea naee kama mwanaume na kupanga mikakati baina yao wao wawili na mtoto simzungumzii mama wa mtoto hapo ni baba na mwanae
 
Ubarikiwe bibi angu kipenzi, una busara sana.
 
Hizo comments sasa, mtoa mada kapata funzo murua.
 
Ni hivi kuongea naee kama mwanaume na kupanga mikakati baina yao wao wawili na mtoto simzungumzii mama wa mtoto hapo ni baba na mwanae
Yeye si wa kuongea na baba mtoto,kwa tabia za wanawake huyo mama mtoto atamgeukia.Kinachotakiwa hapa amwambie mkewe aongee na dada ake(mwenye mtoto) kuwa wayasawazishe na baba mtoto,ili huyo baba abebe majukumu ya ulezi wa mwanawe,sio yeye ajipeleke moja kwa moja kwa jamaa,labda kama atatakiwa kwenye mazungumzo lakini sio sehemu yake kuanzisha mjadala wa huyo mtoto.Ingawa nakubaliana nae kuwa wazazi ni jukumu lao kulea mtoto walomzaa, hasa kama uwezo wanao.Nnavyojua tabia za wanawake si ajabu baba hana tatizo kabisa kumwangalia mtoto wake,ila sababu ana mwanamke mwengine huyo mama mtoto ndo kisa kuchukia na kutaka kumkata jamaa kabisa kwenye makuzi ya mtoto,kama kaamua hivyo jamaa asilaumiwe kukataa jukumu lisolomhusu.wanawake wenzake kama wanaamua kumkatia mzazi mwenzao kwenye makuzi ya mtoto,wao wenyewe wanasimama kidete kumlea mtoto,sio kujifanya u bize alafu mtoto kumsukumia mwengine!.
 
Mkuu sio hivo mtoto niwadada yake..naanzia wapi kuoa mwanamke mwenye mtoto wakat misijawahi kuoa Wala kuzalisha mtu hapo kabla
Mwanamke kama ana mtoto utamjuaje na unawezaje kumtofautisha na mwanamke asiye na mtoto?

Mfano unakutana na mwanamke ana mtoto, anakudanganya hana mtoto.

Utajuaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…