Unamuelewaje mvulana anaelalamikia gharama za chakula cha mtoto ikiwa yeye pia ana mtoto.
Kuna kitu wewe hujakiona kwa Uzi wa huyu jamaa!
Halalamikii gharama za chakula za huyo mtoto. Ukisoma Uzi wake vizuri utagundua haya yafuatayo:
-Mama wa mtoto anaona mtoto anambana anashindwa kufanya shughuli zake vizuri.
-Baba wa mtoto hajamkataa mtoto na aliruhusu akae kwake kabisa. Baba wa mtoto ana kipato cha kumlea mtoto.
-Mama wa mtoto anadai mwanae anateswa na mama wa kambo hivyo hawezi kuruhusu mwanae akae kwa baba yake.
Kilichofuata ni kipi:
-Mama wa mtoto ameamua kumpeleka mtoto kwenye familia ya mdogo wake kila mwisho wa juma.
Hatua iliyopo sasa:
-Mtoto ameanza kuonyesha ishara ya kugoma kuondoka kwenye familia ya mdogo wa dada.
Muhimu ya kuzingatia:
-Mama wa mtoto anamlea peke yake, anaona mtoto anambana kutokana na malezi hivyo inamuwia ngumu kwake kutekeleza shughuli zake kikamilfu.
-Na watoto wanapendeza wanatia huruma kwenye moyo. Na hii Dada mtu kwake imekuwa ni fursa.
-Kuna harufu ya wazi kabisa mbeleni mdogo mtu atatupiwa mzigo wa malezi wote! Kila kitu kina sababu na ndiyo dada yake anaiandaa kuwateka mdogo na mume wa mdogo wake.
Hii ni nukta muhimu ambayo anaweza akaitumia kama karata kwenye familia ya mdogo wake ili mwanae akae ili yeye aweze kufanya shughuli zake.
Malezi yanafahamika kuna mambo ni lazima yatazamiwe:
Ikiwa mtoto atakaa kwa mdogo wake ndipo hapo mume wa mdogo wake (ambaye ni mleta Uzi) anajiuliza; Yule ni dada wa mkewe ni ndugu huruma ipo baina yao. Yeye anaweka kuona ni sawa mtoto wa Dada yake kukaa kwake lakini kuna haya ya:
1)Kimalezi
2) Gharama
Suala la kwanza anaweza akalivumilia lakini vipi suala la pili? Kumbuka hapo mtoto hajakataliwa na baba yake na baba yake kipato anacho hayo ni maamuzi binafsi tu ya huyo dada. Sasa kuna harufu nzima ya mtoto kubaki kwake na mazingira yanaonyesha wazi lakini Je, suala la gharama za malezi ya mtoto yatakuwaje?
Yatakuja kwa wakati ikiwa mtoto atabaki kwake? Yeye hawezi kuongea moja kwa moja na dada wa mkewe bali ni suala la mkewe kuongea na dada yake. Je, mkewe ataweza kuongea nyeupe moja kwa moja? Na baba mtoto hajakataa kulea damu yake.
Na kwa nini mtoto aletwe kwake?Ukisoma maelezo yake kwa kutulia utaona kuna jambo lengine la msingi. Mtoto anahitaji mapenzi ya baba na mama. Kwa nini hizi siku za mapumziko asizitumie vilevile kumpeleka mtoto kwa baba yake kama anavyofanya kumpeleka kwa mdogo wake? Kwa sababu baba hajamkataa! Kwa hiyo, hapa anapigania haki ya mtoto ambayo ninyi hamuioni.
Itakuwa ni upuuzi hayo majukumu yakavikwa familia yake. Binafsi, mimi ningeli kataa kama yeye anavyolikataa. Siwezi kubeba majukumu ambayo hayana msingi. Kuna upole na kuna upole wa kijinga. Msaada unaenda kwa mtu stahiki! Ninyi mnatanguliza hisiya badala ya mustakabali wa mambo jinsi ulivyo, mnamhukumu jamaa ni mchoyo!
Huyo dada asibebeshe watu mzigo! Atafute mfanyakazi atakaye muangalia mwanae kipindi akienda kwenye mihangaiko yake. Au atafute ndugu atakayekuwepo muda wote nyumbani ili amwangalie mwanae.
Vilevile mtoto apelekwe kwa baba yake hizo siku za mapumziko na ukiangalia jamaa hakumkataa mtoto. Aache wivu! Sijui mtoto anateswa aache wivu. Ikiwa ni kweli anateswa azungumze na mzazi mwenzake jinsi gani ya kumlea mtoto wao.