Msaada: Mke wangu anataka tuwe tunaishi na mtoto wa dada yake kila wikiendi na likizo

Msaada: Mke wangu anataka tuwe tunaishi na mtoto wa dada yake kila wikiendi na likizo

Mkuu huku mitandaoni kila mtu hujidai ni mwema na ana roho nzuri
Hamna sababu ya kujidai bana, mtoa mada ange declare kuwa hali yangu ni mbaya hata kula na mke ni shida hatujiwezi. Hapo inge justify utetezi wenu kwake.

Ila kama kila kitu kipo on de right tilaki huo ni uchoyo tu black and white! Tabia ya hovyo sana!
 
Sasa nimeanza kuelewa kumbe hampendi

Kipindi nipo mtoto nna baba na mama wote ila kila weekend tulikua tunaenda kwa dada ake kucheza na watoto wengine na alikua kawaida tu

Sasa kumbe nyuma ya pazia mlikua mnakuja kutuanzishia uzi umu

Dah mtoto wangu atacheza kwao na majirani

Mleta mada acha roho mbaya
 
Habari wakuu mke wangu ana dada yake ambaye kazalishwa mtoto mmoja na Dada yake hayuko katika ndoa, hajaolewa na aliyemzalisha alikuja akaoa mwanamke mwingine

Sasa basi mimi na mke wangu tuna mtoto mdogo wa umri sawa na mtoto wa Dada yake.. mke wangu amekuwa akimchukua mtoto wa Dada yake kila Ijumaa na kumrudisha Jumapili kwa Dada yake

Sasa akiwa anataka kumrudisha mtoto hataki kurudi kwa mama yake anataka kuendelea kuishi nasi wakati huo baba wa mtoto hana muda na mtoto wake kwa mahitaji ya mtoto yaani hamuhudumii.

Mama wa mtoto hataki hata siku moja kumpelekea mtoto kwa baba yake sababu ana mke mwingine atamtesa, Sasa amekuwa akimsukumia kwangu kwa kigezo cha kuja kucheza na mwenzake

Je, ni sawa baba wa mtoto yupo na mama wa mtoto kukataa mtoto kwenda kwa baba kutembea kwa kisingizio Cha mama wa kambo atamtesa hivyo kuona ni sahihi aende kwa mama yake mdogo hali ya kuwa baba yupo na anajichana na maisha?
Kama utaweza uwe unakuja kwangu na familia yako kila weekend na likizo mkuu.

Wengine tunapenda watu.
 
Nyie ndiyo wanafiki wenyewe, watoto yatima wamejaa lakini hata kuwapelekea sabuni hampeleki halafu mnahonga na kununua machangu au kula bata halafu mnaongea ongea tu.
Orphanage zina utaratibu wake.
 
Maisha yetu hayo mkuu. Tena wewe unakua umejitoa umejinyima hadi umewadhulumu watoto wako kwaajili ya hao ndugu kwa miaka yote hiyo na sasa wanakucheka😁😁 Mimi siku hizi nasema kama ni msaada uwe kwa jambo la msingi, na huo msaada umfikie mhusika hukohuko waliko😎

Ila sioni gharama kwa huyu mtoto maana anachofuata hapo ni usalama tuu. Huyu bwanamkubwa cha kufanya akae na mkewe amweleze ni kwanini wakae nae na wakubaliane kama ni kwa muda gani. Na amwambie mkewe kwa kuendelea maamuzi kama hayo lazima wayaamue pamoja kabla ya utekelezaji
Hoyu bwana mkubwa kinachomuuma roho ni viporo vyake vya wali marage kuliwa na mtoto wa mama mdogo.
 
Mkuu mtoto kashaadapt tabia za kike na mama mtu hana habari
Hawa jamaa wasikutishe....nyumba si yako! Matumizi ya familia si unatoa wewe?

Sasa nani anakuamlia jinsi unavyotaka kuishi na familia yako?

Huyo mwanamke alivyokuwa anazaa na mwanaume mwenye mke hakujua kama mtoto atateswa....

Watu wanaofanya makosa wasiyoweza kushughulika nayo tusiwabebe saana....

Huyo mdogo mtu na mme mtu mpeni mtoto ili wakumbuke uchungu wa starehee waliyokuwa wanaifanya....
 
Hama hapo nyumbani muachie mkeo nyumba Pamoja na hayo hakuna sababu maalum ya huyo mtoto kuja kwako, Kwa sababu wewe ulimuoa mkeo sasa anapoletwa mtu mwingine zaidi yake hapo ndio hekima inatakiwa itumike, Binaadam kwa asili ni wabinafsi pamoja na kupenda kote huko ila kila kitu unachofanya unaangalia nafasi yako kwanza katika hilo je unafaidika vipi na jambo hilo kamahilo? Mkuu mji ni wa kwako usipangiwe na wapitaji.
 
Gharama lazima ipo mkuu, ukiona jamaa anavolalamika jua kuna jambo kaliona,
Kushinda kwake siku tatu lazima ale afuliwe na mengineyo pia mkewe pengine kwa kujifanya mwema na nguo na viatu anamnunulia pia,
Usisahau mtoto wa miaka 6 anaweza kula mlo mkubwa kuliko wa mtu mzima.
Hahahahah mtoto wa miaka 6 yupi huyo anaekula mlo wa mtu mzima? Angekuwa 11+ hapo sawa ila 6 yrs ni mdogo sana bana we. Mtoto wa la kwanza ale mlo wa mtu mzima?
 
Hakika mkuu, watu ni Lango la baraka ila jamaa hajui.

Anachotaka nafasi nzuri ya kumshikashika maziwa vizuri mke wake.
Eeh anaona watoto ni kero mpumbavu kweli kweli. Watoto ni baraka sana kwani ni kama malaika wa ulinzi watakuwa wanaizingirs nyumba yako muda mwingi.
 
Hamna sababu ya kujidai bana, mtoa mada ange declare kuwa hali yangu ni mbaya hata kula na mke ni shida hatujiwezi. Hapo inge justify utetezi wenu kwake.

Ila kama kila kitu kipo on de right tilaki huo ni uchoyo tu black and white! Tabia ya hovyo sana!
Mkuu wewe unayasema haya lkn huyafanyi ndio maana umesema hujapata nafasi ya kulea, sio kwamba hujapata bali hujaweka mazingira ya kukaribisha hilo jambo ikiwa unalipenda,
 
Kila Mtu Na Ashinde Match Zake!!

Niko Upande Wa Mleta thread!

[emoji23][emoji23]
Nipo upande wenu mkuu....kila mmoja ashinde mechi zake...

Vitafunwa vya asubuhi tu sikuhizi bei ghali...hasa weekend watu wanakula hatari.

Tehteheth.... ila mimi huwa nashangaa saana. Kwani huyo mwanamke alivyokuwa anafurahia hakujua mwanaume kaolewa na mtoto atakuja kuteseka???
 
Mkuu wewe unayasema haya lkn huyafanyi ndio maana umesema hujapata nafasi ya kulea, sio kwamba hujapata bali hujaweka mazingira ya kukaribisha hilo jambo ikiwa unalipenda,
Wife ana dada yake nae ana mtoto ambaye baba yake ni Laisez faire kama wa huyu mtoa mada ila namsaidiaga mara moja moja mambo yakiwa tight na nilishakaaga nae kipindi kirefu tu so naelewa.
 
Back
Top Bottom