snowhite
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,065
- 24,559
Wanajamvi, ninaomba msaada wa dhati kabisa.
Mdogo wangu wa pekee alifariki mwaka jana. Tulizaliwa wawili tu, wazazi pia walishafariki. Baada ya wazazi kufariki, nilikuwa mama yake, alikuwa baba yangu.
Fact kuwa familia hii nimebaki peke yangu, kila nikiwaza inanistrike vibaya mno! Sijui kama nimekubali kuwa hayupo tena au la.
Naogopa kukubali kuwa nimebaki peke yangu. Ninajikuta kama mahala fulani sikumlinda. Alifariki ghafla, nikaambiwa ni presha. Toka tumezika, nimeshindwa kurudi makaburini.
Ninajihisi upweke mkuu, tulikuwa tukishirikiana kufanya mambo mengi pamoja. Hakika sijui namna sahihi ya kudeal na hii trauma.
Mwenye mbinu na aliyepita same situation anisaidie!
Nina sali, ninamwombea, sijioni kuwa sawa.