Msaada: Mmewezaje kupona maumivu ya kufiwa na mtu wa karibu?

Msaada: Mmewezaje kupona maumivu ya kufiwa na mtu wa karibu?

yes , wanne sasa! nimeadopt his son
Shukuru Mungu amekuachia huyo mtoto, mlee, mfanye kuwa faraja Yako Yani ukimuona upate Ile feelings damu ya mdogo ako inatembea kwenye mishipa ya huyo mtoto......na hivo ni wa kiume, mlee kama crown prince, aje aendeleze kizazi chenu.
Mola akujaze subira.
 
Wanajamvi, ninaomba msaada wa dhati kabisa.

Mdogo wangu wa pekee alifariki mwaka jana. Tulizaliwa wawili tu, wazazi pia walishafariki. Baada ya wazazi kufariki, nilikuwa mama yake, alikuwa baba yangu.

Fact kuwa familia hii nimebaki peke yangu, kila nikiwaza inanistrike vibaya mno! Sijui kama nimekubali kuwa hayupo tena au la.

Naogopa kukubali kuwa nimebaki peke yangu. Ninajikuta kama mahala fulani sikumlinda. Alifariki ghafla, nikaambiwa ni presha. Toka tumezika, nimeshindwa kurudi makaburini.

Ninajihisi upweke mkuu, tulikuwa tukishirikiana kufanya mambo mengi pamoja. Hakika sijui namna sahihi ya kudeal na hii trauma.

Mwenye mbinu na aliyepita same situation anisaidie!

Nina sali, ninamwombea, sijioni kuwa sawa.
Hapo ni kiongozi wa dini tu ndio atakurudisha kwenye mstari, kama wewe ni Muslim mcheki sheikhPonda
 
Shukuru Mungu amekuachia huyo mtoto, mlee, mfanye kuwa faraja Yako Yani ukimuona upate Ile feelings damu ya mdogo ako inatembea kwenye mishipa ya huyo mtoto......na hivo ni wa kiume, mlee kama crown prince, aje aendeleze kizazi chenu.
Mola akujaze subira.
Ahsante sana.
Nitaendelea kufanya hivyo
 
Pole sana Mungu akuongezee imani
Jaribu kutembelea vituo vya watoto yatima utoe chochote uwafariji kupitia kuwafariji utaanza kutibu moyo wako
 
Time is the best healer.
As the time goes on hali ya maumivu na ukiwa vitaenda vinapungua. Naelewa sio rahisi ku-cope na hiyo situation lakini angalau utakuwa sawa kiasi tofauti na ilivyosasa.
Endelea kumtumainia Mungu na kuyaenzi mema ya Marehemu.
Pole sana
 
Nina sali, ninamwombea, sijioni kuwa sawa.

Mchg. Elisha Muliri aliyepoteza mtu wake muhimu wa karibu anazungumza na wewe kukupa ushauri nasaha wa kiroho

Sikia ushuhuda wa mambo makubwa yaliyo mtokea baada ya kufiwa na aliweza vipi kuvuka atika wakati mgumu alio pitia.
Source : Lusungu Benjamini
 
yes , wanne sasa! nimeadopt his son
Pole kwa yote! Kuwa shupavu, najua una mengi mazuri ya kumkumbuka mdogo wako na ya kukufanya ujisikie unyonge, ila jaribu kuishi kama vile yupo, japo hutegemei kukutana naye. Kama unamuota, muote na ikupe faraja kuwa kuna njia mbadala unaweza kuwa naye.
Ukimuangalia mwanae, akupe nguvu ya kuona kuwa anaishi bila ya baba na maisha yanaendelea, uwe imara kwake, usimkatishe tamaa ya maisha kwa kukuona umnyonge na huna raha.
Kubaliana na uhalisia wa uanadamu wetu, leo tupo, kesho hatupo hatuna namna, bali kukubaliana na kila litutokealo. Mwenyezi Mungu azidi kuwasimamia wewe na familia yako!
 
Mchg. Elisha Muliri aliyepoteza mtu wake muhimu wa karibu anazungumza na wewe kukupa ushauri nasaha wa kiroho

Sikia ushuhuda wa mambo makubwa yaliyo mtokea baada ya kufiwa na aliweza vipi kuvuka atika wakati mgumu alio pitia.
Source : Lusungu Benjamini

ahsante sana!
 
Sikumbuki nilicoment hapa au la.Naona ni mwaka sasa ila naamini Mungu amekua mwaminifu kwako unaendelea vizuri.Muda ni tabibu mzuri Sana.
 
Wanajamvi, ninaomba msaada wa dhati kabisa.

Mdogo wangu wa pekee alifariki mwaka jana. Tulizaliwa wawili tu, wazazi pia walishafariki. Baada ya wazazi kufariki, nilikuwa mama yake, alikuwa baba yangu.

Fact kuwa familia hii nimebaki peke yangu, kila nikiwaza inanistrike vibaya mno! Sijui kama nimekubali kuwa hayupo tena au la.

Naogopa kukubali kuwa nimebaki peke yangu. Ninajikuta kama mahala fulani sikumlinda. Alifariki ghafla, nikaambiwa ni presha. Toka tumezika, nimeshindwa kurudi makaburini.

Ninajihisi upweke mkuu, tulikuwa tukishirikiana kufanya mambo mengi pamoja. Hakika sijui namna sahihi ya kudeal na hii trauma.

Mwenye mbinu na aliyepita same situation anisaidie!

Nina sali, ninamwombea, sijioni kuwa sawa.
Acha kuwaza sana Ndugu. Kaz ya Mungu haina makosa
 
Mungu ni Mwema dear!
Angalau now naona naweza maliza one or two days sometimes a week bila kulia, nafkr with time nitakuwa sawa!
THANK YOU kwa kujali kipenzi!
Hii nayo ni faraja tosha!
Ninakushukuru sana!
Mungu ataendelea kuimarisha
Ukiweza kutoa machozi toa tu,,hupunguza machungu

Pia usiache kupigia simu marafiki na uwapendao,kuelezea uchungu wako..ni tiba nzuri pia
Ila kubwa kuliko yote mueleze Mungu, na usichoke kumsihi aondoe maumivu.
 
Nikiwa mdogo nilkuwa na mawazo kwamba mimi ndo nife kwanza kabla ya mama yangu , sababu nampenda sana so sikutaka kushuhudia msiba wake, but unfortunately its 19 years now toka amefariki na yale maumivu nilokuwa nayaogopa ndo naishi nayo sababu kila kilichokuwepo kimebadilika..
Tusidharau mama zetu hata kama wao siyo wanaotafuta hela za matumizi ila utulivu wanaouleta kwenye familia ni kitu kikubwa sana ambacho hakipatikani kwa gharama yoyote ile.
 
Back
Top Bottom