Msaada: Mmewezaje kupona maumivu ya kufiwa na mtu wa karibu?

Msaada: Mmewezaje kupona maumivu ya kufiwa na mtu wa karibu?

Pole sana mkuu. Ndio maisha. Sometimes inabidi kuishi na maumivu...With atime utakua sawa
 
Najuta kusoma huu uzi nikiwa kwenye daladala,nmelia sana ,kufiwa kuacheni nyie.pole ndugu
 
Na ndo kazi yao watu wana ma masters n.k ili kutibu watu kama hao,ww hujakumbwa na tatizo la kisaikolojia, unadhani kulala njaa siku moja ni tatizo? Wanasaikolojia ni muhimu ngoja yakufike ndo utajuwa wana umuhimu gani?

Hakuna fani isiyotegemea MATATIZO ya watu ili iwepo, nitajie fani gani haitatui matatizo ya watu? Hata mpira upo kuleta furaha, kinyumw cha furaha ni nini!?
Katika umri wangu huu, unafikiri nimepitia mapito yaliyonyooka tu!! Kwa taarifa yako, nimepitia mapito mengi tu ya kimaisha! Na kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, nimeweza kuyashinda.
 
Wanajamvi, ninaomba msaada wa dhati kabisa.

Mdogo wangu wa pekee alifariki mwaka jana. Tulizaliwa wawili tu, wazazi pia walishafariki. Baada ya wazazi kufariki, nilikuwa mama yake, alikuwa baba yangu.

Fact kuwa familia hii nimebaki peke yangu, kila nikiwaza inanistrike vibaya mno! Sijui kama nimekubali kuwa hayupo tena au la.

Naogopa kukubali kuwa nimebaki peke yangu. Ninajikuta kama mahala fulani sikumlinda. Alifariki ghafla, nikaambiwa ni presha. Toka tumezika, nimeshindwa kurudi makaburini.

Ninajihisi upweke mkuu, tulikuwa tukishirikiana kufanya mambo mengi pamoja. Hakika sijui namna sahihi ya kudeal na hii trauma.

Mwenye mbinu na aliyepita same situation anisaidie!

Nina sali, ninamwombea, sijioni kuwa sawa.
Pole sana
Maumivu huwa hayaishi,ila huwa yanapumzika tu.

Amini amepumzika,Kuishi kwetu ni Kristo,Kufa ni faida.
 
sometimes huwa nawaza kheri nianze kuondoka mie ndo wafate wazazi wng..maana wakianza wao..sijui itkuaje..
Yarabbi tujaalie mwisho mwema na wazazi wetu.
 
Mkuu soma hiki kitabu utojuta kabisa
JamiiForums-1248131843.jpg
 
Wanajamvi, ninaomba msaada wa dhati kabisa.

Mdogo wangu wa pekee alifariki mwaka jana. Tulizaliwa wawili tu, wazazi pia walishafariki. Baada ya wazazi kufariki, nilikuwa mama yake, alikuwa baba yangu.

Fact kuwa familia hii nimebaki peke yangu, kila nikiwaza inanistrike vibaya mno! Sijui kama nimekubali kuwa hayupo tena au la.

Naogopa kukubali kuwa nimebaki peke yangu. Ninajikuta kama mahala fulani sikumlinda. Alifariki ghafla, nikaambiwa ni presha. Toka tumezika, nimeshindwa kurudi makaburini.

Ninajihisi upweke mkuu, tulikuwa tukishirikiana kufanya mambo mengi pamoja. Hakika sijui namna sahihi ya kudeal na hii trauma.

Mwenye mbinu na aliyepita same situation anisaidie!

Nina sali, ninamwombea, sijioni kuwa sawa.

Hii kitu ni changamoto sana na inaweza kukusababishia depression. Kitu cha kwanza kubali kuwa ni kweli si ndoto. Kitu cha pili badilisha namna ya maisha uliyokuwa nayo wakati akiwepo. Fanya marafiki wapya, anza kuishi upya. Usipende kukaa peke yako, kaa na watu wengi na ambao hasa hawajui lililotokea ili wasikupe pole au kukusikitikia na kukuonea huruma... Kama ni mtu wa kanisani nenda kanisani, imba kwaya, imba kwa sauti. Kama ni mtu wa dunia, nenda club kwenye kelele sana, cheza muziki, kidogo kidogo maisha yatachukua mkondo wake kadiri muda unavyoenda.
Nina ushuhuda na hili, mwaka 2011 nilifiwa na mwenza ambaye ilikuwa bado miezi miwili nifunge naye ndoa. Nilijikuta kama nataka kuwa chizi, shukrani kwa bosi wangu alivyogundua hili alinifanya kuwa busy kazini, kazi nyingi, kufoka mpaka nikaanza kuona nina changamoto kubwa sana ya kazi, na akawa hanipi pumzi. Baadaye akaja kuniambia sababu ya hayo na akaniambia sasa unatakiwa uanze upya na usipende kukaa peke yako. Leo 2023 ninaishi.

Mwisho nakupa pole sana mkuu.
 
Katika umri wangu huu, unafikiri nimepitia mapito yaliyonyooka tu!! Kwa taarifa yako, nimepitia mapito mengi tu ya kimaisha! Na kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, nimeweza kuyashinda.
Sawa. Hongera, so kila mtu anajuwa ataponea wapi sio kila mtu afate ulipo uponyaji wa mwingine dunia pana sana hii mkuu. Nadhani hatuwezi kufanana.
 
Yaani pole sana nimelia kama vile nakujua [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
Kwa kweli inasikitisha lakini hakuna kitu kinacho itwa coincidence, mambo yote yanafanyika kwa sababu, sasa my dear hao wapendwa wako wametangulia ili wewe uishi maisha mazuri kwenye hii Dunia yetu, jichanganye na watu smart, kama ni mfanya biashara au kazini au shuleni na ukumbuke your love ones wapo na wanakusaidia katika kila kitu!
Hata huu uzi pia umeanzisha ili upate namna ya kuishi, huu ni msukumo wao!
Kaa mbali na walevi na mijitu yenye tabia mbovu! Jaribu sana kutenda mema hata kama wakati mwingine una hasira, lakini kumbuka vitu vikishindikana nenda hospital na mwone psychologist ata kusaidia na wala usione aibu!
Kuna watu wengine wana shida katika hii Dunia na sio lazima kufiawa tu, kwenye mambo mengine!
Nakuombea kwa Mwenye Enzi Mungu mwenye wingi wa hekima asimame na asikie kilio chako,
Remain blessed in safe hands of The Almighty One [emoji3516]
 
Pole sana ndugu yangu kwa msiba huu mzito uliokupata! Kusahau siyo rahisi sana itachukua muda mrefu. La msingi ni kupambana na zile hisia ( maumivu, huzuni n.k) unazosikia wakati unapomkumbuka hizi ndizo zinazosababisha matatizo. Kulingana na imani yako lazima ujue mambo yafuatayo; Mwenyenzi Mungu afanyi makosa inatakiwa ukubali kwamba ni amri yake na kwenye hii dunia tunapita tu ni suala la muda. Ongeza sala za usiku kwa hakiki utapata faraja na matumaini mapya Inshallah!
 
Wanajamvi, ninaomba msaada wa dhati kabisa.

Mdogo wangu wa pekee alifariki mwaka jana. Tulizaliwa wawili tu, wazazi pia walishafariki. Baada ya wazazi kufariki, nilikuwa mama yake, alikuwa baba yangu.

Fact kuwa familia hii nimebaki peke yangu, kila nikiwaza inanistrike vibaya mno! Sijui kama nimekubali kuwa hayupo tena au la.

Naogopa kukubali kuwa nimebaki peke yangu. Ninajikuta kama mahala fulani sikumlinda. Alifariki ghafla, nikaambiwa ni presha. Toka tumezika, nimeshindwa kurudi makaburini.

Ninajihisi upweke mkuu, tulikuwa tukishirikiana kufanya mambo mengi pamoja. Hakika sijui namna sahihi ya kudeal na hii trauma.

Mwenye mbinu na aliyepita same situation anisaidie!

Nina sali, ninamwombea, sijioni kuwa sawa.

Ni jambo gumu, ila jionee Huruma, and do your best kuwa na ukaribu na watu hasa Kanisani au msikitini, na kama ni Mkristo, kuna mistari mingi sana ya biblia ya kukupa tumaini.

The only way to change namna unavgofikiri ni kubadili fikra zako na maneno ya Mungu yenye kuleta tumaini, ukila hayo maneno mda mrefu hubadilika na kuwa hai na halisi.

Exchangw your sad mawazo na maneno na ahadi za faraja za Mungu, with time nakuhakikishia utapata faraja ya ajabu sana sana na utasahau shida.

Usikubali kuijaza hiyo hali na faraja zisizo faa za mahusiano na wanaume ambao wanaweza itumia hiyo nafasi kukutumia na kukucheze.

Mungu akusaidie dogo.
 
Mungu akutie nguvu mkuu uweze kuachilia maumivu na kuwa sawa japo sio rahisi ila utakua sawa tu. Kwa upande wangu niliondokewaga na wazazi wote wawili mwaka mmoja walipishana mwezi tu, nikiwa darasa la pili, na hapo nilibaki peke angu mdogo angu alikufa alivozaliwa tu.
Muda mwingine nasemaga tu Mungu asante uliwachukua mapema nishazoea kuwa alone kwamba sina wazazi wala ndugu wa damu (japo natamani dogo angekua hai) , Sawa unakua na ndugu wengine but hamuwezi kuwa na bond kama ya ndugu yako wa damu.
Usijilaumu sana wewe sio sababu ya yeye kufa ni kazi ya Mungu tu.
Pole sana Mkanaani
 
Kufiwa ni kitu Cha kawaida sana ila maumivu utayapata ila DUNIANI ni njia tu
 
Pole sana rafiki, najua ni ngumu ila Mungu wetu mkuu akupe faraja ya roho Insh Allah.
 
Back
Top Bottom