Msaada: Mmewezaje kupona maumivu ya kufiwa na mtu wa karibu?

Msaada: Mmewezaje kupona maumivu ya kufiwa na mtu wa karibu?

Kama umeolewa mume wako na watoto wako ndo wawe faraja yako.

Kama hawapo karibu nawe inabidi utafute hobby itakayokufanya uwe busy.
 
nashindwa hata kutoa ushauri coz I can feel your pain darling ,maana situation Yako viatu havintoshi vyanibana hasaaa,Mungu akupe ponyo dear
 
Big sis; hakiiiiiiii...........

I remember kuna siku ulisimulia kitu like mkiwa wadogo; mdogo wako alibanwa na pumu na mlikuwa mmefungiwa sijui pasipo msaada wowote; ikakubidi uvunje mlango kuhakikisha mdogo wako anatibiwa (kama nakumbuka vizuri ulimshikia panga mlezi wenu alipokuwa harespond chochote kuhusu kumpeleka mdogo wako hospital).......Ilinifanya nione how much ulikuwa unampenda mdogo ako; how exactly big sisters are.

Tunajikutaga sisi ndiyo kama mama wa wadogo zetu na sio madada tena. I know what she/he meant to you; she/he was the only thing left for you after you both lost your parents; you found strength and purpose to live just for her/him. I can imagine how her/her death has hit you. Daah yaani naona hata kutype "pole sana" ni kama daah. Mungu akutie nguvu dada mkubwa.

Please you need to do a closure. Hiyo hatia uliyonayo kwamba maybe hukumlinda ipasavyo ndiyo maana imefariki; inabidi iondoke sasa. Jisamehe kabisa
Kama unaweza kwenda alipozikwa; fika frequently. Mimina moyo wako; ongea yote ambayo unatamani umwambie hata kama hakusikii; I know utalia vya kutosha na kwa kiasi fulani utapata amani ya moyo.

Wakati wa mtu kufa ukifika; hakuna utakachoweza kufanya kuzuia mauti yasimpate. Amini tu wakati wake ulifika; na hata asingekufa kwa presha; angekuwa tu hata kwa ajali au malaria. His/her time was simply up.

Hata katika machozi na uchungu wako mkuu ulionao; usiache kumshukuru Mungu. Mshukuru Mungu hata alikupa Neema ya kuwa na mdogo wako kwa miaka yote hiyo aliyokupa; imagine asingekuwepo na huku wazazi hawakuwepo pia. Mshukuru Mungu amekuachia na mtoto wake wa pekee ambaye ndiyo kumbukumbu halisi ya mdogo wako. Mshukuru Mungu hata umepata nafasi ya kumuona kwa mara ya mwisho na kumpumzisha kwenye nyumba yake ya milele; at least unaweza kwenda kumtembelea kaburini kwake na ukafeel uwepo wake. Imagine wale ambao wapendwa wao wametoweka hawajulikani hata walipo; whether wapo hai au wamekufa; imagine familia zao zinaishi kwenye sintofahamu ya namna gani au unaambiwa tu ndugu yako wamepata ajali ya meli imezama, na miili yao haionekani. So ukija kuangalia; bado zipo sababu nyingi tu za kumshukuru Mungu katika hili pia. Take heart big sis; Mungu atakuvusha katika hili. Usiache kuomba, usiache kuongea na watu; toa yote yaliyo moyoni mwako. It shall be well with you big sis

Sent using Jamii Forums mobile app
yAAAH!
Huyu was a son to me.
Watoto wangu walikuwa wanasema kabisa mama yani Uncle knows unampenda kiasi gani!
Mimi huwa napenda kuvaa raba na mashati ya draft over the weekend!
Ilikuwa tunavaliana na kununuliana.
Niliwahi kulazwa wakati fulani, nikawa naishi peke yangu.
Alihama nyumbani kwake na mkewe na mtoto wake, wakaja kukaa kwangu mwezi!
Ilikuwa anakuja hospitali anakaa hapo kitandani , mi nalala naamka namkuta!
Anafua nguo zangu, ananilisha na kuhakikisha nimeoga ndo anashuka chini anapiga story na walinziiii, ili wamruhusu awe anakuja kuniangalia usiku!
Mahala fulani nilidhulumiwa karibu 5m. Alipojua, alihakikishwa nalipwa na ya usumbufu , pesa niliyodai karibu miaka 3. Alihakikisha inalipwa ndani ya miezi 3.
Yani naomba nikwambie Oddo! Nashindwa hata kumlilia, sijui namliliaje!

Maisha yangu yamebadilika hasa.
Nimekuwa mtu mwingine sana!
Najikaza nacheka, natembea, nafanya projects zake aliachilia katikati!
Just kutamani kutimiza ndoto zake!
Bado najikuta nina ombwe.
Alikuwa ndo msiri wangu, kuna vitu nafkr nitavipoteza just because yeye hayupo!
Naomba sana niweze kuvuka hapa!
Ila Mungu wa Mbinguni anajua nimeondokewa na mtu wa aina gani!
 
Ni rahisi kusema chochote lakini Kwa tuliopitiwa na Hali ya mtoa mada tuna jua anamanisha nini.pole sana mdau hiyo njia ni yetu sote be positive na trust in God Kwa kuwa hutoa na hutwaa.
 
Wanajamvi, ninaomba msaada wa dhati kabisa.

Mdogo wangu wa pekee alifariki mwaka jana. Tulizaliwa wawili tu, wazazi pia walishafariki. Baada ya wazazi kufariki, nilikuwa mama yake, alikuwa baba yangu.

Fact kuwa familia hii nimebaki peke yangu, kila nikiwaza inanistrike vibaya mno! Sijui kama nimekubali kuwa hayupo tena au la.

Naogopa kukubali kuwa nimebaki peke yangu. Ninajikuta kama mahala fulani sikumlinda. Alifariki ghafla, nikaambiwa ni presha. Toka tumezika, nimeshindwa kurudi makaburini.

Ninajihisi upweke mkuu, tulikuwa tukishirikiana kufanya mambo mengi pamoja. Hakika sijui namna sahihi ya kudeal na hii trauma.

Mwenye mbinu na aliyepita same situation anisaidie!

Nina sali, ninamwombea, sijioni kuwa sawa.
Upe muda nafasi,hata kama itachukua miaka kadhaa lakini ipo siku utakuja kuwa sawa na utaweza kwenda hata kaburini kwake.

It's very ok kwa sasa kupitia hali uliyonayo kwakuwa bado una maumivu makali ya kumpoteza,lakini with time utaanza kidogo kidogo kuukubali uhalisia.Mkumbuke yule mtoto Anna aliyepoteza familia yake yote na kubaki mwenyewe,wakumbuke na wengine waliofikwa na misiba kama wewe.Ukishaona hivyo utajikuta unamshukuru Mungu kuwa si wewe peke yako unaepitia kipindi hicho.
 
Pole sana ndugu. Jipe moyo huku ukimtizama Bwana Yesu
 
Mkuu ni mda tu hakuna kingine,mm nilifiwa na mama mzazi mwaka 2019,nili sumbuka sana ata nikiwa kwenye gari nasafari nilikua naumia sana mpaka nalia kabisa.

Lakini kwa sasa nimezoea na kukubaliana na hali hiyo na hakuna jinsi yoyote mpangaji wa yote ni Mungu, pia siyo mm pekee nilipitia hayo mazingira.
 
Jisamehe wewe mwenyewe, msamehe yeye. Wasamehe wote unaodhani hawakufanya yanayopasa na mapungufu yalotokea wakati kabla na baada ya msiba.

Pia msamehe Hata Mungu, na kila mtu. Isamehe Dunia. Na uumbaji wote. Hiyo itakuwa dawa. Kubwa.
Maana msamaha ni zaidi Dawa.
 
Unatakiwa utambue kwanza hayo maumivu yanasababishwa na nin, ukishajua unaweza kuyashughulikia kutokea kwenye chanzo.
 
Wanajamvi, ninaomba msaada wa dhati kabisa.

Mdogo wangu wa pekee alifariki mwaka jana. Tulizaliwa wawili tu, wazazi pia walishafariki. Baada ya wazazi kufariki, nilikuwa mama yake, alikuwa baba yangu.

Fact kuwa familia hii nimebaki peke yangu, kila nikiwaza inanistrike vibaya mno! Sijui kama nimekubali kuwa hayupo tena au la.

Naogopa kukubali kuwa nimebaki peke yangu. Ninajikuta kama mahala fulani sikumlinda. Alifariki ghafla, nikaambiwa ni presha. Toka tumezika, nimeshindwa kurudi makaburini.

Ninajihisi upweke mkuu, tulikuwa tukishirikiana kufanya mambo mengi pamoja. Hakika sijui namna sahihi ya kudeal na hii trauma.

Mwenye mbinu na aliyepita same situation anisaidie!

Nina sali, ninamwombea, sijioni kuwa sawa.
Pole kwa kufiwa na watu wako wa karibu shemela wangu

Hebu sogea huku Bunju nikufariji
 
Wanajamvi, ninaomba msaada wa dhati kabisa.

Mdogo wangu wa pekee alifariki mwaka jana. Tulizaliwa wawili tu, wazazi pia walishafariki. Baada ya wazazi kufariki, nilikuwa mama yake, alikuwa baba yangu.

Fact kuwa familia hii nimebaki peke yangu, kila nikiwaza inanistrike vibaya mno! Sijui kama nimekubali kuwa hayupo tena au la.

Naogopa kukubali kuwa nimebaki peke yangu. Ninajikuta kama mahala fulani sikumlinda. Alifariki ghafla, nikaambiwa ni presha. Toka tumezika, nimeshindwa kurudi makaburini.

Ninajihisi upweke mkuu, tulikuwa tukishirikiana kufanya mambo mengi pamoja. Hakika sijui namna sahihi ya kudeal na hii trauma.

Mwenye mbinu na aliyepita same situation anisaidie!

Nina sali, ninamwombea, sijioni kuwa sawa.
Inategemea una miaka mingapi na wewe ni wa jinsia gani.

Kama ni mwanamke na bado ni mdogo hapo hakuna namna ya kukusaidia. Wanawake ndo mko hivyo, ni watu wa kulia misibani.

Na watu kama wewe ni mtaji mkubwa kwa wale matapeli ambao wanasemaga wana uwezo wa kuongea na waliokufa wakuunganishe nao.

Ila kama ni mwanaume hiyo sio ishu. Watu hufa, tunazika maisha yanaendelea. Tunazika wazazi na watoto wetu wa kuzaa, sembuse mdogo mtu bwana!

Mwisho kabisa ni zaa. Kwa kuwa umebaki peke yako katika uzao wa wazazi wako, basi ongeza spidi ya kuzaa ili uendeleze uzao wa wazazi wako.
 
Pole sana mkuu,binafsi ninapitia maumivu kama ya kwako.Nimefiwa na mama yangu mwaka jana na baba sina.Nimebaki mimi ni mdogo wangu.

Kuna muda ninajikuta machozi yananitoka tu hata mbele za watu,nina shindwa kujizuia.

Kinachonitesa zaidi ni kumbukumbu,hivyo kuna wakati nina amua kijifungia ndani na kulia kwa muda mpaka uchungu utakapo pungua.Lakini pia nina sali sana kumuomba Mungu anipe faraja maana kwa huyo pekee nitafarijika.

Lakini pia,Muda ni daktari mzuri
 
Atakuwa ni mwanasaikolojia bila shaka. Hivyo anatengeneza mazingira ya kazi kupitia matatizo ya mtu.
Na ndo kazi yao watu wana ma masters n.k ili kutibu watu kama hao,ww hujakumbwa na tatizo la kisaikolojia, unadhani kulala njaa siku moja ni tatizo? Wanasaikolojia ni muhimu ngoja yakufike ndo utajuwa wana umuhimu gani?

Hakuna fani isiyotegemea MATATIZO ya watu ili iwepo, nitajie fani gani haitatui matatizo ya watu? Hata mpira upo kuleta furaha, kinyumw cha furaha ni nini!?
 
Ichukue kila siku kama inavyokuja, ukiamka na donge zito la kutaka kumlilia we lia tu, ukihisi kupiga kelele sababu ya uchungu ulionao basi fanya hivyo. Baada ya muda utazoea hali halisi.

Epuka kukaa pekee yako, jaribu kujichanganya na watu. Ni ngumu kukubaliana na ukweli ila moja ya shani kubwa ya Mungu ni kutuumba binadamu na usahau.

Muhimu zaidi ya yote ni kusali sana kwa Mungu na kushukuru Mungu pia kwa lililokutokea maana ya Mungu yote yana sababu zake. Nakuombea sana kwa Mungu akupe amani ya nafsi na ampe pumziko la milele mpendwa ndugu yako.
 
Back
Top Bottom