Mkuu Mzee Mukaruka: Kilimo cha green house ni kilimo ambacho ni cha hatua kubwa zaidi. Ni kilimo cha kulimia ndani ya mabanda ya nailoni. Mabanda haya yanapitisha mwanga vizuri tu na yanakinga mimea dhidi ya mvua inayosababisha magonjwa mara nyingi kwenye mimea, inakinga mimea dhidi ya joto kali au baridi kali kutegemea na lilivyotengenezwa. Banda hilo hukinga mimea dhidi ya magonjwa mengi na wadudu wengi washambuliao mimea. Mara nyingi kilimo hiki cha green house huendana na matumizi ya umwagiliaji kwa njia ya matone kwa hiyo mahitaji ya maji ni kidogo. Kilimo cha kwenye green house kinatoa mavuno makubwa sana ukilinganisha na kilimo cha nje, kwa mfano nyanya hufikia kuzaa mara 10 ya uzazi ukilinganisha na nyanya iliyopandwa nje kwa eneo sawa. Kwa kuwa mazao yanalimwa kwenye mazingira yaliyodhibitiwa (controlled environment) mazao huweza kustawi vema mwaka mzima, tofauti na kilimo cha nje ambapo hali ya hewa majira fulani huathiri uzaaji na ustawi wa mazao.
Pamoja na kwamba kilimo cha Green house kinatoa uhakika mkubwa sana wa kupunguza risk katika uzalishaji wa mazao ni Technolojia ghari. Gharama inategemea iwapo green house imetengenezwa kwa vyuma au mbao (na miti). Green house ya vyuma inadumu zaidi ya miaka 10, bei zake hutegemea ukubwa wake, green house ya eneo 15 m x 8 m inaweza kugharimu kuanzia mil 3 na kuendelea. Green house ya mbao inaweza kuwa nusu ya bei ya green house ya chuma. Ikitengenezwa vizuri inadumu zaidi ya miaka miwili hasa kama mbao zitadhibitiwa zisioze na kuliwa na mchwa.
Nimeambatanisha link kama utafanikiwa kuzifungua zitakusaidia upate picha halisi.
kilimokisasa - Construction of A Greenhouse
kilimokisasa - Construction of A Greenhouse
Hapa Tanzania kampuni ya BALTON Tanzania Ltd ndiyo imejikita kuuza vifaa vya kutengenezea green house. Wao hawajihusishi kutengeneza green house za mbao bali wanauza set nzima ya greenhouse za chuma na nadhani wanatoa msaada wa utaalamu wa kuijenga. Nimekuwekea anwani yao hapa uweze kuwasiliana ili ujue bei zao kwa sasa.
BALTON DAR ES SALAAM
Mikocheni Light Industiral Area, 23 Coca Cola Road
PO Box 712
Dar Es Salaam, Tanzania
Tel: 00 255 22 277 2826 / 00 255 22 277 2831
Fax: 00 255 22 277 5989
Mob: 00 255 754 332 214 / 00 255 754 320 925barua pepe:
balton@baltontz.com
Mwisho namalizia kwa kukueleza kuwa kutokana na ughari wa green house, mazao yanayoshauriwa kulimwa ni yale yenye bei kubwa na uwezo wa kuzaa kwa kipindi kirefu ili uweze kurudisha pesa na kupata faida. Mazao hayo ni kama Nyanya (aina maalum kwa greenhouse - mfano Anna F1), pilipili hoho na matango. Green house zinatumika zaidi mkoani Arusha kwenye kilimo cha Maua. Ni mazao ya bei mbaya tu ndiyo hulimwa humo siyo mahindi wala alizeti.