Msaada,mtaji wa mil.3 kwa mwanza nifanye biashara ipi

Msaada,mtaji wa mil.3 kwa mwanza nifanye biashara ipi

Mkuu maundumula, kujenga green house kimagumashi inawezekana sana, kama unaweza kuview you tube sema nikuelekeze utazame inavyotengenezwa kimagumashi! Unaweza kupunguza gharama hadi nusu ya bei ya green house ready made. Green house ready made ni basically za vyuma hizi za kimagumashi ni za miti na mbao, nailoni na mfumo wa umwagiliaji ni ule ule haijalishi ni aina gani. Ukionaje unaweza uchana na mfumo wao wa umwagiliaji ukatumia watering can.

Mkuu inategemeana na aina ya unacho taka Kupanda, na hata hivyo vitu kama Nylon bado ni ghali sana kwa sababu si kwamba unatumia hizi nylon unazo zijua wewe, kuna Nylon special kwa ajili ya green house, hizi zingine unazo jua hazifai hata kidogo,

Kwanza ni lazima ujue why green house? make si kwamba ni fasheni tu kufanya green house
 
Chasha,

Inamaana kilimo cha Nyanya kwenye Greenhouse hakilipi?
 
Hizo Nylon zinapatikana wapi mazee?
 
Chasha,

Inamaana kilimo cha Nyanya kwenye Greenhouse hakilipi?

Sijasema hakilipi, ila n lazima kwanza ufanye analysis ya kutosha kuangalia kama ukiwekeza huko ni swa au si sawa, unatakiwa uangalie cost zilivyo nabei ya kuuzia, kwa sababu unweza ukawa wewe unatumia ghalama kubwa mwisho wa siku unaenda kushindana sokoni na wanao lima kikawida
 
Chasha,

Inamaana kilimo cha Nyanya kwenye Greenhouse hakilipi?

Sijui kwa Dar ila Mara nyngi zinaagizwa Nairobi, Ila wale wazungu wanao lima maua utaona kwamba zile nyumba zao ni kama kwa pembeni ni Vitambaa fulani vigumu na kwa juu ndo Nyloni
 
Mkuu inategemeana na aina ya unacho taka Kupanda, na hata hivyo vitu kama Nylon bado ni ghali sana kwa sababu si kwamba unatumia hizi nylon unazo zijua wewe, kuna Nylon special kwa ajili ya green house,hizi zingine unazo jua hazifai hata kidogo,

Kwanza ni lazima ujue why green house? make si kwamba ni fasheni tu kufanya green house

Mkuu ninajua ninachokiandika. Ninazifahamu Green house kuanzia historia yake, aina zake, materials zake na requirements zake. Nilishazitumia Ulaya na Kenya ambako wako mbali kwa teknolojia hii. Kenya wanatumia sana green house kwa kiasi kikubwa sana kuanzia pwani ya Mombasa hadi Kisumu! Kenya wamezichakachua na kutengeneza za mbao kupunguza gharama yake. Hizi ndiyo Mkuu Maundumula alikuwa anaulizia za magumashi. Hapa Tanzania green house zinatumika sana kwenye kilimo cha Maua huko Arusha/Moshi. Kwetu Tanzania hivi sasa ndiyo uhamasishaji na uelimishaji wa kuzalisha mbogamboga kwa green house ndiyo unaanza.

Kwa mtu ambaye hajawahi kuona green house nikimweleza kuwa inajengwa kwa Nylon anaelewa vizuri sana, lengo ni kumfanya apate concept, nikiingia deep hadi kumweleza specifics za nylons to the level of microns 200 au 400 mtu ambaye hata hajui green house itakuwa ni kutojua hatua za kuelimisha mtu. Kadharika kwenye thread hii zipo attachments ambazo zinapicha na maelezo kuhusu green house za chuma na za mbao (magumashi).

Pia suala la ughari hili linaeleweka na kwenye thread hii nimeliweka bayana wakati wote kwamba green house ni expensive ndiyo maana hata mazao ya kupanda ni yale yenye bei kubwa tu.

Wadau mjitahidi mfungue hizo atachment muone hizo picha ili muone iwapo hizo nylon ni za kufungia chumvi au ni nylon maalum. Ninajua ninachokiandika na tusigombanie fito wakati tunajenga nyumba ile ile.

Nimeshafahamu baadhi ya wasomaji hawapitii mtiririko wa thread nzima, Mkuu Chasha umekuwa mwelimishaji mkubwa sana wa ujasilia mali humu jukwaani usianze kupingana na mafunzo ambayo wewe mwenyewe unayatoa kuhusu business ideas na watu kuthubutu, wenzetu Kenya wameweza na wamepiga hatua sana kwa green house technology. Huyo mdau aliyeanzisha thread ana 3m huyo anaweza. Tusiwachanganye wasomaji.
 
Green house farming ndiyo emerging fashion for growing valuable vegatable crops! Ni kilimo kinacholipa sana mijini, eneo dogo tu hapo mjini unatoa mzigo mkubwa kuzidi mtu mwenye shamba huko bush. Hivi sasa kwa mwenye hamu ya kulima hata mjini unawelima kama vile inavyofugwa mifugo mijini! Kama unaweza kumudu gharama, green house kwa sasa ni fashion mpya ya kilimo Tanzania inayolipa sana!
 
asante sana mkuu Kubota inaonekana uko fiti kwa ujasiliamali, vipi unaweza ukawa na idea na duka la vifaa vya ujenzi? kama inahitaji mtaji wa namna gani? asante in advance
 
Last edited by a moderator:
asante sana mkuu Kubota inaonekana uko fiti kwa ujasiliamali, vipi unaweza ukawa na idea na duka la vifaa vya ujenzi? kama inahitaji mtaji wa namna gani? asante in advance

Kwi kwi kwiiiii, ha ha hahaaaaaa, Mkuu Igudungwa mimi siko fiti sana kwenye kila ujasiliamali bali masuala ya Kilimo zaidi napo siyo kila kitu, kuna anga zangu ambazo ukiingia nitakuchimbulia toka mzizi hadi suke. Masuala ya ujenzi mkubwa wangu mimi ni mbu mbu mbu kabisa. Ila ukifanya bidii kutafuta kunathread humu JF ambako swali hilo liliwahi kuulizwa.
 
Mkuu heshima kwako kwa michango yako kwenye huu uzi
Hivi ukiagiza greenhouse toka Kenya au China inaweza kupunguza gharama kidogo na ukinunua humu nchini? Vp kama utataka pipes za drip irrigation tu bila green house gharama zake zikoje?
 
Nakushauli fuga kuku wa asili huo ni mtaji mkubwa sana mimi ni mzaliwa wa mwanza kwetu nyamanoro kwangu kawekamo mtaa wa kawekamo zamani msumbiji kwasasa niko biharamlo kagela natafuta maisha ninauzofu na ufugaji wa kuku nimepatasemina {SUA}
 
Ukipenda nitakutafutia na eneo la kufugia na nitakusaidia kwa kadili ya uwezo wangu bule sihitaji malipo m.2 zitatosha kwa mtaji na banda ukianza mwezi wa nne tegemea mwisho wa mwaka kupata m.6 faida kwa kadilio la chini na mtajiwako ukopalepale
 
Mkuu heshima kwako kwa michango yako kwenye huu uzi
Hivi ukiagiza greenhouse toka Kenya au China inaweza kupunguza gharama kidogo na ukinunua humu nchini? Vp kama utataka pipes za drip irrigation tu bila green house gharama zake zikoje?

Mheshimiwa sana SABAYI kuhusu kuagiza greenhouse ili kujua kujua kama inalipa inabidi kulinganisha bei ya Balton Tanzania (ambao ndiyo supplier ninaowafahamu kwa Tanzania) na bei za Kenya. Sijawahi kusikia wala kufahamu bei za Balton Tanzania nami nitajishughurisha kuulizia sasa. Kwa bei za Kenya ninakuwekea Attachment hapa ujionee mwenyewe bei zao na ulinganishe na bei za Balton. Kuna post hapo nyuma inacontacts zao na wewe utatuupdate kwa utakayoyaona huko. Kuagiza China ni cheap sana isipokuwa inategemea na mizengwe ya Bandarini Dar. Inaweza kuwa cheap sana sana sana kuagiza China lakini wachawi waliopo bandarini Dar es Salaam hilo ni janga la maendeleo ya kitaifa. Mimi niliagiza kifaa China meli ilishapakua mzigo tangu tarehe 25 Feb hadi leo tarhe 18 March karibia tutafunga mwezi bado wanajizungusha tu. Ukiagiza China uwe mvumilivu tu lakini inaweza kuwa nafuu zaidi na hasa mzigo ukiwa mkubwa.
 
Attachments

Chasha/kubota,

Hivi nikimtafuta fundi wa kuchomea mageti wa uswahili nikampa design namwambia nijengee kama kahema fulani nataka kukisimika huko kijijini kwangu akanijengea then nahangaioka kutafuta hizo Nylon si nitakuwa nime save sana?
 
Ubarikiwe sana kaka next time pitishia Mombasa then unasafirisha hadi TZ hii nchi imeshikiliwa na Mafisadi kila kona nchi inawenyewe hii
 
Chasha/kubota,

Hivi nikimtafuta fundi wa kuchomea mageti wa uswahili nikampa design namwambia nijengee kama kahema fulani nataka kukisimika huko kijijini kwangu akanijengea then nahangaioka kutafuta hizo Nylon si nitakuwa nime save sana?

Mkuu Maundumula, unaweza kuokoa pesa nyingi sana na hiyo inaweza kukufanya ukajenga green house kubwa zaidi. Ndugu zangu baada ya kuona picha halisi ilivyo kinachofuata ni ubunifu wa kila aina ili mradi kuhakikisha mazingira ndani ya hilo hema yanaruhusu mimea kukua. Hizo nylon maalum huwa zinauwezo wa kuchuja mionzi ya jua kiasi kwamba kipindi cha joto kali mimea humo ndani haiathiriki kwa hiyo hata ukijenga kwa vyuma au iwe mianzi au fito za miti, nguzo na boriti kikubwa utahitajika kununua hizo nyloni maalumu na wavu kwa ajili ya kuingizia hewa. Pia ni muhimu kukumbuka kuwa upepo huwa ni kikwazo pia hivyo inapaswa kuzingatia kuepuka kuezuliwa kirahisi.
 
Anzisha stationary nyamalango italipa maana milion 1.5 utapata photocopy 1milioni chumba na laki tatu desktop laki mbili rim wino na extension cable..... all the best.
 
Back
Top Bottom