Mkuu natumaini makala hii itakusaidia
MAJIBU YA SWALI KUHUSU UKATAJI KIMEO kwa watoto
Haya ni majibu kwa swali alilouliza mdau kupitia blogu za Issa Michuzi na Ahmad Michuzi kuhusu 'ukataji kimeo kwa watoto' na yafuatayo ni maelezo toka kwa Dk. Mkopi aliyepo katika kitengo cha Magonjwa ya Watoto katika hospitali ya Muhimbili.
Kimeo (uvula) ni nini?
Kimeo ni sehemu ndogo ya kinywa inayoning’inia mkabala na mwisho wa ulimi. Hivyo kila mtu huzaliwa na kimeo na kimeo sio ugonjwa.
Kazi ya kimeo ni ipi?
- Husaidia kinga ya mwili
- Husaidia kulainisha koo
- Husaidia kutoa sauti.
Je kwanini watu hukata kimeo?
Kutokana na elimu potovu juu ya kimeo; mfano: Kimeo kimevimba na kikipasuka tu mtoto ndo anakufa, Kimeo kina usaha, Kimeo ni kirefu sana. n.k.
Watu wengine hufikiri kuwa kimeo kinasababisha magonjwa kama vile:- Kukohoa muda mrefu, au Kukonda au Kutapika mara kwa mara au Mtoto kulialia bila sababu. Hii si kweli.
Je ni sahihi kukata kimeo?
HAPANA! Kimeo hakipaswikukatwa kutokana na sababu yeyote ile!
Nini madhara ya ukataji wa kimeo?
Mtoto anaweza kupoteza damu nyingi na kupoteza maisha Maambukizi ya magonjwa mbalimbali kutokana na kutumia vyombo ambavyo si salama kukatia kimeo; mfano:- Pepopunda, Homa ya mapafu, Maambukizi ya VVU, Mototo kupata maumivu makali au Kupaliwa na chakula kupitia puani.
Tufanyeje/Jitihada gani zifanyike ili kuzuia madhara haya yasitokee?
Watoto wanao kohoa muda mrefu, wasiokua vizuri, wanaotapika mara kwa mara, n.k. wapelekwe kwa daktari kwa ajili ya uchunguzi na tiba mbadala!