Msaada: Mtoto ana kitu wanaita kimeo

Msaada: Mtoto ana kitu wanaita kimeo

kanewi

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2012
Posts
298
Reaction score
200
Naulizia kama kuna tiba au huduma yake ikoje, kuna mtoto ana ile wanaita Kimeo, hospitali wameangalia ameonekana nacho na nimewazuia wazazi kwenda mtaani kukikata, sasa naomba mnisaidie maana wa hospitali wamempa dawa ya kukohoa tu na anakohoa mwanzo mwisho.
 
Kimeo au kilimi mara nyingi naona watoto hukatwa. Nishawahi kusikia wapo wanaopona kwa dawa za asili.
Mpe hiyo dawa ya kikohozi atumie dozi ikiisha hajapona rudini hospital kwa uchunguzi zaidi.
 
Huwa wanakata mitaani lakini ni hatari sana!! Kwani hapo hospitalini wamekuambiaje kuhusu imani ya kukikata? uko mkoa gani? nauliza kwa nia njema lakini
 
Tafuta wataalamu wazee anakikata tu anampa dawa ndani ya siku kadhaa anakuwa fit
 
Sikushauri wakikate kwa sababu huwezi kujua kwann kimeongezeka ukubwa.
Jaribu kwenda hosp nyngne hyo inapona bila kukikata anapewa dawa tuu.
Lkn pia kukohoa sana si kukua kwa hicho kilimi hata minyoo hupelekea kukohoa pia hivyo kama hajapatiwa dawa za minyoo kwa muda mrefu jaribu mpatia pia.
 
Naulizia kama kuna tiba au huduma yake ikoje, kuna mtoto ana ile wanaita Kimeo, hospitali wameangalia ameonekana nacho na nimewazuia wazazi kwenda mtaani kukikata, sasa naomba mnisaidie maana wa hospitali wamempa dawa ya kukohoa tu na anakohoa mwanzo mwisho.
Alipelekwa hospitali au zahanati?
 
Mara nyingi watanzania huwa wanavikata kienyeji tu. Mi kijana wangu alisumbua sana, wakasema anacho, mazingira yaliforce kumkatia na ikawa successful na siku c2 baadae akawa safi kabisa.
 
Sikushauri wakikate kwa sababu huwezi kujua kwann kimeongezeka ukubwa.
Jaribu kwenda hosp nyngne hyo inapona bila kukikata anapewa dawa tuu.
Lkn pia kukohoa sana si kukua kwa hicho kilimi hata minyoo hupelekea kukohoa pia hivyo kama hajapatiwa dawa za minyoo kwa muda mrefu jaribu mpatia pia.
Mkuu naomba maelezo zaidi ya minyoo na kukohoa??
Watoto wangu wanaamka saa 11:45 asubuhi kujiandaa kwenda shule na basi la shule na hapo huzunguka mitaani basi likipitia wengine mpaka hata saa 1:30 asubuhi ndio hufika shule. Changamoto nilionayo ni kila muhula wanaugua sana vikohozi, mara zote imekuwa wakianza kwenda shule tu. wakiwa likizo wanakuwa fit kabisa, hawa minyoo wanapatikanaje (mazingira)
 
Mara nyingi watanzania huwa wanavikata kienyeji tu. Mi kijana wangu alisumbua sana, wakasema anacho, mazingira yaliforce kumkatia na ikawa successful na siku c2 baadae akawa safi kabisa.
Unaweza nisaidia gharama zake na ni wapi?
 
Kama upo dar, nenda uwanja wa ndege maeneo ya karakata, ulizia kwa mzee NASORO MKATA KIMEO.
Hata mbagala langitatu msikitini yupo anakata kunafoleni kushinda hospital wahi SAA 12 mwisho SAA sita hii tiba nilikua naidharau uzungu mwingi mtoto alikua anakohoa hadi anatoa chozi kama mzazi nikaenda Sikh mbili tu wakati zakhem hospital kanywa vichupa utafikiri Nina pharmacy ndani
 
Alimpeleka Muhimbili kwenye wa kinywa, walikiangalia wakakiona na kumpatia dawa ya kukohoa tu
Kama ni Muhimbili nakushauri endelea kumpa dawa uliyopewa. Hii biashara ya kupeleka watoto kwa wakata vimeo mtaani sikushauri kabisa
 
Mkuu nikiwa na umri wa miaka 7 hivi mwaka2002 niliwahi kukatwa pale Hospital X kwa Siri sana .... Yaani sijui kwanini wanakata kilimi kwa Siri kiasi hicho aisee .....lakin ukikiacha kikaota Unywele kikakomaa hutakiweza bora uwahi mapema ni Simple tu haichukui hata sekunde10 ... Atakuwa anatumia chai na marufuku vyakula vya mafuta kwa Ndani ya siku 5 -6 hivi ....
 
Mkuu natumaini makala hii itakusaidia

MAJIBU YA SWALI KUHUSU UKATAJI KIMEO kwa watoto
Haya ni majibu kwa swali alilouliza mdau kupitia blogu za Issa Michuzi na Ahmad Michuzi kuhusu 'ukataji kimeo kwa watoto' na yafuatayo ni maelezo toka kwa Dk. Mkopi aliyepo katika kitengo cha Magonjwa ya Watoto katika hospitali ya Muhimbili.
1494448.jpg


Kimeo (uvula) ni nini?
Kimeo ni sehemu ndogo ya kinywa inayoning’inia mkabala na mwisho wa ulimi. Hivyo kila mtu huzaliwa na kimeo na kimeo sio ugonjwa.

Kazi ya kimeo ni ipi?
  • Husaidia kinga ya mwili
  • Husaidia kulainisha koo
  • Husaidia kutoa sauti.
Je kwanini watu hukata kimeo?
Kutokana na elimu potovu juu ya kimeo; mfano: Kimeo kimevimba na kikipasuka tu mtoto ndo anakufa, Kimeo kina usaha, Kimeo ni kirefu sana. n.k.

Watu wengine hufikiri kuwa kimeo kinasababisha magonjwa kama vile:- Kukohoa muda mrefu, au Kukonda au Kutapika mara kwa mara au Mtoto kulialia bila sababu. Hii si kweli.

Je ni sahihi kukata kimeo?
HAPANA! Kimeo hakipaswikukatwa kutokana na sababu yeyote ile!

Nini madhara ya ukataji wa kimeo?
Mtoto anaweza kupoteza damu nyingi na kupoteza maisha Maambukizi ya magonjwa mbalimbali kutokana na kutumia vyombo ambavyo si salama kukatia kimeo; mfano:- Pepopunda, Homa ya mapafu, Maambukizi ya VVU, Mototo kupata maumivu makali au Kupaliwa na chakula kupitia puani.

Tufanyeje/Jitihada gani zifanyike ili kuzuia madhara haya yasitokee?
Watoto wanao kohoa muda mrefu, wasiokua vizuri, wanaotapika mara kwa mara, n.k. wapelekwe kwa daktari kwa ajili ya uchunguzi na tiba mbadala!
 

Attachments

  • 1494448.jpg
    1494448.jpg
    4 KB · Views: 217
Back
Top Bottom