Msaada mtoto anakohoa sana

Msaada mtoto anakohoa sana

Sema Sasa

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2012
Posts
651
Reaction score
898
Mtoto wa mwaka Mmoja na nusu anakohoa leo ni siku ya nane na ni kikohozi kikavu. Alipewa antibiotic fulani ya kifua siku ya kwanza iligoma, basi akachomwa sindano nne za cristapen kwa ajili ya pneumonia lakini hakuna mabadiliko, akaongezewa antibiotics nyingine amplicox na mucolyn lakini bado,

Leo Kapimwa kifua Dr. kasema hana shida yeyote ila kabadilishiwa dawa Kapewa Co trimoxazole bado hakuna badiliko licha ya kuanza kutumia.
Sasa sijui shida ni nini.
 
Kilianzaje ghafla au polepole?
Kinabana au ni kukohoa tu?
Anapata homa?
Kapoteza uzito?

Kuna contact na mtu yeyote mwenye Tb?
 
Tafuta asali ya nyuki wadogo,tafuta na karafuu ya unga,changanya ktk chupa ya ndogo tupu ya mukolyn au yenye ukubwa kama huo.Asali ijae ktk hiyo chupa,chukua kijiko kimoja kidogo cha chai kijae karafuu,hakikisha umechanganya vizuri,mpe kijiko kikubwa cha chakula kutwa mara 2, kwa uwezo wa Mungu atapona
 
Mpeleke hospital specialist wa watoto ,wengi naona wanamuongelea doctor Kimaro sijui kwa Dar..maana mtoto anavyotesa utajikuta unanunua kila dawa unayockia nzuri utajikuta humponyeshi..
 
Kilianzaje ghafla au polepole?
Kinabana au ni kukohoa tu?
Anapata homa?
Kapoteza uzito?

Kuna contact na mtu yeyote mwenye Tb?
Kilianza tu gafla, sasa kutoka ndio shughuli.
 
Tafuta asali ya nyuki wadogo,tafuta na karafuu ya unga,changanya ktk chupa ya ndogo tupu ya mukolyn au yenye ukubwa kama huo.Asali ijae ktk hiyo chupa,chukua kijiko kimoja kidogo cha chai kijae karafuu,hakikisha umechanganya vizuri,mpe kijiko kikubwa cha chakula kutwa mara 2, kwa uwezo wa Mungu atapona
Okay, Asante
 
hyo inaweza kua kilimi hata kijana wangu hali hyo ilimtokea na mwsho wa siku ikawa kilimi. ..jaribu kucheki hyoo
 
Karibuni kwa ushauri na maoni. Kesho ntawajibu na kuwashukiru. Shukrani
 
Back
Top Bottom