Msaada: Mtoto ananyonya sana

momara

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2019
Posts
463
Reaction score
491
Habari,

Ndugu zangu nina mtoto wa kiume wa miezi 3 ananyonya sana mpaka mama yake anachoka na hashibi, ukimtoa analia.

Na clinic wameshaur mtoto anyonye tu maziwa ya mama hadi afikishe miezi 6.

Nini naweza kufanya kumsaidia mtoto na mamake?
 
Ushauri ni mama ale sana,.ale vyakula vya kumpa nguvu na kuongeza maziwa na kufanya maziwa kua mazito ili mtoto ashibe.

Atumie mbegu za maboga,yanasaidia kutoa maziwa lakini pia mkiosha mchele yale maji yake aoshe achemshe aeke chumvi kidogo awe anakunywa kama chai inasaidia kufanya maziwa kua mazito.

Lakini zaidi ya yote kuna maziwa ya kopo nayo ni mazuri pia,anaweza akawa anachanganya,itasaidia mtoto asiwe na njaa.
 
Asante. Vp kuhusu maziwa ya kopo nielekeze kidogo
 
Mwanangu ana week mbili ananyonya hatari. Ila mama anakula supu mda wote na vyakula vya vingi anapata maziw ya kutosha
 
Kama maziwa ya mama hayatoshi na pia anakula vizuri, basi mnaweza kutumia maziwa mbadala mf. Lacogen 1 Ya (0-miezi 6) ili afya na kinga ya mtoto isidhoofu kwa kukosa chakula cha kutosha, hali hii inawatokeaga pia waliozaa mapacha au baadhi ya wanawake kushindwa kutoa maziwa ya kutosha kwa mtoto baada ya kujifungua, jamii zetu hazina elimu ya kutosha kuhusu mambo ya uzazi, sometimes hata baadhi ya hospitali hazitoi elimu kwa ukubwa zaidi na hupelekea kuwepo kwa zana nyingi potofu mitaani
 
Asante
 
Habar

Ndugu zangu nina mtoto wa kiume wa miezi 3 ananyonya sana mpaka mama yake anachoka na hashibi, ukimtoa analia.

Na clinic wameshaur mtoto anyonye tu maziwa ya mama hadi afikishe miezi 6

Nini naweza kufanya kumsaidia mtoto na mamake?
Kiongozi
Inaelekea mama hana maziwa ya kutosha. Jitahidi mama ale vitu vya kumuongezea maziwa.
Kama bajeti haiko vizuri kununua hayo maziwa ya formula, Mwanzishie maziwa ya ngombe (una weka nusu maziwa na nusu maji) mf: unachanganya kikombe kimoja maziwa na kikombe kimoja maji ili yawe mepesi kabisa. Na ikiwezekana upate mtu mwenye ngombe kabisa ili akupe maziwa ya ngombe mmoja (asibadilishe badilishe ngombe) wafugaji wanajua ukimwambia maziwa ya mtoto
Akinywa hayo maziwa yaliyo changanywa na maji akiteremshia na ya mama atakuwa poa kabisa.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…