Msaada: Mtoto ananyonya sana

Bila Shaka huyo mtoto ni wa kiume, huwa wananyonya hao....halafu Baba Kama una wivu vile kila saa kidume kinaning'inia kwenye nyonyo ya nkeo🤣🤣🤣
Yaani nimeona huyu hahitaji ushauri bali makanyo.

Kwa nini wana zaa kabla ya kupevuka?

Yaani hajui ulaji wa mtoto wa kiume na sisi wanaume kiujumla?

Au kwakuwa yeye anaishia kula chips basi anadhani ndo ulaji wa mwanaume?

Bahati yake siyo kijana wangu,ningempiga makofi mbele ya mke wake.
Dah!

Yaani huyo naye utakuta wanashauriana eti wajitenge mbali na wazazi. Wana matatizo mengi sana,sijui kwakuwa vijiwe vyao ni sinema zetu.
 
Siyo mtoto tu,hata anapokuwa na ujauzito wa mtoto wa kiume,kuamka usiku wa ma8 na kusaka chakula ni kawaida. Wakati mwingine hata ujauzito wa mtoto wa kike kuna baadhi nao ulazimika kuamka na kutafuta chakula usiku wa ma8 hasa kuanzia ujauzito wa miezi 7.
 
Mama ale ashibe, kumbuka usimpe mtoto chakula chochote hata maji mpaka atakapofunga miezi sita.
 
Asante
 
Bila Shaka huyo mtoto ni wa kiume, huwa wananyonya hao....halafu Baba Kama una wivu vile kila saa kidume kinaning'inia kwenye nyonyo ya nkeo[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Wewe
 
Asante
 
Asante sana kwa maelezo mazur
 
Safi
 
Maziwa ya ng'ombe hapana mkuu. Bado mdogo sana. Atafute ua kopo na ahakikishe siyo feki. Na pia ya kopo anatakiwa ajuwe kuna ya umri tofauti tofauti. All in all, watoto wa kiume wananyonya sana hivyo mama ale vizuri sana kama wengi walivyoshauri.
Binafsi napenda kubishana kwa hoja pamoja na kwamba najua kabisa huyo mtoto ni mdogo sana na ndio hivyo tena sio kila mtu anaweza kumudu kununua maziwa ya formula
Unaweza kutuandikia tofauti ya component za maziwa ya Binadamu na ya ng"ombe


Kwa upande wa nafaka forcus kwa nafaka ambazo hazijakobolewa (whole grain) na sio lazima uzipate vyote kwa wakati mmoja. (mbaazi & Ufuta ni viungo muhimu pia
Nafikiri akumbuke pia kuwa, akisha changanya maharage ajue yanachelewa kuiva hivyo kama ni uji upikwe muda mrefu
 
Mama ajitahidi kula sana chakula, uji wa lishe aweke na pilipili manga ya kutosha kwenye uji na chai pia. Mboga za majani, maji ya kunywa ya kutosha na supu za moto. Anaweza tumia unga wa mbegu za maboga kwenye vyakula vyake hasa uji na mbogamboga. Pia maziwa fresh ya ng'ombe yanaongeza maziwa( anywe mama)

Kuna faida sana kunyonyesha miezi 6 bila kumpa chochote, magonjwa na hospitali hamtapasikia kabisa. Mama asiwe mvivu wa kula hata usiku aamke kula. Jinsi anavyonyonyesha sana ndio maziwa yanajitengeneza kwa wingi.

Nina kichanga wa wiki na nusu wa kike ananyonya balaa usiku as long as yupo macho ananyonya tuu, so nakula sana bila uvivu, usiku uji hata saa 7 na saa 9 usiku naamka kunywa chai ya pilipilimanga ndio kila baada kunyonyesha nakunywa. Usimpe mtoto uji au maziwa ya ng'ombe.
 

Mkuu Zemanda ,

Mfano mama mwenye maziwa mepesi, ili apate maziwa mazito na ya kutosha taja ratio ya kila nafaka achanganye kusaga unga wa uji. Let say kilo 5.

-Kaveli-
 
atakuja kuwa na akili lakin fisadi huyo! mfundishe kuwa na kiasi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…