Msaada: Mtoto hataki kutumia potty

Msaada: Mtoto hataki kutumia potty

Njaa

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2009
Posts
1,022
Reaction score
412
Hello wanajamvi

Naomba ushauri kwenye hili: Nipo kwenye malezi ya mtoto wa miezi 14, kwa bahati mbaya huyu mtoto amekuwa akitumia diapers (pampers) tangu kuzaliwa kwake hadi hivi sasa.

Kwa muda wote huo amekuwa akijisaidia kwenye hizo diapers. Muda ulipofika wa kumfundisha kutumia pot au kukaa miguuni hataki kabisa, tena hata ile haja ya kutaka kujiasaidia huwa inakatika. Ukimuacha na nguo za kawaida, akijinyea analia na anaogopa sana mavi yake.

Je ni kweli its too late? Tufanyeje aweze kuzoea potty na kutoogopa mavi yake mwenyewe? Maoni please

Nawakilisha
 
Hii ya kuogopa haja yake nakumbuka niliona pia kwa mdogo wangu

Hahaahhaha alikuwa akijisaidia kama hakuna tissue atalia hadi apate wa kumsafisha,utoto bhana!!....yani alikuwa anaona sio haki kushika haja yake mwenyewe,lakini mwingine ndio ana haki ya kushika!😂😂

Sijui walikuja kumsaidia kwa namna gani lakini nafikiri ni suala la utoto,kadri atakavyozidi kukua atabadilika
Endeleeni kumuweka kwenye potty,atazoea labda
 
Ivo pampasi mtoto avae usiku tuu wakati wa kulala au kama mnasafiri vinginevyo mtoto aanze kuzoea mapema choo chake. Mtoto afundishwe mapema muache uzungu wa mapampasi.
 
ni mazoea tu mbadilishieni pampers avae wakat wa kulala tu na safari

mama ahakiishe mtoto akiamka tu asubh unapanga either kwenye miguu au kwenye pot akshiba tu apangwe asiwe mvivu itasaidia kidogo

wangu yuko na six months lakini akishikwa na haja anahangaika mpaka nimpange akijisaidia tu anakua sawa na nilianza hivo tangu yuko na three months
 
kutoogopa mavi yake mwenyewe?

Wewe huogopi mavi??!!, sembuse mtoto asiogope??.

Wewe badala ya kumpongeza huyo mwanao kwa kuogopa uchafu unalaumu!!!.

Halafu hapendi pot kwasababu hizo pots ni kwa ajili ya Watoto wa kizungu au wewe ni mzungu??.

Chimba shimo dogo hapo nyumbani na uwe unamtenga na akizoea atakuwa anajitenga mwenyewe.

Pots are for "bana ba bazungu" 🤣
 
Hello wanajamvi

Naomba ushauri kwenye hili: Nipo kwenye malezi ya mtoto wa miezi 14, kwa bahati mbaya huyu mtoto amekuwa akitumia diapers (pampers) tangu kuzaliwa kwake hadi hivi sasa.

Kwa muda wote huo amekuwa akijisaidia kwenye hizo diapers. Muda ulipofika wa kumfundisha kutumia pot au kukaa miguuni hataki kabisa, tena hata ile haja ya kutaka kujiasaidia huwa inakatika. Ukimuacha na nguo za kawaida, akijinyea analia na anaogopa sana mavi yake.

Je ni kweli its too late? Tufanyeje aweze kuzoea potty na kutoogopa mavi yake mwenyewe? Maoni please

Nawakilisha
Mkemee na kuwa mkali sana.

Watoto wanajua, usimwoneshe kumchekea kwenye mambo yasiyofaa...polepole atakuelewa.

Kingine, miezi 14, mpunguzie matumizi ya Dippers, zinaaminika zina madhara kwa watoto wa kiume na wa kike hasa linapojaa mikojo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ni mazoea tu mbadilishieni pampers avae wakat wa kulala tu na safari

mama ahakiishe mtoto akiamka tu asubh unapanga either kwenye miguu au kwenye pot akshiba tu apangwe asiwe mvivu itasaidia kidogo

wangu yuko na six months lakini akishikwa na haja anahangaika mpaka nimpange akijisaidia tu anakua sawa na nilianza hivo tangu yuko na three months
matoto mengine yanatunzwaaaa du moaka raha
 
Angalia mtoto wako huwa anapata haja mida gani.

Ikifika mida mida hiyo mkalishe kwenye potty ikiwekekana umwekee cartoon au uimbe nae nyimbo za nursery.

Akiweza kutoa Haja kwenye potty mpe zawadi. Makofi yanatosha.
 
Back
Top Bottom