Mtoto ameumia kwa ajali ya gari kwa kujigonga ubavuni gari imepaki. Bahati mbaya amekufa. Wazazi wanasema hatutaki kesi ni kosa la mtoto. Polisi wamekomaa wanataka wapeleke mahakamani. Je sheria inasemaje wadau
Sema ukweli pia umegharamia mazishi kwa kutoa jeneza, sanda, chakula msibani na pengine ulishiriki matibabu. Hiyo ni takrima.
Kisheria wazazi hawana ubavu wa kuzuia kesi isiende mahakamani, maana hata ushahidi wao siyo mhimu sometimes.
Busara ya Polisi kupeleka mahakamani ni ili jambo liishe kisheria, sio kindugu, maana baadhi ya wanandugu, baadae hugeuka, na kutuhumu polisi kula rushwa hadi kushindwa kupeleka kesi mahakamani.
Tena wanandugu wengine huanzia malalamiko yao kwa waziri, Ijp, rpc, na ni wakati wamepata elimu kuwa kama kesi ingeenda mahakamani, wangelipwa pesa nzuri na bima.
Hivyo usiwaamini sana wananchi, wanageuka na wanasahau kila kitu.
Niliwahi kuona mfano wa hili, dereva wa coca aligonga mtembea kwa miguu akafa. Kupitia ofisi, wakatoa milioni moja na gunia kadhaa za mchele kuhudumia msiba. Na ndugu wakasema hawana sababu ya kwenda mahakamani. Baada ya miaka sita, baadhi ya ndugu wakafundishwa kuwa, kama ingeenda mahakamani, wangelipwa fidia na bima maana magari yana bima.
Sasa wakajipanga namna gani ya kufufua kesi? Wakaona njia rahisi ni kuwalalamikia polisi kula rushwa wakashindwa kupeleka kesi mahakamani.
Na kesi ilisikilizwa, ya miaka sita iliyopita. Unaona usumbufu wake?