Msaada: Mtoto kufunga choo

Kawaida sana, ningeshangaa kama angekuwa anapupu kila siku kumbuka maziwa ya mama yana taka kidogo sana kiasi kwamba kujikusanya mpaka kuipata choo ya kutoka inahitaji muda

Asante kwa ushauri
 

Ukute hata kula hali ila unataka apate choo!!..
 
Mbona unahangaika mkuu unaweza pata dawa ikamsaidia lkn tatizo litarejea palepale mpaka avuke miezi mitatu ndio hupata choo marakwamara

Kwa sasa hivi nifanyaje??? Naona kama anahangaika
 
Hajapata Choo muda gani? Sijui ni kawaida am not sure lakini, mwanangu alikua anakaa 4 hadi 6 days bila kupupu na sikuwahi kumpa chochote na hiyo hali ikaisha yenyewe tu pole

Aaaah! kwenye mambo hayo mm nilikuwa sikufikirii kabisa mkuu, kumbe umo!!!!
 
Hakikisha na wewe mama unapunguza kula nyama huku ukiongeza kula mboga mbonga kwa wingi,zinasaidia pia akinyonya kulainisha choo chake.
 
Evelyn Salt ameongea jambo la maana na lizingatie, watoto wa umri huokufunga choo kwa siku 3-5 mara nyingi ni kawaida (kaa hakuna tatizo lingine). Ikizidi hapo waone madaktari. Kuna wengine hua wanawapa mafuta ya samaki!

Naona watoto huwa wanapitia hiyo hali..... Kwa wale wenye imani zao wanasemaga eti mtoto asipo pupu ni anakua anapata mwili (ananenepa) teh sijui ina uhusiano gani
 
Last edited by a moderator:
Mnyonyeshe kila saa ashibe vyema na mchuwe tumbo kwa mafuta ya nazi yaliyopashwa moto. Sishauri mtoto wa umri huo kupewa chochote tofauti na ziwa la mama na kama imebidi mpe mafuta ya samaki yale ya ladha ya machungwa na jitahidi asb mapema 12 mnyweshe na saa 4usk. Ikigoma kama unaweza pata samli ya kutikisa maziwa ya mgando uwe unamlambisha. Kinginee mvue nappy mpkake sabuni mkunduni sabuni ya kufua akae nayo dk kama 10 atakunya hivyo akimaliza mnawishe kuiondoa mabak yote ya sabumi na kinyec
 
Pole mama mzazi. Huyo mtoto isijekuwa ushamuanzishia vyakula vingine. Mpk sasa anatakiwa awe anashibia kwenye ziwa la mama tu na si vinginevyo. Km anapewa vyakula vingine inakuwa vigumu kuchambuliwa. Tumbo lake lina iwezo wa kuchambua (kumeng'enya) maziwa tu halijawa tayari kwa vitu vingine. 1. Mtoto akimaliza kunyonya hakikisha baada ya muda anacheua. Hata ikipita saa nzima hakikisha anacheua. Mlaze kifudifudi msuguesugue mgongoni yatatibu mpk acheue. 2. Kama analialia ina maana amemeza hewa nyingi wakati wa kunyonya na imejaa tumboni inamsumbua ambsyo huweza kusababisha hali hiyo. Fanya yafuatayo: 1. Jaza maji ua uvuguvugu kwenye beseni la kimuogeshea. 2. Muweke kwenyemaji kwa dk 10-15 ukiwa unamchezesha taratibu. 3. Mkono 1 mshikilie wakati mkono mwingine unapapasa tumbo lake tatatibu kwa mwendo wa duara kwenda mbele na nyuma (clock n anticlockwise). Mtoe na mfute vizuri. Endapo hatapata choo fanya hivi tena. Mlaze chsli chuku mafuta yoyote ya maji yapashe moto kidogo. Chovya vidole vyako 4 kwenye mafuta yenye uvuguvugu na usugu taratibu tumbo lake kwa mwendo ule2 wa duara kwenda mbele na nyuma. Hata ksma tumbo lilikuwa linamuuma litaacha. Pole. Waweza tuma PM au nipigie 0784305504.
 
Binafsi nilitumia maji tu..ongeza idadi ya maji anayokunywa.ataanza kupata choo ondoa hofu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…