Msaada: Mtoto kufunga choo

Msaada: Mtoto kufunga choo

Asante...


Mnyonyeshe kila saa ashibe vyema na mchuwe tumbo kwa mafuta ya nazi yaliyopashwa moto. Sishauri mtoto wa umri huo kupewa chochote tofauti na ziwa la mama na kama imebidi mpe mafuta ya samaki yale ya ladha ya machungwa na jitahidi asb mapema 12 mnyweshe na saa 4usk. Ikigoma kama unaweza pata samli ya kutikisa maziwa ya mgando uwe unamlambisha. Kinginee mvue nappy mpkake sabuni mkunduni sabuni ya kufua akae nayo dk kama 10 atakunya hivyo akimaliza mnawishe kuiondoa mabak yote ya sabumi na kinyec
 
Asante.
Nitazingatia ushauri wako


Pole mama mzazi. Huyo mtoto isijekuwa ushamuanzishia vyakula vingine. Mpk sasa anatakiwa awe anashibia kwenye ziwa la mama tu na si vinginevyo. Km anapewa vyakula vingine inakuwa vigumu kuchambuliwa. Tumbo lake lina iwezo wa kuchambua (kumeng'enya) maziwa tu halijawa tayari kwa vitu vingine. 1. Mtoto akimaliza kunyonya hakikisha baada ya muda anacheua. Hata ikipita saa nzima hakikisha anacheua. Mlaze kifudifudi msuguesugue mgongoni yatatibu mpk acheue. 2. Kama analialia ina maana amemeza hewa nyingi wakati wa kunyonya na imejaa tumboni inamsumbua ambsyo huweza kusababisha hali hiyo. Fanya yafuatayo: 1. Jaza maji ua uvuguvugu kwenye beseni la kimuogeshea. 2. Muweke kwenyemaji kwa dk 10-15 ukiwa unamchezesha taratibu. 3. Mkono 1 mshikilie wakati mkono mwingine unapapasa tumbo lake tatatibu kwa mwendo wa duara kwenda mbele na nyuma (clock n anticlockwise). Mtoe na mfute vizuri. Endapo hatapata choo fanya hivi tena. Mlaze chsli chuku mafuta yoyote ya maji yapashe moto kidogo. Chovya vidole vyako 4 kwenye mafuta yenye uvuguvugu na usugu taratibu tumbo lake kwa mwendo ule2 wa duara kwenda mbele na nyuma. Hata ksma tumbo lilikuwa linamuuma litaacha. Pole. Waweza tuma PM au nipigie 0784305504.
 
Naona watoto huwa wanapitia hiyo hali..... Kwa wale wenye imani zao wanasemaga eti mtoto asipo pupu ni anakua anapata mwili (ananenepa) teh sijui ina uhusiano gani

Dah! hii nayo mpya, mie nilivyo chikondee ntaulizia vizuri huenda nilikua napupuu kutwa mara 3 au 4.
 
Dah! hii nayo mpya, mie nilivyo chikondee ntaulizia vizuri huenda nilikua napupuu kutwa mara 3 au 4.

Ha ha ha si dhani kama kuna uhusiano wowote hapo ni watu tu na imani yao, kuna mdau kaeleza kuwa sababu ni maziwa ya mama, accumulation yake hadi yatengeneze taka mwili inahitajika muda....hii inaingia akilini
 
Back
Top Bottom