Habarini wakuu.Poleni kwa majukumu.
Huyu mtoto alianza kuchemka(joto kupanda sana) jumamosi usiku wa septemba 7. Jumapili tulimpeleka zahanati akapimwa malaria, hamna. Dokta akasema itakuwa ni mafua tu labda ndio inayopandisha joto.
Tulipatiwa amoxylin, cetrizen na paracetamol.
Ila joto halijashuka kabisa tangu aanze kutumia dawa.Hapa shida inaweza kuwa nini wakuu?
NB:Mtoto hana maumivu ya kichwa.
Hajapoteza hamu ya kula, haisi kichefuchefu na hatapiki. Anacheza vizuri ila shida ni hili joto kupanda sana na halitaki kushuka.