Msaada; Mtoto wa miezi miwili analia sana!!

Anahitaji jina LA babu/bibi yake mzaa baba.
 
Watu kwa ushirikina bana, hatari!! Kila comment ushirikina tuu!! What happened to common sense?

Back to mtoa mada, mtoto hulia mda wote meaning hata kulala saa moja mfululizo hawezi? Analia hata akiwa ananyonya?
 
Solution yake huwa inakuaje hapo? Tho mtoto anafanana na mama yake

Basi kama ni hivyo Mkuu Mtoto kafanana na Mama yake huenda tatizo sasa likawa katika Jina ambalo umempa. Siyo kila jina ni la kumpa tu Mtoto wako. Jitahidi sasa uwatafute Wazee tena hasa akina Mama au Bibi watajua jinsi gani ya kukusaidia haraka kwani Kwao hakuna kinachoshindikana na wanayajua mengi ya Kiuzazi kuliko hata sisi Wanaume. Kila la kheri na pole sana kwa Mtoto wako kukumbwa na hilo tatizo Mkuu.
 
Watu kwa ushirikina bana, hatari!! Kila comment ushirikina tuu!! What happened to common sense?

Back to mtoa mada, mtoto hulia mda wote meaning hata kulala saa moja mfululizo hawezi? Analia hata akiwa ananyonya?
Hapana kulala analala ila akiamka ananza.. Na kunyonya ananyonya vzur.Sema kwenye in between hapo kunyonya na kulala kuna kilio kirefu.. Then mara nyingi utasikia kama kitu tumboni kinalia ndo ananza lia
 
Na hakuna kitu kinakosesha raha kama mtoto kulia masaa yote.. Na kunakipindi hataki umuweke chini anataka umbebe tu.. Ukimlaza chini kilio.. Yani kanatupa wakati mgumu sana
Fuatilieni kwa makini, kilio ndio lugha pekee ya mtoto. Huenda tumbo linamsumbua, au sikio, colic n.k. Muombeni sana Mwenyezi MUNGU awalindie mtoto wenu maana watoto wachanga wana mitihani katika ulezi.
 
Msaidie kumuweka begani, mimi ilibidi niwe namsaidia mke wangu maana alikuwa anamuweka hadi anachoka mtoto hajabeua. Saidianeni, ni kipindi kigumu, mke anachoka sana.
 
Hapana kulala analala ila akiamka ananza.. Na kunyonya ananyonya vzur.Sema kwenye in between hapo kunyonya na kulala kuna kilio kirefu.. Then mara nyingi utasikia kama kitu tumboni kinalia ndo ananza lia
Kwa comment hii, Jibu lipo wazi, mtoto huyo tumbo linamsumbua, kutana na daktari wa watoto. Pia kuna dawa za kienyeji kwaajili ya shida za tumbo kwa watoto wachanga. Kuwa makini pia na dawa za kienyeji, usigeuze mwanao kuwa wa majaribio
 
Eidha jina mlilompa halitaki.Mbadilisheni...but kwa umri huo ni Sawa kulia.Hata Wangu walikuwa hivyo hivyo.Siku zinavyoenda ataacha.pia usishangae kuona ananyonya Lkn hapati Choo.ni kawaida.Usije anzisha thread
 
Hakuna kitu kibaya kama mzazi kutokuwa na uhakika na imani yako.

Unapofikia level ya kuzaa mtoto kuna mambo lazima uyaweke sawa. Mfano, unatakiwa uwe karibu sana na Mungu kwa kuomba na kumuombea mwanao mkiwa wewe na mama yake bila kutegemea mtu mwingine.

Kwa njia hiyo itakusaidia kuondoa au kuprevent outside attack za shetani au watu wenye nia mbaya na mwanao.

Kwa jinsi ulivosema, naamini huyo mtoto amepatikana kwa maandalizi yote ya kupata mtoto hivyo hata jina ulilompatia uliliombea na ulimuombea toka yuko tumboni. Kama hukufanya hivyo, hilo ni kosa kubwa sana. Hii ni sawa na kugoogle majina, badala uombe kwanza ushauri kwa Mungu.

In short Zingatia kukaa vizuri na Mungu wewe kwanza kabla hujatafta msaada wa nje. Watoto wanakuwa na mambo mengi sana ambayo ni predictable. So Unapokuwa na familia ujanjaujanja ni hatari sana. Watoto wakati mwingine wanachezewa na kutishwa na wachawi halafu wewe umekaa kuuliza nimpeleke kwa mchungaji gani. Act wewe mwenyewe kwanza kwa uhakika.
 
Kaka nataka kutoa maelezo ya tiba kutokana na style anayoumwa mtoto huyu anayezungumziwa ndo maana nataka kumuelekeza huyu dawa maana sio wote wa style hii
Kwa hiyo Avatar yako, ni hakika utamuelekeza kwenda kupiga ramli. Na ndio maana unamwita chobingo. πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Kuna viongoz wa dini wenye vipawa mbalimbali siyo mbaya mtu mwenye uhitaji kupata huduma.
 
Jamani mtoto anamiezi miwili lakini analia sana.. Si mchana si usiku.. Tumejaribu remedy mbalimbali ikiwemo kumtoa gesi tumboni kwa kumlazia tumbo lakini bado hali tete.. Sababu inaweza kuwa nn?
Pole sana ila navyojua mm akifikisha miezi mitatu hilo tatizo la kulia litaisha. Watoto wengi wachanga wako hvyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…