Juisi ya machungwa peke yake kwa mtoto mdogo hivyo inaweza kumletea shida,Jaribu juisi ya matunda yasiyo na acid,mfano juisi ya ndizi mbivu au ya parachichi unaweka na vichungwa kidogo sana na mpe mtoto mara moja tu kwa siku muda ulex2,
Pia kumbuka juisi usimpe mtoto nyingi,ni vijiko vikubwa vitatu mpaka vinne vinamtosha,na maji pia ni kijiko kikubwa kimoja au viwili basi,
hakikisha anashiba vizuri kama walivyoshauri hapo juu,kingine muangalieni labda mnamfunika manguo mengi kupita kiasi anasikia joto au mnamsahau na pempas/nepi muda mrefu inamkera,mnamuweka pozi moja la kumbembeleza anachoka,pia mmemfungia ndani kwenye chumba ambacho hakuna hewa safi inayoingia kirahisi
mama mtu ale ashibe sawax2 mtoto apate maziwa mazito, na kama ni mtoto wa kiume inawezekana hashibi vizuri,mfanyie mpango wa maziwa ya kopo au uji wa dona mwepesi sana,unaochujwa unakuwa kama maziwa (akina bibi wanajua jinsi ya kupika huu uji wa watoto wachanga),Me wife nilikuwa naweka sura ya kazi hasa likija swala la yeye kugonga msosi alipojifungua,wanawake wa siku hizi wanautaka umisi wakati wa malezi ya mtoto mchanga,usikubali hilo kaka,mtoto ataharibika.