Msaada; Mtoto wa miezi miwili analia sana!!

Msaada; Mtoto wa miezi miwili analia sana!!

Summary ya michango:
1. Inawezekana mtoto hashibi so wengine wameshauri nimwanzishie uji/maji/juisi(nasubr aproval ya juisi kama inafaa au lah)
2. Wengine wapo kiimani zaidi so wamenambia nifanye maombi chumba anacholala mtoto(hili litafanyika soon) plus kubadili jina la mtoto
3. Kumuona specialist wa watoto(hili tutafanya)
4. Wengine wameshauri kuwa makini kwenye unyonyeshaji as inawezekana mtoto akawa anavuta gesi nyingi. Hili ntalifanyia kazi kwa uangalizi maalumu
Inaendelea...
 
Huu sasa ni ubinafsi. JF ingekuwa hivi, isingepata wafuasi.
Weka maelezo hapa ili usaidie na wengine.
Kaka nataka kutoa maelezo ya tiba kutokana na style anayoumwa mtoto huyu anayezungumziwa ndo maana nataka kumuelekeza huyu dawa maana sio wote wa style hii
 
Mkuu haiwezekani kushare hapa ili nawengine wafaidike..
Nisawa ila nataka kujua zaidi kuhusu mtoto huyu ili nimuonyeshe dawa mbalimbali ndo maana nikamwambia ajaribu kama anamtekenya au anamminya tumbo akiona anajikunjakunja(kujinyonga) aniambie nakama vipi awekee sikio kwenye tumbo wakati ule ndo anaanza kulia asikilize kua atasikia sauti ya tumbo kunguruma? Akinipa mrejesho namuelezea dawa sasa akipona ataleta mrejesho humu mkuu
 
Jaman mtoto wa miezi miwili juice?? Mi nadhan n mda wa maziwa tu au wajuz mnasemaje
Mtoto wa miezi miwili haruhusiwi kula wala kunywa kitu chochote tofauti na maziwa na dawa pale itakapo mlazimu hivyo kama itagundulika anaumwa na dawa ni juice hana budi kunyweshwa mkuu
 
kama mmebadili majina ila bado tu,,,ebu mkumbuke baba ake wa ukweli ....(BIOLOGICAL FATHER)
 
Nisawa ila nataka kujua zaidi kuhusu mtoto huyu ili nimuonyeshe dawa mbalimbali ndo maana nikamwambia ajaribu kama anamtekenya au anamminya tumbo akiona anajikunjakunja(kujinyonga) aniambie nakama vipi awekee sikio kwenye tumbo wakati ule ndo anaanza kulia asikilize kua atasikia sauti ya tumbo kunguruma? Akinipa mrejesho namuelezea dawa sasa akipona ataleta mrejesho humu mkuu
Ukimminya anatakiwa kufanya nn kama asipojikunja? Ili tuchukulie kama reference point
 
Jamani mtoto anamiezi miwili lakini analia sana.. Si mchana si usiku.. Tumejaribu remedy mbalimbali ikiwemo kumtoa gesi tumboni kwa kumlazia tumbo lakini bado hali tete.. Sababu inaweza kuwa nn?
Mtoto wangu wa kwanza alikuwa kama wa kwako, tatizo tuliambiwa na Dr bingwa wa watoto ni gesi .Kuwa makini unapomnyonyeaha tumbo lake liwe intact na la kwako...yaani alale kiubavu.Baada ya kunyonya mlaze begani kwako hadi acheue...endelea hivyo hivyo ili kutoa gesi tumboni.

Hii husababishwa na ulaji wa ndizi kwa wingi pindi mama akiwa mjamzito(Google).

Baada ya miezi 3 itakwisha kabisa. Poleni sana, umenikumbusha mbali.
 
Niwape pole aisee..ndio changamoto za malezi hizo.. Au pengine anaumwa hamjui
 
Mimi nina utaalamu kidogo na hawa watoto wadogo chini ya miaka 5

Jaribu kumshika tumbo akiwa amelala na kumshika pembeni(mbavuni) ukiona anajinyonga hilo ndo tatizo lake naugonjwa huo hospital hawana dawa ila kuna majani ambayo ni dawa ila sidhani kua huko hapo ila jaribu kuni PM unipe no za whatsap nikutumie picha za dawa na tuwasiliane tuweze kumsaidia mtoto maana hata kama wamemloga itasaidia
Vipi ushauri wa kuombewa!!
 
Jamani mtoto anamiezi miwili lakini analia sana.. Si mchana si usiku.. Tumejaribu remedy mbalimbali ikiwemo kumtoa gesi tumboni kwa kumlazia tumbo lakini bado hali tete.. Sababu inaweza kuwa nn?

Unauhakika ulipojifungua huko ' Leba ' huyo uliyenae ndiyo alikuwa Mwanao halali? Yawezekana analia lia hivyo kwakuwa pengine Wewe siyo Mama yake au labda Manesi walikuchezea mchezo au walikosea wakati wanakukabidhi. Hili nalo huwa ni tatizo sana Mkuu. Pole sana lakini!
 
Solution yake huwa inakuaje hapo? Tho mtoto anafanana na mama yake
 
Back
Top Bottom