Msaada; Mtoto wa miezi miwili analia sana!!

Mkuu kuhusu bb mama anasaidiwa na bb upande wangu(mwanaume).. Nmeuliza labda kuna haja ya kumleta na bb upande wa mama.. Na kuhusu mchungaji nmemuomba jamaa atuambie kanisa alilompeleka mwanaye akaombewa ili na mm nmepeleke mwanangu aombewe.. As tupo disperate
Aje hapo hapo mnapoishi Nyumba au majirani wanaweza kuwa siyo wazuri kwako.. Mtoto ni Malaika anaona vitu vingi sana hapo hapo Nyumbani kwenu mnapoishi au anapoishi ndipo Maombi yanapotakiwa kufanyika Jaribu Mkuu..
 
Pole. ndio watoto walivyo. Hiyo ndio njia yao ya kujielezea iwapo hajuona kuwa hawako vizuri. Mara nyingi hulia kwa sababu ya njaa,Ugonjwa,joto, njaa au aina fulani ya maumivu.
Utapewa ushauri kibao, mar hivi mara vile.
Ila mwishowe kabisa nakushauri mpeleke kwa Daktari.

Kuna wakati nilisoma ushauri kibao humu, kwenda kwa daktari hakuna hata moja ya humu yaliyosaidia. Daktari akampa amoxylin syrup, akapopata nafuu.

So, mpeleke kwa Dr kwa ushauri bora zaid.
Mtoto wako alikua na umri gani?
 
Tutafanyia kazi mkuu ushauri wako
Mtoto kulia ni ishara ya kutoshiba. Aidha kama ni mtoto wa kwanza lazima mama afunzwe jinsi ya kunyonyesha bila kuingiza gesi. Utakuta tumbo limejaa lakini 60 percent ni gesi! Unashauriwa usichoke kumweka begani ili abeue sana na si mara moja. Je choo anapata? Kumbuka huu ni wakati wake wa kujenga mwili usisahau kumpatia maji na juisi ya machungwa! Wangu katika umri huo alikuwa hajisaidii hata siku 12 nilipofanya hayo tatizo liliisha
 
Aje hapo hapo mnapoishi Nyumba au majirani wanaweza kuwa siyo wazuri kwako.. Mtoto ni Malaika anaona vitu vingi sana hapo hapo Nyumbani kwenu mnapoishi au anapoishi ndipo Maombi yanapotakiwa kufanyika Jaribu Mkuu..
Sawa mkuu nitafanyia kazi ushauri wako next week tutafanya ibada nyumbani
 
Mtoto kulia ni ishara ya kutoshiba. Aidha kama ni mtoto wa kwanza lazima mama afunzwe jinsi ya kunyonyesha bila kuingiza gesi. Utakuta tumbo limejaa lakini 60 percent ni gesi! Unashauriwa usichoke kumweka begani ili abeue sana na si mara moja. Je choo anapata? Kumbuka huu ni wakati wake wa kujenga mwili usisahau kumpatia maji na juisi ya machungwa! Wangu katika umri huo alikuwa hajisaidii hata siku 12 nilipofanya hayo tatizo liliisha
Yani mkuu unayoyaongea utafikiri unaelezea ya mtoto wangu.. Kuna kipindi mtoto alifunga choo siku saba.. Ndi akajisaidia week ilopita.. But now naona siku mbili zimepita hajajisaidia.. Kuhusu juisi ya machungwa tutalifanyia kazi leo.. Na kuhsu kumweka begani nafikiri ntamueleza mama yake awe anafanya zaidi ya mara moja.. Mana nahisi huwa anamfanyia maramoja tu akishamnyonyesha..
 
Ndiyo, inaonekana mmemuiba huyo mtoto😛. Mzazi hawezi kuanzisha thread kisa mtoto analia.
Hapana.Inawezekana hiyo ndiyo tafsiri yako sitakulaumu kwa hilo..
Tatizo la mtoto kulia limekuwa kubwa ndiyo maana tunajaribu kuseek msaada kwa wanaofahamu kwa kuwa humu jf kuna watu wa kada mbalimbali. Thats why kuna watu humu wametoa michango mizuri tu ambayo tutaifanyia kazi.. Ata ww kama unajambo unalifahamu usisite kutuambia kwani haitanisaidia peke yangu na wengine pia wenye tatzo kama langu
 
Morogoro..
Mwz kuna mama anaitwa mama Yusufu mmasai anasaidia hata wa kwangu alipitia shida kama hiyo. Nilipelekwa kwake na wauguzi wa Hospital ya mkoa (Sekou toure) alimpa dawa na akasema hapana pia tena na hakulia tena na Mtoto alilala siku mbili mfululizo
 
Sasa kwa ss wa morogoro tunasaidiwaje?
 
Mtoto kulia ni ishara ya kutoshiba. Aidha kama ni mtoto wa kwanza lazima mama afunzwe jinsi ya kunyonyesha bila kuingiza gesi. Utakuta tumbo limejaa lakini 60 percent ni gesi! Unashauriwa usichoke kumweka begani ili abeue sana na si mara moja. Je choo anapata? Kumbuka huu ni wakati wake wa kujenga mwili usisahau kumpatia maji na juisi ya machungwa! Wangu katika umri huo alikuwa hajisaidii hata siku 12 nilipofanya hayo tatizo liliisha
Hili ndo jawabu la matatizo yote, mwambie shemeji ajaribu kucontrol gas isiingie dogo atakuwa anajaa gas tu wala siyo kushiba. First born wangu alisumbua kiaina mwanzoni baadae mchezo tukaujua aah ikawa mtelemko. Juice ya machungwa au machenza eee bwana inakuwa swaafi kabisa. Pia shemeji ajaribu kupunguza kula mayai, pilipili au kwa kifupi vyakula vinavyoweza kumsababishia mtoto gas tumboni. Nawewe kaka mkubwa jitahidi kufuata maelekezo ya kampelewele hapo juu!! Bila kusahau kuna madaktari bingwa wa watoto, weka appointment uende ukapate ushauri zaidi ya kitaalamu. Usihofu litaisha hilo!! Kutokuwa na hofu pamoja na kuwa na imani ndiyo uanaume wenyewe mkuu.
 
Jamani mtoto anamiezi miwili lakini analia sana.. Si mchana si usiku.. Tumejaribu remedy mbalimbali ikiwemo kumtoa gesi tumboni kwa kumlazia tumbo lakini bado hali tete.. Sababu inaweza kuwa nn?
Mimi nina utaalamu kidogo na hawa watoto wadogo chini ya miaka 5

Jaribu kumshika tumbo akiwa amelala na kumshika pembeni(mbavuni) ukiona anajinyonga hilo ndo tatizo lake naugonjwa huo hospital hawana dawa ila kuna majani ambayo ni dawa ila sidhani kua huko hapo ila jaribu kuni PM unipe no za whatsap nikutumie picha za dawa na tuwasiliane tuweze kumsaidia mtoto maana hata kama wamemloga itasaidia
 
Hili ndo jawabu la matatizo yote, mwambie shemeji ajaribu kucontrol gas isiingie dogo atakuwa anajaa gas tu wala siyo kushiba. First born wangu alisumbua kiaina mwanzoni baadae mchezo tukaujua aah ikawa mtelemko. Juice ya machungwa au machenza eee bwana inakuwa swaafi kabisa. Pia shemeji ajaribu kupunguza kula mayai, pilipili au kwa kifupi vyakula vinavyoweza kumsababishia mtoto gas tumboni. Nawewe kaka mkubwa jitahidi kufuata maelekezo ya kampelewele hapo juu!! Bila kusahau kuna madaktari bingwa wa watoto, weka appointment uende ukapate ushauri zaidi ya kitaalamu. Usihofu litaisha hilo!! Kutokuwa na hofu pamoja na kuwa na imani ndiyo uanaume wenyewe mkuu.
Shukrani mkuu
 
Back
Top Bottom