Msaada, mtoto wangu hatembei

akilala haweze kukaa mwenyewe hadi akalishwe mkuu, anachoweza yeye ni kushuka kwenye kiti tu, suala la kuchepuka kwangu mimi hapana, labda mwenzangu (mama yake) sababu siwezi jua na siwezi kumsemea
 
Ni kweli wng miezi kumi yeye kutembea kwake hd apate sehem ya kushika na ikitokea yuko peke anasimama na kutembea akitokea mtu ghafla anakaa
 
akilala haweze kukaa mwenyewe hadi akalishwe mkuu, anachoweza yeye ni kushuka kwenye kiti tu, suala la kuchepuka kwangu mimi hapana, labda mwenzangu (mama yake) sababu siwezi jua na siwezi kumsemea

Dah! Kumbe we ni me!! Nilidhani ni ke. Wanaume hatukimbilii kuona wanetu wakitembea. Utamkuta barabarani tu siku moja. Mtoto mlemavu anaonesha dalili zifuatazo kama si zote lakini mara nyingi: Hawezi kuamka kitandani, hawezi geuza shingo wala kuikaza, hawezi kukaa mwenyewe hata ukimtengenezea ngata, na macho kupepesa hawezi.
Huyu wako anashuka mwenyewe kwenye kiti. Usimsumbue mtoto, atatembea tu. Je, Umewahi kuchunguza kwenye family yenu?? Huenda huwa mnachelewa sana kutembea.
 
Ni kweli wng miezi kumi yeye kutembea kwake hd apate sehem ya kushika na ikitokea yuko peke anasimama na kutembea akitokea mtu ghafla anakaa

Mwimbe ule wimbo wa kikwetu. Kasimama peke yakeeeee na kumshangilia utashangaa ataanza kukufuata.
 
Hilo la kuchunguza kwenye familia yetu kama tunawahi au kuchelewa, naweza kusema kwa kifupi wengi wanawahi ndio maana imekuwa gumzo kwenye familia baada ya huyu wangu kuchelewa.
 
Hilo la kuchunguza kwenye familia yetu kama tunawahi au kuchelewa, naweza kusema kwa kifupi wengi wanawahi ndio maana imekuwa gumzo kwenye familia baada ya huyu wangu kuchelewa.

Basi usiendelee kuchunguza kwani tiyari kuna viashiria kuwa unataka kusema; Nina shaka na huyu mtoto si wangu. Hapana, ni mtoto wako tu. Tuliza mzuka atatembea tu. Acha shaka juu ya mkeo ndugu. Hilo gumzo kwenye familia limeanzia wapi?? Mbona wasikusaidie kumshukuru Mola kuwa, mmepata mtoto mapema? Angalieni wanaume, tunachokifanya hakimpi Mola utukufu.
Nitamuamini mke wangu siku zote wala simdhanii mabaya kamwe.
 
Huwa inatokea, kuna watoto huwa hawatambai inatokea siku anasimama na kutembea,
Huu uzi umenikumbusha ushauri uliotolewa huko fb, "ushauri jaman, mtoto wangu hatembei" jibu likatoka hana pa kwenda.
[emoji23] [emoji23] [emoji2] hana pa kwenda
 
Ndio wapi huko Mkuu?

Inakupasa uanze kumuona daktari bingwa wa watoto, atakuhudumia Kwa kufanya vipimo, Kisha ataweza kumpatia multi vitamins na dawa nyingine Kama ataona ni vyema, mkisha tumia Dawa baada ya muda wataangalia maendeleo , Kama bado huyo daktari wa watoto bingwa ndiye atashauri umpeleke Kwa mama cheza Muhimbili !
Pia anzeni kumsihi Mungu awafanyie wepesi sawasawa na Imani yenu wakati mkiendelea na kwenda hospital!
Mungu ni mwema atatembea tu tena hadi mtashangaa!
Ila mchukue hatua ya maombi na dua wakati huo huo kwenda Mihimbili kuona daktari bingwa wa watoto!
 
ahsante kwa ushauri mkuu
 
Mimi mwanangu hakutambaa hata kidogo alikuwa anaburuza matako chini mwisho wa siku akasimama na kutembea moja kwa moja ila alikuwa bonge sana
 
Kama anaweza kushuka kwenye kitanda au kochi .. usihofu atatembea mara moja na kukimbia kabisa
 
Huja mmbemenda kweli wewe...????
 
Mkuu kila mtoto ana stage zake za kukua... Wa kwangu alianza kutembea na mwaka 1 na miezi 8 baada ya kumkomalia kumfanyisha mazoezi... Nilichogundua mtoto alikua anabebwa sana pindi nikiwa sipo, nikapiga marufuku mtoto kubebwa pasipo ulazima na nikawa namfundisha mwenyewe pia alikua hapendi kula nikawa nahakikisha kila jioni lazima nimlishe... Week 2 tu dogo akaanza mabadiliko...
Wengine hutembea na 2 years...
 
Angalau umenipa moyo, ngoja nimkazanie kumlisha maana hapendi kula zaidi ya kunyonya
 
Angalau umenipa moyo, ngoja nimkazanie kumlisha maana hapendi kula zaidi ya kunyonya

Ndo maana pia nilikwambia ukienda kumuona daktari wa watoto atampatia multi vitamins ambazo zitaimarisha vitu vingi mwilini mwa mtoto!
Sasa huko kunyonya Kwa mtoto wa umri huo hakutoshi na mama anatakiwa asiwe mvivu wa kula na kunywa supu na uji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…