Msaada muda wa kubadili oil kwenye gari.

Inategemeana na aina ya Oil ila msikilize Fundi...
Mwezi uliopita ninefanya service sehemu ambayo sijazoea aisee ni maumivu wahuni Wamenifungia Filter vibaya kumbe inaleak taratibu bila kushtuka ningechoma engine.
 
Hii ya kuvuja ni magari yote mkuu au huwa inatokea??? Oil imevuja mpaka imeishaa na haijawahi nitokea toka nianze kufanya service fala sana yule fundi.
 
Ni kweli Mkuu,nimefungua bonet ya hii gari nimekuta maandishi yana recommend kuwa oil ibadilishwe kila baada ya kilomita 15,000...nafikiri nitabadili soon ila ukwel oil iliyopo bado ni mpya kabisa.View attachment 3205234
Labda ubadili isizidi km 10,000.

Nina mashine ya Kijerumani kila nikibadilisha oil na oil filter niki reset inaonyesha kuja kubadili oil ni km 15,000 ila mimi uwa nabadili oil ikifika km 7,000.
 
Hii ya kuvuja ni magari yote mkuu au huwa inatokea??? Oil imevuja mpaka imeishaa na haijawahi nitokea toka nianze kufanya service fala sana yule fundi.
Mfano sump ikitoboka au kupasuka na oil kumwagika
 
hiyo Oil ya Synthetic uliyoweka ni nzuri inaenda kms 5000, wengine hutembea hata zaidi kidogo hasa kama umeweka Filter nzuri.
Ukiweka Oil hakikisha unanunua Filter nzuri, sipendelei zile wanauza mafundi.
Njongeza: Engine Oil inatakiwa kubadilishwa ndani ya miezi 12 hata kama kama gari imetembea kilometa chache.
 
Unanunua wp Castrol OG kaka?
Gerezani kariakoo mtaa wa kiungani/Livingstone , Duka linaitwa SAI ENTERPRISES hawa ni wahindi ambao dealer authorized wa Castrol...pia Kuna wahindi wengine ambao ni wakala wa Castrol wapo mtaa msimbazi/mvita hawa wanauza pia na oil filter BOSCH original
 
Kama unatumia Fully Synthetic Oil badilisha kila ikifika km 5,000.

Mimi kwasasa natumia PUMA Fully Synthetic Oil baada ya kuachana na CASTROL Edge Fully Synthetic Oil
Mkuu umeshatumia hii Castrol oil edge ya kisasa?
Maana bei yake imechangamka na mzuri Sana kama unataka kutumia Kwa safari ndefu.
Bei yake ni Tsh 165,000/= Kwa jumla na maduka mengine wanauza 180,000
 
Mkuu umeshatumia hii Castrol oil edge ya kisasa?
Maana bei yake imechangamka na mzuri Sana kama unataka kutumia Kwa safari ndefu.
Bei yake ni Tsh 165,000/= Kwa jumla na maduka mengine wanauza 180,000 View attachment 3211024
Sidhani kama hii ni Synthetic Oil!

Bei za Oil za Castrol na PUMA ni sawa sababu zote zilizopo Bongo zinatengenezwa South Africa.

Nilikuwa natumia Castrol Edge Synthetic Oil 5W30 kwa gari ya Kijapan na 5W40 kwa Mashine ya Mjerumani nikaachana nazo baada ya kampuni ya PUMA kuacha kuuza hizi Oil nikahamia kwenye PUMA Synthentic Oil mpaka sasa.

Kuwa makini sana na hizi Castrol Oil za sasa kuna ambazo zimechakachuliwa
 
Hii ni fully synthetic mkuu kabla ya kununua nilianza Kwanza kufanya utafiti pamoja na mafundi, hizo Castrol oil za kuchakachua nazijua vizuri Sana na bei zake ni 65,000/= mitaa ya shaurimoyo na msimbazi...
Ishu za oil nazijua Sana hasa Kwa Castrol oil na total.
Hybrid car wanatumia Sana oil hii ya CASTROL
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…