Msaada: Mume wangu hajitumi. Anaweza kulala siku nzima nyumbani na akaona ni sawa tu

watusakama watu wa mwambao 😀
Si kila kazi ni miguvu physical tu yakhee, kazi zingine ni akili tu atiii
 
Rafiki ataonaje maushauri ya wadau?
Kwanza amuombee kwa Mungu aliyemuumba, atajua kiumbe wake ana shida gani. Pia mwambie mama yake aongee na kijana wake..
Ukiona kijana kaoa lakini anapenda kushinda kwao na wazazi hawamshauri kuconcetrate na mkewe kama yaagizavyo maandishi matakatifu, elewa mama ndiye kisababishi.

Ananufaika na mizunguko ya kale kagari kwa kupenda usafiri wa bwelele.

Huyo hawezi kuwa mshauri mzuri wa ndoa ya mtoto wake.
 
Kuichapa anaichapa? kama Kuna changamoto njoo inbox plse utayapata yote unayohitaji
 
Hilo gari ni lake? Au la boss?
Mafuta anaweka nani?

Au wataka sema hiyo 150k yako monthly, ndo inatumika kufanyia service za gari pia?

Mnaishi nyumba ya kupanga? Au mmejenga?
Kama ni ya kupanga, twambie nani analipa kodi.

Umesema mumeo ni dereva Bolt.
OK! Tujiulize, "mtu analo gari, na lipo road kila siku afu bado unamuona ni 'hajitumi'?" 🤔
Okay basi kama hajitumi, umtume wewe sasa.

Au sisi ndo hatujaelewa? Au ulimaanisha hajitumii kimapenzi?

Au labda pengine ni vile haupendi kuona mumeo akiwa muda mwingi yupo na mama'ake mzazi? Unapata wivuuuu eh 😎
 
Nicheki PM tumpe kazi
 
Sasa hukujua Hilo kipindi Cha uchumba wenu? Hukuchunguza shughuli zake hasa ni nini? Au hamkukaa uchumba? Unakubali vipi kuolewa na mtu ambaye humjui vzuri!! Damn
 
Bila shaka huyo ni sele
 
Mnawakataa WASUKUMA mnawakubalia masharobaro halafu baadae mnakuja kulia.
 
Jambo la muhimu kuliko yote ni kuongea nae juu ya mambo wewe mwenyewe,yaani mkiwa 2 tu,iwapo hamna matokeo ita wazazi wake muongee,ikiwa hamna matokeo,ita wazazi wako,wazazi wake kwa pamoja muongee,iwapo hamna matokeo ita viongozi wa dini mlikofunga ndoa muongee.Kwa vyovyote vile ni lazima utapata ufumbuzi
 
Huyo mmeo atakuwa ndo hawa wanaokesha mitandaoni wanatutukana ..nakushauri nenda ukareport Polisi aje akamatwe akalale ndani hata mwaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…