Msaada: Mume wangu hajitumi. Anaweza kulala siku nzima nyumbani na akaona ni sawa tu

Msaada: Mume wangu hajitumi. Anaweza kulala siku nzima nyumbani na akaona ni sawa tu

Me 50 na ke 43
mmmh kuna mambo yanahuzunisha kwakweli, at the age of 50 bado mtu hajitambui?!!

Jitahidi tu kupambana dada uendeleze familia, no way! Kama umeshahangaika mpaka kwa washenga huyo hakuna namna utamfanya abadilike ni mpaka aamue yeye.
 
Aya ya mwisho inaonesha kuwa huyu rafi yako ni wewe. You can edit that.
Kuhusu ushauri; sisi wanaume tunajituma sana hapo kuna tatizo hujagundua. Jaribu kuchunguza vizuri na kwa kuongea naye. Kuna vitu vinamkata hamu ya kujituma.
Anachagua masaa ya kufanya kazi na hela hana? Makazi menyewe kasaidiwa. Kweli?! Na ni mume?!!
Does he even think of his future let alone his family?!
 
Hamna mume hapo. Tafuta mwanahme mwingine maisha yaendelee. Hapo hamna maisha wala future
 
Anachagua masaa ya kufanya kazi na hela hana? Makazi menyewe kasaidiwa. Kweli?! Na ni mume?!!
Does he even think of his future let alone his family?!
Mkuu ukifika miaka 50 unawaza future ya kazi gani tena?? Ni kumalizia tu maisha yaliyobaki urudi kwa muumba
 
Chanzo hapo mama yake siku zote wakina mama tatizo kwa watoto wao wakiume
 
Gari ni yake alipewa na mdogo wake ili aendeshee maisha. Anatoka nyumbani saa tatu asbh anaenda kwao (gari analaza kwao) kidude anakiwasha mchana anadai ndo hakuna foleni, ikifika saa kumi na moja jioni anakizima anasema jioni ni foleni barabarani hasara. Akipata mteja anakopa liten la kuweka mafuta akimaliza ruti analipa (mara nyingi anamuomba mama yake hapo kwao kisha akirudi anamrudishia) Tunakaa kwny nyumba ya mdogo wake (mdogo wake anaishi UK). Nyumbani anarudi saa moja au mbili usiku

Mimi nipo kwny stoo ya mmama anauza mkaa ndio nauza hapa napata 150k kwa mwezi

Nadhani nimejibu maswali yako, nilikuwa mbali na mwenye simu
Kama hujui kuendesha gari, jifunze udereva upate leseni na kukisajili bolt halafu wewe uanze kuendesha hiyo Bolt. Utaacha hiyo kazi ya mkaa na kuendesha bolt full time mchana, usiku unampa mbususu ajipigie. Hela itapatikana
 
Mbona umesema hataki kazi na tena ni dereva wa Bolt? Anaendesha saa ngapi?

Hilo gari analotumia kama Bolt ni nani mmiliki?
 
Mkuu ukifika miaka 50 unawaza future ya kazi gani tena?? Ni kumalizia tu maisha yaliyobaki urudi kwa muumba
Hilo nalo neno!
Ila kwanini alioa? Angebaki nyumbani amalizie maisha.

BTW, mtoa maada hajatuambia kuhusu watoto. Yawezekana jamaa watoto wake ni wakubwa na wanajitegemea au wanajiweza kaona ndo muda wake wa kupumzika na kula bata. No stress 😀
 
Habari za leo wana jamvi, tafadhali msaidie rafiki hapa, kama bandiko lake linavyoeleza...

Nimeolewa miaka mitatu iliopita na mume wangu ni dereva wa bolt. Tatizo kubwa alilo nalo ni hajitumi, yani anaweza kulala siku nzima nyumbani na akaona ni sawa tu.

Anapenda sana kwenda kwao, kila siku lazima aende kwao, atashinda huko jioni ndo arudi tunapoishi. Hz tabia mimi zinanikwaza na kuniumiza sana maana maendeleo tutayasikia kwa jirani. Hamna future yoyote katika maisha yetu. Na huko kwao sio kama anakazi anafanya nope, ni aidha ashinde tu jioni anaende kucheza draft kijiweni au amuendeshe mama ake kwny safari zake za kila siku.

Nimeongea nae, nimeshirikisha wasimamizi wa ndoa mpaka nimekata tamaa maana hakuna mabadiliko. Yani haoni kama anapaswa kubadilika, kipato changu mimi hakitoshei majukumu ya nyumbani (nalipwa laki na nusu tu kwa mwezi)

Hebu nishaurini nifanye nini wana jamvi kabla sonona haijanimaliza
Bila shaka huyo kwanza atakuwa Toto la mwisho.

Huyo achana naye. Tena achana naye haraka sana, watu hawabadilikagi atabadilika kidogo kisha atarudi tena hukohuko baada ya mda kidogo.
 
Back
Top Bottom