Msaada: Mume wangu hajitumi. Anaweza kulala siku nzima nyumbani na akaona ni sawa tu

Hebu kuwa serious kidogo Zuriel_cfc .
Una miaka 40+ na mumeo 50+.
Ww unalipwa 150k kwa mwez.
Mko Dar.

Yeye ni mvivu na hajishughulishi zaid. Anafanya Bolt.
Je! huwa anafanya saa ngap?.
Kwa wiki anafanya mara ngap?.
Gari ni ya kwake?.
Mna nyumba au mmepanga?.
Mna familia?.
Je Yeye anatokea familia bora, kwamba wanamsaidia hela mara kwa mara?.

Ni muhimu kujua tatizo ni kubwa kias gan kabla ya kukushauri maana naona kuna vitu hujaviweka sawia.
 
Mpaka unakuwa JF maana yake wewe una akili, ilikuwaje ukaolewa na Mwanaume kama huyu?
 
Umeolewa na Mama's Boy.

Ni tatizo hilo jinasue mapema ,muache bila kumuachia maumivu maana hao madereva wa boda/baja huwa na matatizo ya afya ya akili asije kukupa BETO.
 
Kama hajitumi, mtume wewe!
 
Kuna swal.nimekuiliza hijajibu na kuna mdau pia kakuuliza swal.hilohlo hijajibu?

Isije ikawa.kampen.ya kudhalilisha wanaume humu jukwaan
Gari ni yake alipewa na mdogo wake ili aendeshee maisha. Anatoka nyumbani saa tatu asbh anaenda kwao (gari analaza kwao) kidude anakiwasha mchana anadai ndo hakuna foleni, ikifika saa kumi na moja jioni anakizima anasema jioni ni foleni barabarani hasara. Akipata mteja anakopa liten la kuweka mafuta akimaliza ruti analipa (mara nyingi anamuomba mama yake hapo kwao kisha akirudi anamrudishia) Tunakaa kwny nyumba ya mdogo wake (mdogo wake anaishi UK). Nyumbani anarudi saa moja au mbili usiku

Mimi nipo kwny stoo ya mmama anauza mkaa ndio nauza hapa napata 150k kwa mwezi

Nadhani nimejibu maswali yako, nilikuwa mbali na mwenye simu
 
Aya ya mwisho inaonesha kuwa huyu rafi yako ni wewe. You can edit that.
Kuhusu ushauri; sisi wanaume tunajituma sana hapo kuna tatizo hujagundua. Jaribu kuchunguza vizuri na kwa kuongea naye. Kuna vitu vinamkata hamu ya kujituma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…