Msaada: Mwanangu amepinda mguu

Msaada: Mwanangu amepinda mguu

mapozi baby

Member
Joined
Jun 26, 2015
Posts
50
Reaction score
13
Mwanangu mguu wake mmoja kama umepinda kidogo nimejaribu kumpeleka CCBRT lakini kila siku wananipiga kalenda mara njoo baada ya miezi mi3 mara miezi 6, Hata sielewi nifanyeje na mwanangu.

Naogopa atapata kilema cha maisha, Sasahivi anamiaka miwili na nusu.

Kama kuna mwenye ushauri anisaidie please.
 
Pole.ila peleka hii kitu jf doctor ndo utapata msaada zaidi
 
Mtafute dk bakki pale kibaha hospital ya mifupa hutajuta

Yesu akutangulie
 
Vp alikuwa ananyonya kidole cha mguu?
 
Kuna hospital moja iko dodoma ngoja nifanye mawasiliano kesho nitakuambia jina lake
 
mwanangu mguu wk mmoja km umepinda kdg nimejaribu kumpeleka ccbrt bt kila ck wananipiga kalenda mara njoo baada ya miezi mi3 mara miezi 6,ht cielewi nifanyeje na mwanangu naogopa atapata kilema cha maisha,sahv anamiaka miwili na nusu.km kuna mwenye ushauri ansaidie plz.

pole sana,mpeleke mwenge kwa bishop kakobe,alishaombea mwenye mguu mfupi ukanyooka ukawa kama wa pili.hakuna la kumshinda mungu.
 
heri wa kwkwo wangu hana nguvu kwa kiuno na analingana nawako na hasimami wala hatembei sasa nashinda kwa maombi tu
 
Poleni sana wenye watoto wenye ulemavu,najua vile inakuwa kwa maana nilijaaliwa mtoto Wa ivo na kwa Neema za Mungu amenyooka.alikuwa na clubfoot au talipes sasa yuko vema.
Mpeleke kwa huyo daktari Wa mifupa.
Wangu alikuwa akipata matibabu ya kunyooshwa kwa wiki hadi alipofanyiwa upasuaji na kupewa viatu maalumu.
 
ulimtibia hsptl lpi mkuu?
 
Wangu hana mvungu kwenye mguu wa kushoto. Nimempeleka ccbrt but nataka nimpeleke kwingine. Naomba details za madaktari engine.

Wa kwako alikuwa na tatizo gani na ulimpeleka wapi?
 
ulimtibia hsptl lpi mkuu?

Kulikuwa na daktari akiitwa john rugambwa wilayani bunda mkoani Mara ndie aliekuwa akimtibu kwa miaka mitatu mfululizo,nilipoteza mawasiliano ya huyo daktari,alikuwa daktari mkuu Wa wilaya ya bunda baadae. Lakini pia hospital ya Bugando na Ccbrt kuna hao madaktari.
Bugando Mwanza wanahudumia watoto walemavu chini ya daktari Isdori na Rachel.
Mkuu nicheki pm nikupe namba zao.
 
Wangu hana mvungu kwenye mguu wa kushoto. Nimempeleka ccbrt but nataka nimpeleke kwingine. Naomba details za madaktari engine.

Wa kwako alikuwa na tatizo gani na ulimpeleka wapi?

Me wakwangu pia hana mvungu kwny mguu wa kushoto,nimempeleka ccbrt wanazingua na me ningependa kujua nijaribu wap kwingne mwanangu apone km hl tatizo linatibika aisee.
 
Wangu hana mvungu kwenye mguu wa kushoto. Nimempeleka ccbrt but nataka nimpeleke kwingine. Naomba details za madaktari engine.

Wa kwako alikuwa na tatizo gani na ulimpeleka wapi?

Alizaliwa amepinda mguu Wa kushoto kuanzia kiunoni,nilianza matibabu ya kumnyoosha kcmc moshi,mount meru Arusha kote sikufanikiwa ndipo nikasikia kuna daktari bunda mkoa Wa Mara hospital ya mission,nikaenda akaanza matibabu kwa huyo dokta akiitwa john rugambwa, alikuwa akishirikiana na waitaliano,then huyo daktari akawa daktari Wa wilaya lkn aliendelea na huduma,nilikuwa nikienda clinic kila alhamisi kwa miaka mitatu almost,baadae akawa amenyooka mtoto nikawa mbali na huko lkn nampeleka Ccbrt monthly and quarterly clinic.
Kwasasa daktari nilipoteza mawasiliano Yake.
 
Me wakwangu pia hana mvungu kwny mguu wa kushoto,nimempeleka ccbrt wanazingua na me ningependa kujua nijaribu wap kwingne mwanangu apone km hl tatizo linatibika aisee.
Ile material inayotumika kwenye viatu hivyi vya ccbrt kiukweli sijapenda.

Its hard plastic, motto Wang alia za kutembea kama amewekewa vyuma, pia akawa hana furaha, hachezi.

Ma nivue, Ma nivue, mwishowe I gave up.
 
Back
Top Bottom