Msaada: Mwanaume ninayeishi naye haoneshi kunipenda na hataki tuachane

Watu wanachungulia babes zao wanaendeleaje as if wanaangalia maharage waliyoyabandika jikoni. Week nzima huwasiliani na mwenzio si unaweza kuta amekufa hadi ashazikwa
Wenzio wanamjulia hali kutwa Mara tatu km dose ya panadol
 
Huo upuuzi ulinishinda. Nitajidanganya tu kama huyo wa mleta mada. Lakini nitajisahau tu. Lakini madili ya hela na washkaji huwa sisahau kabisa
Na hata sio upuuzi labda km maisha bado yanakuchanganya, watu wako bize tena matajiri wenye pesa lakini hawasahau kuwajulia hali wenzi wao tena mara nyiiingi tu kwa siku
 
Eti mko kwenye mahusiano ila inapita wiki hamuwasiliani!! Hata kaka yangu tu sipitishi wiki sembuse mpenzi!!!

Yaani siku tu kupita hapana aisee, hayo mahusiano ya hivyo siyataki jamani.
Kwa kweli hayo maigizo me siwezi. Siku inapitaje kwa mfano?
 
Gerls wanapenda yule boy mkitembea kwa Barabara AMBEBE POCHI SI NI KWELI GERLS

wanapenda yule mwanaume ukipiga chafya asemee POLEHEE KWANI UMEUMIA

wanapenda yule mwanaume ameota ndoto mbaya amlalamikie na amwambie POLEHE JAMN

Sasa kibaya hakuna mwanaume wa namna hiyo kulelewa kinyanya
Akati na huku life imekaza babako mwenyewe hajakudekeza unataka udeke MTU MWENYE NDEVU NA UKOO UNAMTEGEMEA
PAMBANA TU NA HALI YAKO JAMN
 
Watu wanachungulia babes zao wanaendeleaje as if wanaangalia maharage waliyoyabandika jikoni. Week nzima huwasiliani na mwenzio si unaweza kuta amekufa hadi ashazikwa
Jitu la ivo kwanza bora uwe single ieleweke sasa unawasliana na mpenzi baada ya wiki amekuwa baba mkwe
 
Na hata sio upuuzi labda km maisha bado yanakuchanganya, watu wako bize tena matajiri wenye pesa lakini hawasahau kuwajulia hali wenzi wao tena mara nyiiingi tu kwa siku
Kiufupi siwezi na sitokuja kuweza kama vp na aniache tu akatafute atakayekuwa na huo muda wa kuandika txt.
 
Kiufupi siwezi na sitokuja kuweza kama vp na aniache tu akatafute atakayekuwa na huo muda wa kuandika txt.
Ukikua kiakili, kifedha, kimahusiano hasa unaingia kwene ndoa utajicheka sana na hayo mawazo yako sjui uko kidato bado??
 
Kuna wanawake wanapenda Attention aisee..Kuchat muda wotee...umuulize anakula nini.. Alafu sikukukuu hizi mwisho wa siku uambuliee kupigwa mazingaa
 
Sasa mwenzio atajuaje unaempenda jmn....hapa ninawiki naumwa nimelazwa jamaa hata kuja kuniona hamna... hata kutuma 100 ya matibabu hakuna yaan mpaka naona aibu wanaoniuguza wakiuliza mwenzio kaja inabidi niongee uongo kasafir kikazi
Achana nae, rudisha mpira kwa kipa we we timua zako. Cha msingi uwe na sababu za kuishi hapa malazi,Chakula na mavazi.
 
Ukikua kiakili, kifedha, kimahusiano hasa unaingia kwene ndoa utajicheka sana na hayo mawazo yako sjui uko kidato bado??
Nipo kidato cha ngapi? Nimesoma enzi hizo ukitumiwa barua na picha ya mpenzi nalala nayo kitandani wiki nzima. Nikienda prep naisoma hiyo tu wiki nzima. Barua tunaandika na kuchora kopa kwenye karatasi na kunyunyizia perfume. Sijui kama hata ulikuwa ushazaliwa?

Nishakuwa na wapenzi hadi nimecheka sasa hivi nawaangalia tu jinsi wanavyojidekeza.
 
Kumbe bado uko kwenye stage ya wapenzi
 
hakupendi.Achana nae.Oa mwingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…