Msaada: Mwanaume ninayeishi naye haoneshi kunipenda na hataki tuachane

Msaada: Mwanaume ninayeishi naye haoneshi kunipenda na hataki tuachane

Hiyo ni tabia yetu watu wa Kanda ya ziwa hasa sisi wakurya....! Sio kwamba hatupendi ila ndivyo tulivyoumbwa
 
Wewe kwa sasa kwa tulia jamaa anakupenda ndio maana mko kwenye mahusiano na wazazi wemeridhia,pia usisahau huyo jamaa ni wa mkoani hana mbwembwe kama wa sisi wa dar,,nadhani umenielewa,,I love u baby,sweet, na majina kibao ya kimahaba na malove bite shingoni ukiyata rudi dar,,,mkoani utakonda bure
 
Kwa umi wako huo,kama uko romantic sijaona tatizo la mwanaume.
 
Mama ndivyo tulivyo.
Kuna mwenzio mpaka ananiogopa maana muda wote nimenuna.na kuwa na hasira.na majibu ninayomjibu uwa anajuta.
na ninao wanne wote mwendo ndo huo huo.
Uwa simtafuti mtu wanaanza wenyewe.
Kwa hyo tuvumilie tu.ila akianza kukupiga hyo ni hatua nyingine
 
Anakupenda sema hayupo Romantic.. Wapo Guys type iyo..thread yako inaonesha untakana attention tu
 
Yaan jf bhan jamaa kutulia
Uko hajui Kama anajadiliwa na watu zaid yae100 juu ya matatizo yake [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Ukute na yeye yupo ila ajitambui pengine naye anachangia mada
 
Mh! Mara hakujali ukimwomba msaada, mara kipato chake kidogo kushinda chako, mara hakuiti bebi!!! Haya ni madhara ya kuolewa katika umri mdogo, ulitakiwa ule maisha kwanza uitwe bebi utumiketumike na watu kadhaa ujue kwamba mtu anaweza akakuita bebi na shida yake ikawa K tu, akili ikikaa kiutu uzima ndiyo unaolewa sasa.
 
I hope mko poa guys

Naitaji ushauri hapa serious kabisa

Mimi ni mwanamke nina miaka 30 nina mchumba ambaye wazazi walishatupa ruhusa ya kuishi pamoja

Mwaka 2016 nilipata kazi ya muda mfupi katika kampuni fulani nilifanya kazi ndani ya miezi minne nilikutana na kaka ana 33 kwa a

Huyu Kaka nilimpenda sana alikuwa mtu fulan mpole hana Mambo ya ajabu ukweli nilitokea tu kuvutiwa nae. Nikafanya juhudi tukawa marafiki wa karibu, kusaidiana mambo mbalimbali haikupita muda tukawa tumeanza mahusiano ya kimapenzi

Uzuri jamaa alikuwa hayupo katika mahusiano serious, alikua na mwanamke ambae walikua hawafahamiani aliunganishiwa na jamaa tu so wakawa na mapenzi ya kwenye simu

Baada ya miezi 6 jamaa akanipeleka kwao kunitambulisha ilikua Desemba mwaka jana, Februaru mwaka huu alihamishwa mkoa mwingine kikazi nami nikaacha pale nikaanza biashara zangu binafsi. March akaja nyumbani kwetu kujitambulisha, Juni kupanga na kutoa mahari.

Oktoba Wazazi pande zote mbili walikutana kupanga mambo ya ndoa, wazazi wake wakaomba tuchukuane tu kwa sasa hawana uwezo tutafunga ndoa mwaka kesho. Hii ni sawa kwa jamii ya wasukuma wa kijijin kwani huamini ukishamtolea mahari mwanamke tayari wanakuja kumchukua. Familia yangu ikakubali

Kilichonileta kwenu

Baada ya kukaa kiuchumba na jamaa nilikua nahisi hanipendi tangu kabla hajanipeleka kwao nikawa najiondoa kwake ajabu nikikaa nae nikimwambia tuachane hakubali kabisa anaweza hata jitupa chini akibembeleza nisimuache

Nikimuangalia ni mtu ambae haoneshi kama ananipenda anaweza kaa siku 1 au 2 bila kunipigia. Ninaweza pata shida kunisaidia akawa mzito mno. Ni mtu ambaye hajali unaumwa, umepata matatizo unaishi vipi haelewi

Mwanzo nilihisi labda anamahusiano mengine lakini nilifanya uchunguzi sikubaini hicho. Mi nampenda najikuta naumia nahitaji kupata attention yake, muda wake, nilishaongea nae sana. Ni mtu ambae hata kuniambia nakupenda au nimekumiss au kuniita tu mpenzi wangu ni ngumu labda muwe kitandani kapandwa na hisia anaweza fanya hivyo au muwe mna ugomvi anakubembeleza au ndio mmeelewana

Atafanya hivyo for 2 days then anarudi katika hali yake

Nilishaongea nae kama hanipendi nimeshamuomba aniache niumie badae nitazoea hataki. Kuna kipindi nilimwambia aniache tu atafute mwanamke anaempenda na nikamchunia kweli

Aliteseka sana alinitafutia washauri sio ndugu zake, rafiki zake na zangu. Nashindwa kuelewa nitaishije na huyu mtu jamani. Sielewi ni maumbile yake yuko hivi, makuzi au tu hanipendi!

Amekulia kijijini hasa tena hasa nashindwa kuelewa labda ndivyo alivyo. Nawaza labda yupo kwangu kimaisha tu sababu yeye ana kazi nzuri mshahara mkubwa lakini familia ya kwao inamuelemea ukoo mzima unamtegemea yeye

Mimi kipato changu kidogo kwake lakini nina maendeleo kidogo namzidi na ninafanya vitu vya msingi. Nahisi labda jamaa amefata maisha!

Wadau samahani kwa kuwachosha naombeni mawazo yenu
Huyo jamaa anakupenda ila hayo ni maumbile yake yupo hivo sio mtu wa kuongea jitahidi kua nae mtaishi kwa aamani
 
Back
Top Bottom