Msaada: Nahisi mwilini nina sumu

Msaada: Nahisi mwilini nina sumu

Master SM

Member
Joined
May 29, 2020
Posts
55
Reaction score
54
Habari zenu wanajamvi, naandika haya nikiwa nahofu kutokana na hali ninayohisi; nahisi mwili kupungua mwilini, nahisi baridi tofauti na awali bila mabadiliko ya hali ya hewa.

Nilishawahi kuleta Uzi humu jukwaani kuhusu maswaiba ya kazini na mauzauza kisa cheo, Sasa nahisi nimelishwa kitu kinachonitafuna mwilini.

Siku chache nilizungumza na ndugu zangu wakaribu na kunishauri niwe makini kwani hapo naweza fanywa kitu kibaya, sasa bahati mbaya nilikula chakula ambacho mpaka sasa nakihisi kulikua sio Cha kawaida, na mpaka Sasa nimejiwekea limit ya kutokula chakula Cha kazini.

Naweza kusamarize issue iliopo, ipo hivi; niliajiriwa na kampuni moja hivi kukaimu nafasi flani Ya uongozi, nimeingia kazini nimekuta wapo wakongwe kwenye kazi na hao ndio wanaoweka kinyongo kwani nafasi isiwe yakwao, na zilizala ikaanzia hapo.

Ushauri wenu wanajamvi ni muhimi sana
 
Aiseee!
Tukushauri kujua kama umekula chakula chenye sumu ama lah au tukushauri kama ubaki kazini ama utoke uwapishe wakongwe au tukushauri uende kwa Mganga akuzindike au tukushauri nini mwenzetu.
 
Aiseee!
Tukushauri kujua kama umekula chakula chenye sumu ama lah au tukushauri kama ubaki kazini ama utoke uwapishe wakongwe au tukushauri uende kwa Mganga akuzindike au tukushauri nini mwenzetu.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] angestick kwenye issue ya afya kwanza ....then hvo vingine akipata muda avifungulie uzi
 
Acha imani za kishirikina japo yapo ila kimini ndiyo unaipa nguvu upande wa giza, mwenye haki ataishi kwa imani bro
 
Nimeenda maabara nimejieleza naambiwa nipime minyoo, Sasa najiuliza minyoo na nilichoendea mbona tofauti?
 
Ondoa hofu iyo hofu ndio chanzo cha mwili kuhisi dhaifu na ndio chanzo cha kuleta uzi wako hapa Jf
 
Back
Top Bottom