Play station
Member
- May 8, 2014
- 19
- 44
Habarini ndugu zangu wa JF natumahi nyote ni wazima! Tafadhali naombeni ushauri juu ya hiki kisa changu.
Mimi ni mtumishi mpya wa serekali ,nafanya kazi taasisi A ambayo haiko kwenye mfumo wa cheki namba wala huduma za lawson. Nina miezi minne kazini! Kabla sijasaini offer nilikuwa na pending interview ajira portal kwenye taasisi B (yenye maslahi mazuri zaidi) taasisi B iko kwenye mfumo wa cheki namba na lawson.
Nikiwa sina hili wala lile naingia tovuti ya ajira nakutana na habari njema kuwa nimepita usaili taasisi B. Nawakumbusha tena huu usaili wa taasisi B niliufanya nikiwa bado sijasaini offer ya kazi taasisi A.
Nafika hadi utumishi na kuchukua barua yangu ya kazi na kuipeleka kwa mwajiri wangu mpya, nishajaza baadhi ya fomu! Kitu kinachonifanya niombe msaada kwenu leo hii ni hiki, je nawezaje kuhamia taasisi B pasipo kupata shida yoyote?
Nimejaribu kumshirikisha mkuu wangu wa taasisi A kuwa nimepata kazi nyingine ,amegoma kuniachia kwa njia zile za utaratibu, amekaza kuwa bado ana mahitaji na mimi .nipo njia panda kuna watu wengine wamenishauri niandike barua ya kujiuzulu , wengine wamesema niondoke tu bila kuaga ... Bado sijui nifanye nini!
Naombeni ushauri ndugu zangu kipi nifanye hapa??
NATANGULIZA SHUKRANI