Msaada: Nahitaji kuhama kutokea Taasisi A kwenda Taasisi B za Serikali, Nifanyeje?

Nimekuelewa vizuri sana
 
Tamaa sio nzuri mkuu, najua selection zimetoka za TRA kule ila njaa mbaya. Tulia uliko mambo yatajiseti mbeleni tu.
 
Zote hizo ni Serikali. Taasisi zinagawanyika kutokana na mgawanyo wa majukumu. Kiacha kazi ni hatarishi aisee. Sema mwajiri wako wa sasa angekuwa muungwana angekuacha uende kwenye Taasisi pana. Usiache kazi Serikali ni moja.
 
Kwanza hakuna taasisi ya serikali ambayo hakuna check no
Taasisi za serikali zisizo na check namba zipo. Pia hawalipiwi hazina wao wanazalisha na wanajilipa kutokana na uzalishaji wao. wala mambo ya lawson hayapo.
Kuna jamaa yangu yupo Taasisi moja ya serikalini nilipomuuliza kuhusu check namba alishangaa ni kitu gani tena lawson ndio kabisa hajawahi hata kuisikia.
 
Kwanza hakuna taasisi ya serikali ambayo hakuna check no
kuna Taasisi za Umma hazijaingia kwenye mfumo wa lawson,na wala hawana check Namba.Mimi nilikuwa mtumishi kwenye taasisi ya aina hiyo na sikuwa na check namba lakini nilipohamishiwa serikali kuu ndo taratibu za utumishi zikafanyika kama vile ni fresh employment ndio nikapatiwa check Namba.Hivyo kama yupo kwenye taasisi isiyotumia lawson ana option ya kwenda kuajiriwa kama mtumishi mpya au alternatively aende Utumishi watam-advise the way forward ambayo haitaleta shida kwake
 
Mimi ni mtumishi wa serikali nishakuwa na cheki namba lazima ufute taratibu za kuhama kwa boss wako ila ukiondoka kinyamela itakula kwako hautoweza kuajiriwa tena serikali so kuwa muwazi mkuu
 
Ondoka bila kuaga uhesabike mtoro watakufuta wenyewe, yaani umepata maslai mazuri bado unashangaa.
 
Mimi ni mtumishi wa serikali nishakuwa na cheki namba lazima ufute taratibu za kuhama kwa boss wako ila ukiondoka kinyamela itakula kwako hautoweza kuajiriwa tena serikali so kuwa muwazi mkuu
Shida ya utumishi ukipata shida ya kufukuzwa Kazi ni wepesi Sana yaani fasta tu unalamba barua na sio ishu za kuhama au jambo la kheri utasubiri sana.
 
Ndugu yangu kila mtu ametoa ushauri mkubwa mzuri Sana ila jibu kuu wanalo utumishi nenda utumishi usiende kokote zaidi ya utumishi kawaelezee concern yako, watakupa ushauri mzuri tu, then ufatilie, boss hanuniwi usigombane nae, mwisho wa siku watamuuliza boss wako utendaji kazi wako na nidhamu akikuchafua umeharibu mkuu, so nenda utumishi moja kwa moja bila iukata kona maana muda unazidi kweda mkuu siku zitaisha hujafanya chchte. Asante.
 
Huwezi kuhama hadi umalize kipindi cha matazamio. Baada ya kumaliza muda matazamio utapewa barua ya kuthibitisha Kazini hiyo ndio itakuwezesha kuhama
 
Umenikumbusha hili, lilitokea kwangu pia nakuelewa. Nikichofanya bila ushauri kwa yoyote na kwa sababu sikujua, niliandika 24 hrs notice ya resignation nikalipa na one month salary.
Tofauti kidogo, mie nilitoka kwenye check number kwenda pasipo na check number. Years later, tukatakiwa kuhamia kwenye hiyo Lawson ie hcmis. Huko wakauliza km niliwahi kuwa na check number nikakubali. Wakauliza km niliacha kazi kwa kufuata utaratibu nikawapa barua, yakaisha.
Ila nakusihi sana nenda utumishi wakusaidie. Ni upumbavu sana kumzuia mtumishi eti wanamuhitaji.
Wao watapewa mwingine.
 
habari, sasa kama haupo kwenye mfumo wowote na wala check number, swali, mshahara walikuwa wanakulipaje unachukua cash au?

inaonekana hiyo taasisi A siyo Taasisi ya Kiserikali, ingekuwa ya kiserikali lazima uwe na chech number. ushauri wangu andika barua ya kuacha kazi masaa 24 na unarudisha na mshahara wa mwezi mmoja.

ile jaribu kupata ushauri sehemu nyingine pia kabla hujafanya maamuzi ambayo yatakuletea shida baadaye.
Lakini naamini kama taasisi ya kiserikali lazima ungekuwa na check number
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…