Msaada namna ya kuhuisha (re-new) leseni ya udereva

Msaada namna ya kuhuisha (re-new) leseni ya udereva

Habari za humu, kuna rafiki yangu alipoteza leseni yake ya kuendeshea gari na anahisi amepotezea porini na kuipata itakua ngumu.
Je kuna gharama kwa ajili ya kupata leseni mpya? maana hiyo alirenew November 2017.
Na je ni gharama ni kiasi gani?
Asanteni
Nenda ofisi yoyote ya TRA na TIN namba yako uliyokatia leseni ukiwa na loss report ya polisi,utapewa form ujaze na utaenda bank kulipia sh 41500/=then wataiona kwenye systeam na utapewa leseni yako.
 
Nenda ofisi yoyote ya TRA na TIN namba yako uliyokatia leseni ukiwa na loss report ya polisi,utapewa form ujaze na utaenda bank kulipia sh 41500/=then wataiona kwenye systeam na utapewa leseni yako.
Mmh mimi nikafikiri labda haitazidi 15000 maana jamaa karenew November mwaka jana.
Kumbe ni kama ime expire unarenew. Ok nashukuru
 
Aanze kuripoti polisi, zen aende TRA atapewa fomu atajaza na kuipeleka polisi kitengo cha usalama brbrn atajaziwa madaraja yake. Zen utarudi TRA watakupa kakaratasi ka kulipia baada ya kulipia atasubiri kwa muda atakaoambiwa
 
Nenda pale Mayfair plaza mikocheni ukiwa na leseni yako ya zamani, utapewa karatasi ya kulipia benki kiasi cha shillingi 40,000/=, then waulize urudi tarehe ipi kuja kuchukua leseni yako mpya, very simple
Nashukuru kwa majibu. Niko mkoani hata Mayfair plaza Mikocheni sipajui. Dar napajua Ubungo, Mwenge, Kariakoo, Posta na Feri tu
 
Muda wa leseni yangu umeisha ila haujazidi mwaka na ninahitaji ku renew upya.

Mara ya kwanza nilipohitimu mafunzo ya idereva na kupewa cheti ndugu yangu flani alikuwa ana connections tra na matrafiki, alinisaidia kupata leseni fasta ila kwa sasa hayupo karibu.

ningependa kujua ni vitu vipi natakiwa niandae ili kwenda kupata leseni mpya.

Pia ni changamoto zipi naweza kuzipata na ni jinsi gani naweza kuzitatua kutokana na uzoefu wenu.

Najua wengi kwa harakaharaka kama kawaida yao watasema kwanini sijaenda TRA, jibu ni kwamba jamiiforums ni kama kijiji na nyie ni kama ndugu hivyo inarahisisha zaidi process kwa kutumia uzoefu wa wadau.

Naombeni mchangie mawazo yawe faida kwangu na hata kwa wengine kwa sasa ama hapo baadae.

Nawasilisha!!!
 
Back
Top Bottom