Hii kazi ni ya Siku moja tena haifikishi hata masaa matatu kwa airtel nenda kwenye airtel shop yao ambayo iko jirani na wewe uhakikishe uwe na tin, leseni ya biashara kitambulisho cha uraia ,barua kutoka serikali ya mtaa na passport size picha moja ukitoka hapo nenda makao makuu ya voda wako bagamoyo road acha documents hizo hapo juu kama hazijagongwa mhuri wa mwanasheria watakutoza 15000 kwa ajili ya huduma hiyo ukimaliza voda pitia haloshop ipo mbele ya vodacome kama unaelekea Victoria/ makumbusho acha detail ukimaliza hapo nenda makumbusho tigo shop watakupa no ya wakala mkuu kulingana na unapofanyia biashara yako ukitoka tigo unaingia ttcl wako pale sayansi kijitonyama ukimaliza hapo unarudi hapa zantel wapo shopez napo unaacha detail nadhan kwa Siku utatumia masaaa 2-matatu na hiyo mitandao 6 nadhan ndio inayofanya huduma ya kutoa pesa hapa nchini? Ila kwa taadhari kuwa na angalau balance ya 70000 unapokua unapeleka hizo document maaana chochote kinaweza kutokea