Msaada namna ya kutoa mimba bila kupata madhara kiafya

nimesikitishwa sana na thread yako.na si kweli kuwa unampenda huyo demu wako.kwanza elewa kuwa kutoa mimba ni uuaji.bila kujali kama hiyo mimba ni ya nusu saa,au ya wiki mbili au ya miezi tisa.huo ni uuaji.na sababu uliitoa ya kutaka kutoa hiyo mimba si ya msingi.hebu fikilia kama je wakti wa process ya kuitoa hiyo mimba ikatokea akafariki.je utasikitika?au je utafurahia?KAMA KWELI UNAMPENDA NA KAMA KWELI ITATHIBITIKA KUWA ANA MIMBA.MIMI NAKUSHAURI USIWE NA MAWAZO YA KUITOA HIYO MIMBA.bwana mambo ya siku hizi inawezekana ana yai hilo hilo moja tu na akiitoa hiyo mimba hapati tena mtoto ktk maisha yake.
 
Mmmh...Ndugu yangu naomba uachane na hayo mawazo ya kutoa mimba..Jamani watu wanatafuta watoto hawawapati.. Nyie Mungu kawapa Baraka hiyo halafu mnataka kutoa mimba...! Hata kama mlikuwa hamjapangia kuzaa hilo suala la kutoa mimba kwa kweli siwashauri kabisaaa..
 

Well noted!.Thankx
 

Thankx,jf ndo jibu halis,nimefarijka sana!,what iz the way foward?
 

Hilo ulilofikiria ni zaidi ya haya unayoleta hapa
Suala la kuwa heshima kwa mama mkwe itashuka kwa kuwa binti yake kapata mimba sidhani ndio likufanye ufikirie kutoa mimba
Limekwisha tokea na mimba ipo je heshima ni muhimu kama hicho kiumbe ambacho unatarajia ukitoe
Ndoa sio pesa mkuu kama wewe ni mkristo nenda kanisani kwako waambie aise mambo yamekuwa haya nataka mtoto wangu azaliwe kwenye ndoa sidhani kama watakuambia nenda kajiandae ufanye harusi kubwa ya gharama
Sana sana watakuambia we njoo ujeumalize mambo yako haraka
Nahata kama huna kazi mkuu sidhani kama hilo ni suluhisho
Iache mimba ikue na naamini unapambana kuyaweka maisha sawa na hapo kati kati unaweza ukapata kazi
Je ukiitoa mimba na kesho ukapata kazi utamlaumu nani mkuu
 
buStani ikimwangiliwa vizuri lazima ikue babaaa, sa we kama haMtaki kuzaa si mgetumia kinga? kama hiyo haitoshi kuna kitanzi,vidonge vya majira,sindano njia za asili za kuzuia vyote hivyo mmeshidwa? jamani embu mwacheni zitto kabwe na spika wa baadae akue.TAFADHALI MSIMTOE aje afurahie ulimwengu wa digital na yeye.
 

Elezeeni ukweli kwa wazazi na kwamba mko tayari kuoana. Kama mko Arusha na mmoja wenu amesomea uhasibu kuwasaidia nitamtafutia sehemu ya kufanyia "internship" ili tuu msikiue hicho kiumbe.
 

Huyu Mungu sijui kwa nini tunapenda kumuweka majaribuni, kwa nini huyu Mungu asikusaidie kwa kumletea kifo huyo mpenzi wako umpendae wakati anakiua hicho kiumbe ambacho mmekipata wakati wa furaha yenu? Jamani huyu Mungu walau angenisikiliza tu kwa ombi hili moja na akawasamehe hata wale waliochoma makanisa kule Zanzibar lakini akajibu ombi hili.
 
Angalia sana ndugu yangu hakuna kitu kibaya kama kutoa mimba kwasababu eti hujajipanga kimaisha hujui Mungu kakupangia nini wewe inawezekana kabisa Mungu kakupa mtoto mmoja tuu na ndiyo huyo unafikiria kumuua kisa eti hujajipanga, utajipanga lakini yawezekana usipate tena mtoto. kutoa mimba kuwe kwasababu za kitabibu na siyo sababu dhaifu kama hii.
 

Thanks kuluthumu kwa ushaur wako,nmekupata!
 
Elezeeni ukweli kwa wazazi na kwamba mko tayari kuoana. Kama mko Arusha na mmoja wenu amesomea uhasibu kuwasaidia nitamtafutia sehemu ya kufanyia "internship" ili tuu msikiue hicho kiumbe.

thankx ndachuwa kwa good advice!
 
But haijampa madhara yeyote yale hadi sasa yuko kawaida. zaid na zaid nifanyeje wakuu?
 
Kwa nza haujathibisha kama hiyo ni mimba kwa vile haujaenda kufanya testing. Lakini hata ikiwa ni mimba kweli sikushauri uitoe kwa sababu
  1. Unaweza kusababisha kupoteza maisha ya mama
  2. Unaua kiumbe kisicho na hatia
  3. Against human right
  4. Huenda huyo ni mtoto pekee uliyepangiwa
  5. Wapo wanaohangaika kila hospitali kupata mtoto na hawapati
  6. Wapo wanaotamani japo mtoto wa kusingiziwa
  7. ...
 
mi naamini ukimuomba mungu atakusaidia, na si kumuudhi kwa kutoa mimba, mfano, mie nina mtoto, na ni huyo huyo unayemuita wa bahati mbaya, coz nilidu siku mbovu kikaitika, ila sikuwaza kutoa mimba kwani nilijua roho hiyo itanitesa maishani, na sikuwa tayari, nilichoamua ni kulea mimba na baadae mtoto. amesha zaliwa ana miezi 8, nampenda ni wa kiume,kumbuka matatizo ndo kipimo cha akili, funga mkanda vaa uhusika, tafuta kazi/maisha nina uhakika kama uko serious mungu atakubariki utapata kazi, mwambie mungu '' baba nina nia, sitaki kuua, nibariki nipate kazi, nioe, nitunze familia'', naamini atakusikia , na ndani ya miezi 6, utakuwa umepata kazi, umejipanga sawa sawa na mwezi wa 7 utaoa, we jaribu utanipa majibu. na mwezi wa9 katoto ka kiume mtazaa. amini nimekutabiria, fanya utaweza. ila usichague kazi. demu wako kamaliza chuo, mwambie atafute hata kitempo cha kufundisha kama kazi zimekuwa ngumu. ila usiue ni dhambi.
 
Kaka wewe ni shahid kuwa kila sku MMU watu wanaomba ushauri hawana nguv za kiume, wengne hawana watoto na hata mtaani kwenu pia!!
Jua kuwa wadogo zake wataja lilia kaka/dada yao af mseme mnawangiwa kumbe kumbe damu na dhambi inawatafuna
hizo ndo challeng zenyewe katka maisha we ulifkili ni zipi au kwa wengine tu! pigana mtoto wakiume zamu yako !kama kutoa mimba ndo solution basi hata usihangaikie kutafuta kazi nenda kwa mganga akupe utajiri ili uue ndug yako ili wewe u survive na mkeo maana unalike shortcurt solution!!
Kama unampenda utamlinda!!
 

mnyongeni asante sana kwa ushauri wako wenye mfano hai mungu akuzidishie siku nyng za maisha yako.Thanks much madam.Yaan nmefarijka sana na yeye wif yako amefarjka sana,ninaye hapa hapa anapitia kila post inayoingia hapa.
 

Thankx much bro Goddy na mungu akubariki
 

Ungekuwa una heshima usingejiingiza kwenye uzinifu nje ya ndoa. Vuna ulichopanda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…