Mkuu bado unaendelea na huu mradi wa maji ya kuvuna
Binafsi nimechimba kisima cha futi 16 urefu na futi 16 upana; nina miaka 3 mvua zinakutana. wakati wa kujenga hakikisha unatumia water proof, na cement ya kutosha, mimi nimetumia tofali "6. Nimefunga sim tank 5000lts juu, maji yanapanda kwa automatic pump, na kisha yanateremka kwa gravity. Nayatibu maji kwa kuweka water guards za kutosha, na sijapata tatizo lolote. kutegemeana na fundi,nilitumia kama 4-6 milioni, na sitarajii kujiunga na dawasco labda waseme mvua hakuna miaka miwili mfllizo. Ukitaka shule zaidi google rain water harvesting and treatment; nilipata shule nzuri toka Australia.