Msaada, naona haki haijatendeka

Msaada, naona haki haijatendeka

Wa Igima

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2014
Posts
376
Reaction score
110
Habari Wana JF,

Adhabu inasemaje kwa mtu ambaye amekamatwa na baadhi ya vitu vya wizi. Je, anatakiwa kulipa vyote au kurudisha hivyo alivyo kamatwa navyo?

Kisa kipo hivi, kuna mtuhumiwa alikamatwa na vitu vya wizi ye akadai aliuziwa lakini ushahidi ulikuwa unaonesha aliiba kesi ilikuwa ni ya kuvunja na kuiba.

Hukumu ilitoka hivi, mtuhumiwa kwenda jera miezi sita au kulipa faini ya shilingi elfu hamsini na mshitaki alirudishiwa baadhi tuu ya vitu vilivyo patikana lkn siyo vyote. Vitu vyote kwa ujumla vilikuwa na thamani ya milioni moja na nusu na case ilikuwa mahakama ya mwanzo.

Swali: Je, haki kweli imetendeka hapa? Na nikifungu gani kimetumika kutoa hukumu ya hivi?

Kama mshitaki nitumie njia ipi ili haki itendeke.

Msaada tafadhari.
 
karibuni wazee wa sheria mtoe msaada
 
Pole mkuu! Ila hukumu huwa inategemea na mahakama iliridhika vipi na ushahidi uliotolewa! Na pia kosa halisi alilotiwa hatiani muhusika! Mfano hapo kuna mambo matatu umeyasema kuhusu sakata hilo:
1.kuvunja nyumba
2.Kuiba vitu vyenye thamani ya 1.5
3.Kununua vitu vya wizi
Sasa hapo iwapo mahakama itajiridhisha kuwa mhusika hakuiba vitu, bali aliuziwa na mtu mwingine, hapo hukumu yake ni tofauti na mtu aliyetiwa hatiani kwa makosa hayo mengine ya kuvunja na kuiba vitu hivyo.
Pia ili mhusika alipe vitu vyote panahitajika pia kuthibitisha kwanza kuwa ni kweli ulikuwa mmiliki halali wa vitu hivyo vyote, hapo uonyeshe risit za manunuzi. Pia ithibitike pasipo shaka kuwa ni yeye aliiba vitu hivyo vyote, hapo ndipo mahakama inaweza kumtia hatiani kurudisha vitu hivyo vyote.
Pia lazima ieleweke kuwa kesi ya kumshtaki mtu kama mwizi ni tofauti na kesi ya kumshtaki mtu, kumdai akulipe alichokuibia!
Hivyo nakusihi kama bado una madai unayoweza kuyathibitisha , basi tafta mwanasheria akushauri nini cha kufanya katika rufaa utayoikata!
Wanasheria mnaweza kuongezea hapa.
 
habari.wana jf

Adhabu inasemaje kwa mtu ambaye amekamatwa na baadhi ya vitu vya wizi.je anatakiwa kulipa vyote au kurudisha hivyo alivyo kamatwa navyo?

kisa kipo hivi, kuna mtuhumiwa alikamatwa na vitu vya wizi ye akadai aliuziwa lakini ushahidi ulikuwa unaonesha aliiba kesi ilikuwa ni ya kuvunja na kuiba.

hukumu ilitoka hivi, mtuhumiwa kwenda jera miezi sita au kulipa faini ya shilingi elfu hamsini na mshitaki alirudishiwa baadhi tuu ya vitu vilivyo patikana lkn siyo vyote. Vitu vyote kwa ujumla vilikuwa na thamani ya milioni moja na nusu na case ilikuwa mahakama ya mwanzo.

swali je haki kweli imetendeka hapa? Na nikifungu gani kimetumika kutoa hukumu ya hivi?

kama mshitaki nitumie njia ipi ili haki itendeke.

Msaada tafadhari.
Taaja baadhi ya vitu vilivyoibiwa tupate thamani
 
Pole mkuu! Ila hukumu huwa inategemea na mahakama iliridhika vipi na ushahidi uliotolewa! Na pia kosa halisi alilotiwa hatiani muhusika! Mfano hapo kuna mambo matatu umeyasema kuhusu sakata hilo:
1.kuvunja nyumba
2.Kuiba vitu vyenye thamani ya 1.5
3.Kununua vitu vya wizi
Sasa hapo iwapo mahakama itajiridhisha kuwa mhusika hakuiba vitu, bali aliuziwa na mtu mwingine, hapo hukumu yake ni tofauti na mtu aliyetiwa hatiani kwa makosa hayo mengine ya kuvunja na kuiba vitu hivyo.
Pia ili mhusika alipe vitu vyote panahitajika pia kuthibitisha kwanza kuwa ni kweli ulikuwa mmiliki halali wa vitu hivyo vyote, hapo uonyeshe risit za manunuzi. Pia ithibitike pasipo shaka kuwa ni yeye aliiba vitu hivyo vyote, hapo ndipo mahakama inaweza kumtia hatiani kurudisha vitu hivyo vyote.
Pia lazima ieleweke kuwa kesi ya kumshtaki mtu kama mwizi ni tofauti na kesi ya kumshtaki mtu, kumdai akulipe alichokuibia!
Hivyo nakusihi kama bado una madai unayoweza kuyathibitisha , basi tafta mwanasheria akushauri nini cha kufanya katika rufaa utayoikata!
Wanasheria mnaweza kuongezea hapa.
asante kwa mchango
 
Back
Top Bottom