Msaada: Nasumbuliwa na tatizo la moyo

Unasumbuwaliwa Na panic atack

Hilo tatizo limeshanipata Mimi

Na kizuri zaidi uo sio ugonjwa apana Bali Na matatizo ya saikolojia tu

Mtu unafikiri kuwa ni mgonjwa kumbe wapi
Ebu njoo pm
 
Pole,
Unaishi mkoa gani? Ulipo unawezapata asali ya nyuki wadogo(nyuki wapore?)

Itafute asali ya nyuki wadogo uwe unatumia kijiko kimoja mara2 kwa siku huku unatumia ndizi mbivu mara kwa mara na kujitahidi kupunguza msongo wa mawazo.

Ukizingatia hayo utaishi kama wenzako
 
Shukrani mkuu,nipo Arusha
 
Amini utapona na afya yako itarudi sawa
 
Pole sana mkuu,
Muhimu
jitahidi kuepuka stress zisizo za lazma .. vilevile usiruhusu mishtuko isiyo ya lazma ( panic shocks)
Kama ni mtu wa ibada, jitahidi kujichanganya na wenzio, usiwe mpweke! Ukiwa na tatizo la moyo ,one of best solution ni kuepuka msongo wa mawazo.
 
Check your cholesterol level, kama ipo juu tuanzie hapo kwanza!
 
Pole sana gentleman. Halafu usiweke akilini sana kwamba unaumwa hiyo itaharibu psychology yako... Pia kama unaweza tafuta kitabu kinaitwa “ The power of your subconscious mind” utakuja kunishukuru baadae.
 
Kumbe huwa una mawazo mazuri tu ila huwa unajitoaga akili, umemshauri vema na ni wazi kuwa mawazo yanampelekesha.
 
Dah polee sana mkuu utapona tu Kikubwa Muombe Mungu na je baada ya kutumia dawa kwa miezi kadhaa bado moyo unaendelea kuvuta au hali imetulia now?
 
Pole sana kiongozi Mwenyezi Mungu atakuponya , hizo dawa za kienyeji ulizozitumia ni dawa mkuu?
 
Mkuu kikubwa ni maombi hakuna linaloshindikana juu ya maombi...

Nikupe historia fupi ya matatizo yangu yaliyonikutaga kipondi cha miaka kadhaa iliyopita

Kipindi nipo form 3 njia ya kwenda shule ilikuwa lazma nipandishe mlima, ni ilikuwa ndo njia yangu ya kila siku,kuna siku ghafla tu nikakuta nimepandisha mlima kufika juu nikaanza kusikia moyo unaenda kasi mapigo ya moyo nayasikika mpaka masikioni hali ile ilinitisha kwa kweli, siku ya pili ikawa hvyo hvyo pia ikabidi nipate wacwac sikusema home, siku ya tatu maeneo ya moyo nikaanza kusikia maumivu makali sana mpk ikabidi nianze kuwaambia nyumban nikajua labda yatapita nikanunua panadol lkn yale maumivu hayakukata wiki nzima na yalikuwa makali ikabidi niende hospital doctor akanipa dawa akasema kwamba sometime mishipa ya moyo huwa inabana na kushindwa kufanya kaz vzur, akanipa dawa nikaanza kutumia dawa zikaisha hali ilizidi kuwa mbaya nikarud hospitali nikapewa nyingine nazo zikaisha pasipo mafanikio hali ikawa mbaya zaidi nikawa siwez kukimbia, kuinama, kubeba kitu kizito, maumivu ya moyo kama kuna kitu ndani ya moyo alafu moyo una tight usiku nikilala pumz nakosa, kwa dalilo zote nilizonazo nilikuwa nikifuatilia mitandaoni nakuta ni HEART ATTACK pamoja na MOYO KUTANUKA nikasema maisha yangu sindo yanaelekea mwishoni ukifikiria moyo ndo engine, ikabidi niende hospital nyingine zaidi ya 3 (sikupata wazo la kwenda kwa dactari bingwa wa moyo) nilikuwa naenda hospital tu hizi za kawaida, nilipima vipimo vyoote kwa upande wa damu ,vidonda vya tumbo na vinginevyo, ikafika kipindi nilipewa mpaka vidonge vya kupunguza mawazo wakasema huenda labda nina mawazo, vidonge vya vidonda vya tumbo nilitumia sanaaa ingawa nilionekanaga sina ila madactar walikuwa wanasema kwamba sometime vidonda vya tumbo huwa havionekani ila dawa zote ziliisha lakn wapi ugonjwa uko palepale kifo nilikuwa nakuona mbele yangu, sikuwao kupima kipimo chochote cha moyo ila nilijua 90% kwamba hili tatizo ni la moyo, hapo ni ndani ya mwaka mzima, mara ya mwisho nikaenda hospital moja hivi hapa mjini nikamuelezea doctor hali yote niliyopitia pamoja na dawa zoooote nilizotumia doctor akabaki kaduwaa ndo alipozidi kunitisha kabisa sababu niliona kwamba doctor mwenyewe ameshakata tamaa na tatzo langu, akaniambia "Nakupiga x ray kama hakutoonekana tatizo lolote nitakuandikia rufaa uende kwa madactari bingwa wa moyo" kiufupi nilikata tamaa nikaona maisha yangu yanaelekea mwishoni sababu mpaka inafika hatua ya kupelekwa huko it mean kwamba shida niliyonayo ni kubwa. PAMOJA NA UANAUME WANGU NILILIA SITOSAHAU.....majibu yalitoka ya X ray kwamba hakuna tatizo hvyo inabidi nipewe rufaa ikabidi nirudi nyumban, nikasema hapa hakuna msaada uliobaki isipokuwa ni Mungu pekee, nikawa naenda shule nikirud napita kanisani kwenye ibada za jion, kule kwenye rufaa nikaachana nako nilibaki tu na dawa baadhi ndo nikawa nazitumia tu ilimrad ziishe kisha Mungu ajue hatma ya maisha yangu. Basi nilienda kanisani nikawa nako naanza kukata tamaa ila nikawa najipiga moyo konde, siku ambayo haikujulikana niliamka zangu asubuh kwa ajili ya kwenda kumuomba Mungu juu ya hili tatizo langu nilipofika kanisani nikaomba nikarudi nyumbani nikalala, asubuh yake nikaamka nikaona mbona kama ile hali siisikii , sikuamini nikatoa nguo nifue nikaona nikofit maana nilikuwa siwez hata kufua ,nilikuwa nafuliwa . Tangu siku hyo mpaka leo huu mwaka wa 8 silisikii tena hilo tatzo Ni Mungu pejee aliyenisaidia mpaka kufikia hapa.
MUOMBE MUNGU ANATENDA KWA WAKATI WAKE
 
Mkuu umeshapata uponyaji ondoa wasiwasi na mawazo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…