Msaada: Nasumbuliwa na tatizo la moyo

Msaada: Nasumbuliwa na tatizo la moyo

Mkuu kikubwa ni maombi hakuna linaloshindikana juu ya maombi...

Nikupe historia fupi ya matatizo yangu yaliyonikutaga kipondi cha miaka kadhaa iliyopita

Kipindi nipo form 3 njia ya kwenda shule ilikuwa lazma nipandishe mlima, ni ilikuwa ndo njia yangu ya kila siku,kuna siku ghafla tu nikakuta nimepandisha mlima kufika juu nikaanza kusikia moyo unaenda kasi mapigo ya moyo nayasikika mpaka masikioni hali ile ilinitisha kwa kweli, siku ya pili ikawa hvyo hvyo pia ikabidi nipate wacwac sikusema home, siku ya tatu maeneo ya moyo nikaanza kusikia maumivu makali sana mpk ikabidi nianze kuwaambia nyumban nikajua labda yatapita nikanunua panadol lkn yale maumivu hayakukata wiki nzima na yalikuwa makali ikabidi niende hospital doctor akanipa dawa akasema kwamba sometime mishipa ya moyo huwa inabana na kushindwa kufanya kaz vzur, akanipa dawa nikaanza kutumia dawa zikaisha hali ilizidi kuwa mbaya nikarud hospitali nikapewa nyingine nazo zikaisha pasipo mafanikio hali ikawa mbaya zaidi nikawa siwez kukimbia, kuinama, kubeba kitu kizito, maumivu ya moyo kama kuna kitu ndani ya moyo alafu moyo una tight usiku nikilala pumz nakosa, kwa dalilo zote nilizonazo nilikuwa nikifuatilia mitandaoni nakuta ni HEART ATTACK pamoja na MOYO KUTANUKA nikasema maisha yangu sindo yanaelekea mwishoni ukifikiria moyo ndo engine, ikabidi niende hospital nyingine zaidi ya 3 (sikupata wazo la kwenda kwa dactari bingwa wa moyo) nilikuwa naenda hospital tu hizi za kawaida, nilipima vipimo vyoote kwa upande wa damu ,vidonda vya tumbo na vinginevyo, ikafika kipindi nilipewa mpaka vidonge vya kupunguza mawazo wakasema huenda labda nina mawazo, vidonge vya vidonda vya tumbo nilitumia sanaaa ingawa nilionekanaga sina ila madactar walikuwa wanasema kwamba sometime vidonda vya tumbo huwa havionekani ila dawa zote ziliisha lakn wapi ugonjwa uko palepale kifo nilikuwa nakuona mbele yangu, sikuwao kupima kipimo chochote cha moyo ila nilijua 90% kwamba hili tatizo ni la moyo, hapo ni ndani ya mwaka mzima, mara ya mwisho nikaenda hospital moja hivi hapa mjini nikamuelezea doctor hali yote niliyopitia pamoja na dawa zoooote nilizotumia doctor akabaki kaduwaa ndo alipozidi kunitisha kabisa sababu niliona kwamba doctor mwenyewe ameshakata tamaa na tatzo langu, akaniambia "Nakupiga x ray kama hakutoonekana tatizo lolote nitakuandikia rufaa uende kwa madactari bingwa wa moyo" kiufupi nilikata tamaa nikaona maisha yangu yanaelekea mwishoni sababu mpaka inafika hatua ya kupelekwa huko it mean kwamba shida niliyonayo ni kubwa. PAMOJA NA UANAUME WANGU NILILIA SITOSAHAU.....majibu yalitoka ya X ray kwamba hakuna tatizo hvyo inabidi nipewe rufaa ikabidi nirudi nyumban, nikasema hapa hakuna msaada uliobaki isipokuwa ni Mungu pekee, nikawa naenda shule nikirud napita kanisani kwenye ibada za jion, kule kwenye rufaa nikaachana nako nilibaki tu na dawa baadhi ndo nikawa nazitumia tu ilimrad ziishe kisha Mungu ajue hatma ya maisha yangu. Basi nilienda kanisani nikawa nako naanza kukata tamaa ila nikawa najipiga moyo konde, siku ambayo haikujulikana niliamka zangu asubuh kwa ajili ya kwenda kumuomba Mungu juu ya hili tatizo langu nilipofika kanisani nikaomba nikarudi nyumbani nikalala, asubuh yake nikaamka nikaona mbona kama ile hali siisikii , sikuamini nikatoa nguo nifue nikaona nikofit maana nilikuwa siwez hata kufua ,nilikuwa nafuliwa . Tangu siku hyo mpaka leo huu mwaka wa 8 silisikii tena hilo tatzo Ni Mungu pejee aliyenisaidia mpaka kufikia hapa.
MUOMBE MUNGU ANATENDA KWA WAKATI WAKE
Hili nalo naamini ni tatizo pia
20220423_074941.jpg
 
Mkuu Nina ndugu yangu wa damu ana matatizo Kam haya naomba kujua dawa za kienyeji ulizo tumia mkuu samahani lakini.
 
Pole sana mkuu, kwanza ondoa hofu hio ndio sayansi ya kwanza ya tiba kwenye kupona ufuatilie kitu kinaitwa Epigenetic
Pili tatizo lako chanzo chake hakikutibiwa that's why unapoteza muda kwenye conventional medicines. Sababu kubwa ya magonjwa ya moyo (coronary heart diseases) ni high amount of cholesterol in the blood ambayo inazuia damu isizunguke ipasavyo had mwishowe inasababisha build up of plague yaani kuta za mishipa ya damu kuziba. Mbaya zaid kuna mishipa midogo sana (veins) kwenye moyo hivyo ikishaziba damu inapita kwa shida sana pia kutokana na sababu hii inatrigger clotting factors kuinitiate clotting damu inaganda sasa ni ngumu sana kupata mzunguko mzuri wa damu hapa ndio utaanza kupata dalili za miguu au mikono kufa ganzi, kuchomachoma, kichwa kuuma hasa maeneo ya mishipa ya pembeni karibu na macho.
 
Hatua za haraka zakufuata ni hizi,
Kwa imegency unatakiwa uwe na Aspirin ndani kwako 24hrs ukiona hali inakuwa mbaya utumie 1 tablet hii inasaidia kuyeyusha damu na hivyo kukuepushia chance ya kupata stroke au heart attack, mara nying hutokea wakati wa asubuhi hivyo ni vizuri uimeze usiku kabla ya kulala au pindi unapojisikia vibaya kwa dalili kama vishipa ya kichwa kuuma, miguu kufa ganzi, kuto kuona vizuri
Hatua ya pili Lazima ubadilishe Diet yako (mlo) hii ndio sehemu muhimu sana
Sababu kuu ya magonjwa mengi ya moyo ni high cholesterol, hyperlipidemia yaani mafuta mengi jamii ya saturated fat, mafuta yaliyonatabia yakuganda na ni mazito.
List hii ya vyakula usitumie
1. Mafuta hata tone moja lisiwekwe kwenye chakula Chako
2.chumvi hata isiwekwe kabisa kwenye msosi wake
3.Sukari usitumie kabisa utaipata kwenye matunda
3. Kahawa, sio nzuri inapandisha pressure
4 vyakula vilivyokobolewa mfano wali huu tuliozoea mweupe, chapati, maandazi, vitumbua,mkate n.k
5vyakula vilivyosindikwa kwa sababu vinakuwa na free radicals nyingi

Vyakutumia kwa wingI
1.Mboga za majani (super greenfood) kwa sababu zina madini, essential phytonutrients na antioxidant kwaajili yakuondoa hizo free radicals na kupunguza cholesterol pia kizuri zaid kusaidia cell kujijenga upya hasa Mboga muhimu ni spinach, cerely na kale kazitafute japo zinakuwa adimu sana
2 Matunda ya aina zote muhimu sana ni Zabibu kwasabu inasaidia blood, circulation kutokana na uwepo wa nitric oxide production initiator, parachichi usitumie mpak utakapo kaa vizuri kabisa
3Whole food vyakula vizivyokobolewa mfano magimbi, viazi, maharage, mchele wa njano, mahindi tena ukipata yale ya njano inakuwa poa sana
 
Pia utumie vitamin E vidonge kavitafute ni Antioxidant nzuri sana na inazuia damu kuganda pia inapungua cholesterol kwa usalama zaid tofauti na statins ambazo side effects zake ni kubwa for long term use ,pia utafute vidonge venue vit B6 na B12 ni nzuri kwa afya ya moyo na damu.
Bila kusahau kunywa maji mengi sana na kuacha kunywa soda
Karanga usitumie kwanza kutokana na hali yako chskukazania ni hivyo vitu
TAFADHALI HUU NI USHAURI TU NASIO MBADALA WA MATIBABU YAKO, SIO MBADALA WA USHAURI WA DAKTARI WAKO
 
Pia usinywe maziwa, usile samaki na nyama kwa sababu ya saturated fats( mafuta mabaya yenye kuganda) wengi watashaangaa had samaki ila ukweli ndio huo, kuna aina ya samaki ambao want omega fatty acid imezoeleka kama mafuta ya samaki kitaalamu unashauriwa uyapate kutoka kwenye vyakula jamii ya mbegu japo sio mbaya ukawa na omega 3 fish oil na ni powerful kuondoa cholesterol
Onyo!! Unapotumia vitE + omega 3 fish oil usijetumia na Aspirin kwa sababu zote huyeyusha damu hivyo inaweza kupelekea severe bleed yaani kuvuja damu kwa wingi
Bila kusahau mazoexi madogo kama kukimbia kwa wastani, wanaita cardioexercises sio kubeba vitu vizito
 
Usiwe na shaka utapona na kuwa sawa, hatua ya kwanza nenda Jakaya pale Muhimbili Muone mkurugenzi kwa Sasa ni Dr. Kisenge ni mtu mwema sana atakusaidia.
 
Hope mko poa. Miaka ya nyuma Kama 10yrs ago wakati wa utoto, nilipenda sana kucheza Mpira, nilipokuwa nakimbia Sana nilikuwa nasikia Kama Kuna kitu kinabana kwenye moyo afu kinaacha Basi nikawa nachukulia poa, kwa kua haikunizuia kufanya kazi zangu za kila siku.

Miaka ilienda nkawa Kama muda mwingine napumbua kwa shida yaani hewa inabana na kuachia, mie nilichukulia poa kwa kua haikuwa serious, nilikuwa nadhani labda Nina nyama kwenye pua maana na mother yangu pua take zilikuwa zinabana.

Lakini siku moja moja nilikuwa na experience Kama mapigo ya nguvu ya moyo, mie nachukulia poa, nilikuwa nachukulia poa kwa sababu nilikuwa siumwi chochote, afu nilikuwa busy na kusoma hizo miaka.

Mwaka 2020 mwishoni nilikuwa nafanya mapenzi na demu wangu nkaisi Kama naishiwa pumzi, Basi nili notes kuwa ntakuwa na shida kwenye moyo, nkajipanga kutafuta hela niende hospital kubwa

Mwezi wa pili 2021 kabla sijaenda hospital nilipata mapigo ya moyo yanayoenda mbio kinyama, moyo ulikuwa unadunda Kama utachomoka, Basi moyo ukaanza kuuma yaani nilishituka hatari, Basi nkatafuta hela nkaenda hospital kwa specialist wa moyo.

Nilipima vipimo viwili, electrocardiogram na echocadiogram. Majibu yalikuwa hivi

Valves zote ziko vizuri, Ejection fraction Ni 86% wakati kwa normal heart Ni 75%, Diastolic disyfunctional grade one(I) afu nilikutwa na hypertrophic cardiomyopathy.

Doctor Ali conclude kuwa moyo wangu umetanuka, especially left ventricle (LH) nilikuwa Sina nguvu ata, ATA kunyanyua kikombe nilikuwa siwezi, moyo wangu ulikuwa unauma Sana, nilikuwa naisi kizunguzungu hatari, nilikuwa na difficult I breathing. Na kifua kubana nkitembea haraka au kunyanyua kitu ATA ndoo.

Nilianza dozii ya vidonge vya losartan na lasix. Nilipangwa kuuzulia kriniki kila baada ya wiki mbili, afu Sina bima Sina kazi. Nilimeza vidonge kwa 5months, nkaacha kwenda clinic maana ukienda unapewa vidonge hivyo hivyo na kupimwa pressure.

Badae Kuna watu washawai kupatwa na moyo kutanuka, wakanishauri nitumie na dawa za kienyeji.baada ya mwaka wa kutumia dawa za kienyeji na za hospital ( baada ya 5 months niliacha dawa za hospital nkaanza za kienyeji) haya ndo matokeo.

  • Difficult in breathing imeisha napumua vizuri
  • Nguvu ninazo natembea, sio Kama zamani sema siwezi kukimbia maana moyo utauma
  • Moyo kuuma imeisha, labda nikimbie au kubeba vitu vzito
  • Moyo kwenda mbio imeacha

Matatizo mapya
- yaani siwezi kufanya physical exercise, nkikimbia kidogo moyo utaenda mbie na ku feel uncomfortable

- kufanya mapenzi labda goli moja, sijawa stable

- Tatizo kubwaaaa Ni mkono wa kushoto na bega la kushoto, yaani mkono wa kushoto nkiufanyisha kazi utasababisha niumwe na kifua, na moyo kwenda mbio hatari, upande wa mgongo chini ya bega la kushoto ukifanya kazi kidogo au kubeba vitu vizito, au kufanya mapenzi kwa muda utasikia maumivu uko mgongoni upande wa kushoto.

Kutopona kunanifanya nakuwa na depression hatari mawazo kama yote, na pressure kupanda Mara kwa Mara,

Hapa nilipo Sina amani Wala furaha na maisha,dawa nilizozitumia zimewaponyesha watu wengi ninao wafahamu sahivi wanaendelea na life, Mimi sijui Ni ugonjwa gani huu, mwaka mzima siponi, sijui nimerogwa au Nini, wenzangu niliowakuta hospital kwa tatizo la moyo kutanuka washapona, sio wanyonge Kama Mimi, yaani nkitembea haraka shida, kukimbia shida, kunyanyua kitu kizito shida, ku sex shida khaaa.

Msaada wakuu,
Pole sana ndugu kama unapatikana Arusha nenda hospital ya moyo medcare ipo Arusha kaonane na daktari wa moyo anaitwa Julius onesmo
 
Pole kiongozi pia angalia na vyakula unavyokula pia aina ya mazoezi unayopiga mfano kupiga chuma, punguza chumvi, acha kabisa matumizi ya energy drinks na kahawa ni mbaya Sana weka mbali na watoto.
 
Pia acha mawazo hata kama maisha ni magumu penda kujipa furaha kwa maelezo zaidi inbox [emoji392] me
 
Mawazo ni ugonjwa mbaya sana unasababisha mengine yaongezeke ,mawazo,wasiwasi hupelekea moyo kwenda kasi sanaa,ni vyema kubadili badili hospital madokta wengi ni hovyo
 
nakushauri kitu kimoja kwanza,
Moyo umetanuka doctor amekwambia nini chanzo cha moyo kutanuka,,,
Mimi nilikutana na mambo kama hayo 2014,2015,2016,2017,2018 nimezunguruka kika kona
NIMEPIMA colestral , hb,ECG, valve,
Sukari,presha,Echo...Xray,,
Nikatoka hapo kikaenda clinik za tiba mbadala nikaanzia kwa Abdalah mandai longoni, G,mboto,
Nikaenda Sinza kwa doctor John lupimo
Safari ni ndefu mno ,,matibabu nimepitia ngazi mbali mbali ni mabonde na maporomoko,, inafikia mahala unakata tamaa za maisha kabisa...
Ushauri wangu mdogo wangu,,
Nenda upande wa pili wa shilingi..
Moja,,,
Inawezekana ikawa ni jini
Sihr .....uchawi
Presha ,moyo,sukari,macho
Kichwa kuuma sana,mgongo,upungufu wa nguvu za kiume
Kuumwa na kifua,mbavu ..miguu ,magoti
Wakati mwingine ni michezo ya Kiswahili utapoteza muda na pesa zako nyingi sana
Washirika siku hizi teknolojia yao ipo juu sana..pole sana mdogo wangu..
 
nakushauri kitu kimoja kwanza,
Moyo umetanuka doctor amekwambia nini chanzo cha moyo kutanuka,,,
Mimi nilikutana na mambo kama hayo 2014,2015,2016,2017,2018 nimezunguruka kika kona
NIMEPIMA colestral , hb,ECG, valve,
Sukari,presha,Echo...Xray,,
Nikatoka hapo kikaenda clinik za tiba mbadala nikaanzia kwa Abdalah mandai longoni, G,mboto,
Nikaenda Sinza kwa doctor John lupimo
Safari ni ndefu mno ,,matibabu nimepitia ngazi mbali mbali ni mabonde na maporomoko,, inafikia mahala unakata tamaa za maisha kabisa...
Ushauri wangu mdogo wangu,,
Nenda upande wa pili wa shilingi..
Moja,,,
Inawezekana ikawa ni jini
Sihr .....uchawi
Presha ,moyo,sukari,macho
Kichwa kuuma sana,mgongo,upungufu wa nguvu za kiume
Kuumwa na kifua,mbavu ..miguu ,magoti
Wakati mwingine ni michezo ya Kiswahili utapoteza muda na pesa zako nyingi sana
Washirika siku hizi teknolojia yao ipo juu sana..pole sana mdogo wangu..
Uliponaje ndugu yangu utusaidie na sisi?
 
Back
Top Bottom