Msaada: Natafuta digital camera na printer nzuri kwa ajili ya biashara ya passport size photos

music mimi

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2013
Posts
500
Reaction score
888
Wadau wa technology.

Naomba msaada wa mawazo yenu, najua mpo wenye experience ya kutosha kwenye hivi vifaa.

Nataka kununua digital camera na printer mahsusi kwa ajili ya kazi ya picha za passport.

Nahitaji kwa ajili ya kutoa passport za haraka zile za dakika 3.

Nachoitaji ni kusaidiwa jina la camera & printer (isiyoitaji computer) na bei zake nahitaji yenye bei ndogo kwa ajili ya kuweka stationery au kuzunguka nayo kuwafata wateja.

Ikiwezekana na duka naloweza kuvipata, mimi napatikana dar es salaam kwa sasa.

Natanguliza shukrani.

MM
 
Printer tafuta za Epson andaa kama laki 4 au 6 hapa
Camera tafuta za Sony laki 8 inakuhusu
 
Mkuu mimi nahitaji simple tu kwa ajili ya kazi za stationery mtaani na kupita kwenye mashule na vyuo na vikundi. Hizi bei zako naona kubwa sana mimi nilikuwa napiga hesabu ya laki tatu hadi nne kwa vote...kuna printer niliwai iona sehemu ni ndogo sana inatoa passport photo pekee alafu ni kama portable fulani sema ilikuwa zamani kabla sijapata hii idea yani anaprint hakuweka kwenye PC na picha ikatoka vizuri tu
 
Za bei ya chini ya hapo zipo pia mkuu
 
Bajeti muhimu, kama una simu inayopiga vizuri unaweza uka anza nayo, watu wengi tu wanatumia simu biashara hio. Pia kumbuka simu inapiga picha nzuri kuliko point and shoot camera, ni either unatumia simu ama kama unanunua Camera hakikisha ni Dslr level, ukiweka tu hio keyword jiji ama fb marketplace zitakuja.

Kuhusu printer za passport sina uzoefu nazo, ila kama printer nyengine hakikisha running cost ni ndogo, vyema pitia kwa wahusika wenyewe mtaani watakupa details zaidi ama kama kuna Anayefanya hio kazi humu atakuja.
 
Wadau wa technology.

Naomba msaada wa mawazo yenu, najua mpo wenye experience ya kutosha kwenye hivi vifaa.

Nataka kununua digital camera na printer mahsusi kwa ajili ya kazi ya picha za passport.

Nahitaji kwa ajili ya kutoa passport za haraka zile za dakika 3.

Nachoitaji ni kusaidiwa jina la camera & printer (isiyoitaji computer) na bei zake nahitaji yenye bei ndogo kwa ajili ya kuweka stationery au kuzunguka nayo kuwafata wateja.

Ikiwezekana na duka naloweza kuvipata, mimi napatikana dar es salaam kwa sasa.

Natanguliza shukrani.

MM
Nicheki 0713349984, mimi ni Photographer, napatikana Makumbusho Dar es Salaam
 
Bajeti muhimu, kama una simu inayopiga vizuri unaweza uka anza nayo, watu wengi tu wanatumia simu biashara hio. Pia kumbuka simu inapiga picha nzuri kuliko point and shoot camera, ni either unatumia simu ama kama unanunua Camera hakikisha ni Dslr level, ukiweka tu hio keyword jiji ama fb marketplace zitakuja.

Kuhusu printer za passport sina uzoefu nazo, ila kama printer nyengine hakikisha running cost ni ndogo, vyema pitia kwa wahusika wenyewe mtaani watakupa details zaidi ama kama kuna Anayefanya hio kazi humu atakuja.
Mkuu sio lazima iwe DSLR, kumbuka mtu anabhutaji simple tu.

DSLR hamfanyi photoshoot haitajinhiyo japo inafanya yote hadi passport
 
Chukua Google Pixel, itumie kwa kupiga picha. Pixel unyama saana. Printer vipo vile vidogo portable. Kaulizie kariakoo kwenye maduka ya computer watakuwa nazo.
 
Tafuta portable printer hizi zinatoa picha hadi size ya 5x7 Sasa utajua namna ya kugawanya uweke passport Canon printer zipo ndogo zinazofanya kazi hiyo ila hazitumii wino zinatumiwa cartridge, nakuonya kwa sababu hii kazi ni vyema utafute printer hapo kariakoo Kuna printer za 400k,mpaka 600 mfano ukiingia vizuri utakutana na l805 used utaipata kwa 650 , utakutana na l130 unaweza ipata kwa 400k mpaka 500k, lakini kwa sababu unatakabeinchee tafuta l3250 ni latest printer inauzwa 450 na hii unatumia ink tank achana kabisa na Yale ma portable ya cartridge utaumia na kujilaumu.

Kama uko MOROGORO mjini Kuna duka la kamera la mhindi karibu na round about Kuna Sony compact camera zipo hapo 250 mpaka 300.

Lakini kwa budget Yako nunua printer ya 450 kisha tumia simu Yako kama kameraana hiyo business kwa budget iliyo nayo ni maghumashi,.

Ahsante @chiefmkwawa
 
Hiti itakufaa sana tena ina kiscreen cha kueditia picha hapohapo.
Screenshot_20250617-233430_Google.jpg
 
Bajeti muhimu, kama una simu inayopiga vizuri unaweza uka anza nayo, watu wengi tu wanatumia simu biashara hio. Pia kumbuka simu inapiga picha nzuri kuliko point and shoot camera, ni either unatumia simu ama kama unanunua Camera hakikisha ni Dslr level, ukiweka tu hio keyword jiji ama fb marketplace zitakuja.

Kuhusu printer za passport sina uzoefu nazo, ila kama printer nyengine hakikisha running cost ni ndogo, vyema pitia kwa wahusika wenyewe mtaani watakupa details zaidi ama kama kuna Anayefanya hio kazi humu atakuja.
Mkuu mbona DSRL ni za kiwango cha juu sana, hizo ni za professional photographers na bei yake iko juu. Inaonekana bajeti yake ni ndogo. Kama hawezi kutumia simu basi anunue digital cameras za casual photographers mfano za Nikon, Canon Sony, nk.
 
My point asinunue Digital camera za kawaida yaani point and shoot zimezidiwa quality na simu tayari, either unanunua simu ama unanunua Dslr.
 
Yes kwa kazi yako chukua hit ninayo Kama mpya kabisa...Ila nishahama kwenye hio technology...kwa kutembea inafaa haina wino kumwagika Wala Nini ku print mwisho 4*6
Cartridge yake kila baada ya picha 50 unabadilisha,ila ingekuwa inatoa 5× 7 ingekuwa safi sana
 
Back
Top Bottom